Nimesoma bandiko lako na kupitia rejea mbalimbali kuhusiana na mada husika. Niliposikia habari za Mbowe kuwa naye ameombwa na wazee kutangaza nia na kusudio la kugombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), nilipatwa mshangao kwa kuwa nilitegemea CHADEMA kuepusha aina yoyote ya mchuano kati ya Mwenyekiti Mbowe na Tundu Antipas Lissu, lakini kwa kuwa wanasiasa huwa wana trick na malengo tofauti, hiyo haikunisumbua sana.
Japo bado nikawaza iwapo Tundu Lissu atachuana na kumshinda Mbowe katika kura za wajumbe, hii itakuwa na maana gani hata kama CHADEMA haitashinda kiti cha Uraisi?
Nikiangalia na kurejea kwenye historia ya Wagombea wa Urais kutokea CHADEMA kuanzia mwaka 2005 kwa kuwa Uchaguzi mkuu wa 1995 CHADEMA haikuwa na mgombea wa Urais, halikadhalika pia Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2000 pia hawakuwa na mgombea.
Hii ina maana kuwa tangu kuanza UCHANGUZI MKUU wa vyama vingi mwaka 1995 CHADEMA imeshiriki uchaguzi mkuu kwa nafasi ya Urais mwaka 2005, 2010 na 2015.
Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 CHADEMA ilimsimamisha Freeman Aikael Mbowe, ambapo alimaliza nafasi ya tatu akiwa na kuwa kura 668,756 asilimia 5.88% ya kura zilizopigwa.
Mwaka 2010 CHADEMA ilimsimamisha Wilbroad Slaa ambapo ilipata kura 2,271,491 sawa na asilimia 27.05% kutoka asilimia 5.88% ilizopata miaka mitano iliyopita.
Tunafahamu mwaka 2015 chini ya mwavuli wa UKAWA CHADEMA ilimsimamisha Edward Lowassa ambapo ilipata kura 6,072,848% sawa na asilimia 39.97% za kura za URAIS.
Kwa nini nimeanza kwa kueleza haya, ni kwa sababu mara nyingi wachambuzi wa siasa hawapendi kuangalia historia. Wachambuzi wengi hasa hawa vijana wenye ushabiki huwa hawaoni mbali zaidi ya ushabiki wao.
Mazingira na pressure za mwaka wa uchaguzi hufanya watu wengi kutokuona uhalisia wa hali ya kisiasa. Waliosoma Takwimu kuna mambo kadhaa ambayo wameyagundua hapo.
Sasa turudi kwenye kupata mgombea kwa mwaka 2020 ndani ya CHADEMA. Mwaka 2015 hali ya nani agombee urais kwa tiketi ya CHADEMA ilibadilika kwa sababu ya ujio wa Lowassa. Hivyo wengi walikubali kuwa Edward Lowassa anafaa, japo kuna yalizungumzwa nyuma ya pazia, kwa sasa hayo hayana umuhimu sana japo yametuachia somo kubwa.
Wote tunakubaliana kuwa Lowassa alikuwa na mvuto, alikuwa anajulikana, alikuwa anauzika, alikuwa anafahamikabna zaidi sana alikuwa na mtaji wa kuutafuta Uraisi.
Hivyo kujiunga kwake CHADEMA ikawa mtaji kwa Chama na hatimaye kwa UKAWA. Lakini kabla ya ujio wa Edward Lowassa ni wazi kuwa mtu aliyekuwa na nafasi kubwa ya kupata uungwaji mkono mkubwa basi alikuwa Dr. Wilbroad Slaa.
Leo tupo hapa mwaka 2020, na inaonekana wengi walidhani kuwa mgombea angekuwa Tundu ANTIPAS Lissu kwa sababu mbalimbali.
Inawezekana Lissu ndiye mjenga hoja mzuri na mzungumzaji mzuri kuliko mtu mwingine yoyote ndani ya CHADEMA.
Kisiasa wanasiasa wanazidiana katika vipawa na vipaji, wanaweza kuwa wana-itikadi moja, wanaweza kuwa na sera na mipango inayofanana lakini huwa wanakuwa na vipawa tofauti. Rejea Barack Obama na Macron wa Ufaransa.
Kama Mbowe ana nia ya kushindania nafasi ya kugombea Urais kupitia CHADEMA ni wazi kuwa atapata kura za Kamati za Chama na ataweza kupata nafasi hiyo kwa sababu ya historia na nafasi yake ndani ya Chama.
Peter Msigwa na Lazaro Nyalandu, sioni nafasi yao katikati ya Lissu na Mwenyekiti Mbowe. Pia sioni uwezo wao binafsi katika nafasi wanayoitaka. Ni aina ya wagombea wanaotegemea kuuzwa na Chama lakini wao wenyewe wana ushawishi mdogo sana.
Kwa siasa za sasa, unahitaji pia ushawishi binafsi wa mgombea kwenye nafasi ya Urais.
Kwa hali ilivyo na kama Mwenyekiti atagombea hakuna wa kumzuia japokuwa haitawapa mtaji mkubwa sana CHADEMA katika Uchaguzi Mkuu.
Lakini inawezekana pia ni hesabu za mwenyekiti kwa kuwa haijulikani kama Tundu Antipas Lissu anaweza kuwa na sifa za kukubalika kugombea nafasi hiyo kutokana na mambo kadhaa.