Mkuu mwenyekiti wa JEC, naomba vigezo nilivyoviainisha hapo juu vitumike kuengua jina la NYANI NGABU kwa sababu huyu Bwana: ni mshari, mkorofi, mbabe, ana dharau na mara nyingi husababisha migongano humu ndani kiasi cha kupelekea kupewa BAN (Mheshimiwa Roboti anihukumu kama hajawahi kutoa Ban kwa huyu Bwana)...
Binafsi alishawahi kunitukana na kunidhalilisha kwenye post moja kwa kukosea kuandika kiingereza fasaha hali iliyonifanya nikashindwa hata kutekeleza majukumu yangu ya siku hiyo kutokana na mfadhaiko nilioupata. Kuona NYANI NGABU akipewa sifa za ushiriki wa JF Man of the Year ilhali kuna watu ambao kwa namna moja au nyingine walishawahi kuathirika kutokana na kauli na kejeli zake ni kuikosea heshima jamii ya Wana-JF hao ambao wanaamini kuwa JF ni mahali pa kusaidiana na kuelimishana na siyo kudhalilishana...
JF man of the Year ni shindano ambalo kwa imani yangu litapelekea baadhi ya wana-JF kuiga matendo na kauli za washiriki kwa imani kuwa hao ndiyo vioo vya jamii ya JF ili mwakani nao waweze kushiriki hili shindano kwa kuiga yale yaliyosemwa, yanayosemwa na yatakayosemwa na hawa washiriki. Je kutoka kwa NYANI NGABU tuige/tujifunze jinsi ya kudharau? Kukejeli? Kutukana? Kudhalilisha wengine? Kujisifu hata kwa mambo yasiyo na msingi?
Nitafurahi iwapo mchakato huu utakuwa huru na wa haki kwa kuzingatia misingi yote ya Demokrasia ikiwa ni pamoja na wengi wape na pia wachache waheshimiwe "Majority rule and minority right".. Na kwa kuzingatia hilo basi nitashukuru kusikia kauli yako Mheshimiwa Mwenyekiti wa JEC pamoja na utekelezaji wa niliyoyaainisha kwa manufaa ya JF pamoja na wana_JF wote popote walipo.. Pamoja na yote aliyowahi kunitendea huyu Bwana naomba niweke wazi kuwa sina chuki naye bali nimeamua kuanika wazi mambo yake ili jamii ya wana-JF iweze kuelewa ukweli na kufanya maamuzi ya busara katika harakati hizi za kumpata JF Man of Year 2010.
Nashukuru kwa kunielewa.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Jamii Forums.
TANMO - Tanzania Ni Moja