JF Woman and Man of The Year 2010: Mchakato Wa Kuwapata

JF Woman and Man of The Year 2010: Mchakato Wa Kuwapata

Ni Nani Anafaa Kuwa "JF Man of the Year 2010"?

  • Acid

    Votes: 23 40.4%
  • Kiranga

    Votes: 12 21.1%
  • Nyani Ngabu

    Votes: 22 38.6%

  • Total voters
    57
  • Poll closed .
Mkuu mwenyekiti wa JEC, naomba vigezo nilivyoviainisha hapo juu vitumike kuengua jina la NYANI NGABU kwa sababu huyu Bwana: ni mshari, mkorofi, mbabe, ana dharau na mara nyingi husababisha migongano humu ndani kiasi cha kupelekea kupewa BAN (Mheshimiwa Roboti anihukumu kama hajawahi kutoa Ban kwa huyu Bwana)...

Binafsi alishawahi kunitukana na kunidhalilisha kwenye post moja kwa kukosea kuandika kiingereza fasaha hali iliyonifanya nikashindwa hata kutekeleza majukumu yangu ya siku hiyo kutokana na mfadhaiko nilioupata. Kuona NYANI NGABU akipewa sifa za ushiriki wa JF Man of the Year ilhali kuna watu ambao kwa namna moja au nyingine walishawahi kuathirika kutokana na kauli na kejeli zake ni kuikosea heshima jamii ya Wana-JF hao ambao wanaamini kuwa JF ni mahali pa kusaidiana na kuelimishana na siyo kudhalilishana...

JF man of the Year ni shindano ambalo kwa imani yangu litapelekea baadhi ya wana-JF kuiga matendo na kauli za washiriki kwa imani kuwa hao ndiyo vioo vya jamii ya JF ili mwakani nao waweze kushiriki hili shindano kwa kuiga yale yaliyosemwa, yanayosemwa na yatakayosemwa na hawa washiriki. Je kutoka kwa NYANI NGABU tuige/tujifunze jinsi ya kudharau? Kukejeli? Kutukana? Kudhalilisha wengine? Kujisifu hata kwa mambo yasiyo na msingi?

Nitafurahi iwapo mchakato huu utakuwa huru na wa haki kwa kuzingatia misingi yote ya Demokrasia ikiwa ni pamoja na wengi wape na pia wachache waheshimiwe "Majority rule and minority right".. Na kwa kuzingatia hilo basi nitashukuru kusikia kauli yako Mheshimiwa Mwenyekiti wa JEC pamoja na utekelezaji wa niliyoyaainisha kwa manufaa ya JF pamoja na wana_JF wote popote walipo.. Pamoja na yote aliyowahi kunitendea huyu Bwana naomba niweke wazi kuwa sina chuki naye bali nimeamua kuanika wazi mambo yake ili jamii ya wana-JF iweze kuelewa ukweli na kufanya maamuzi ya busara katika harakati hizi za kumpata JF Man of Year 2010.

Nashukuru kwa kunielewa.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Jamii Forums.

TANMO - Tanzania Ni Moja

TANMO;

JEC imekaa na kuyapitia malalamiko yako na kuyaona kuwa ni ya msingi sana. Pamoja na kuwa mchakato wa kura za maoni ulishapita ambapo hasa pingamizi hili lilitakiwa liwekwe, tumeona ni vema pia tusikilize na upande wa pili wa NN kabla ya kutoa uamuzi wa mwisho.

Mwishoni, kama unaweza ukatuletea ushahidi wa malalamiko unayoyatoa utakuwa umetusaidia sana, na NN atatakiwa kuyatolea maelezo, bila shaka.
 
Max Shimba yumo humu humu, hajaenda popote, fungueni macho mtamuona!
 
Mmewapa somo wagombea kuwa matokeo yakitangazwa hakuna kukataa???
 
TANMO;

JEC imekaa na kuyapitia malalamiko yako na kuyaona kuwa ni ya msingi sana. Pamoja na kuwa mchakato wa kura za maoni ulishapita ambapo hasa pingamizi hili lilitakiwa liwekwe, tumeona ni vema pia tusikilize na upande wa pili wa NN kabla ya kutoa uamuzi wa mwisho.

Mwishoni, kama unaweza ukatuletea ushahidi wa malalamiko unayoyatoa utakuwa umetusaidia sana, na NN atatakiwa kuyatolea maelezo, bila shaka.

Mheshimiwa, Nakumbuka Ushahidi wangu ulifutwa na mamod's ili kurejesha hali ya amani baada ya kutokea malumbano baada ya kukejeliwa na huyu Muungwana.

Ila kimantiki naweza kuwasilisha ushahidi huu hapa:

I am disqualified already. Damn!!!

Lakini pouwa....lazima kuna mtu atanipendekeza kwa ile au zile ID zangu tofauti....

Swali langu ni: Je ninyi wenyewe hamkuliona hili kuwa huyu Bwana mwenyewe anajijua kuwa hafai na bado mkamweka ashiriki shindano?
 
Mheshimiwa, Nakumbuka Ushahidi wangu ulifutwa na mamod's ili kurejesha hali ya amani baada ya kutokea malumbano baada ya kukejeliwa na huyu Muungwana.

Ila kimantiki naweza kuwasilisha ushahidi huu hapa:

Swali langu ni: Je ninyi wenyewe hamkuliona hili kuwa huyu Bwana mwenyewe anajijua kuwa hafai na bado mkamweka ashiriki shindano?

TANMO, nimekusoma.

JEC bado inasubiri maelezo ya NN, baada ya siku tatu kama hakutakuwa na utetezi, JEC itachukua hatua stahili.
 
Back
Top Bottom