Jicho ndani ya habari: Waandishi wa habari hawajawatendea haki wananchi kwa kutochambua bajeti kuanzia bungeni hadi mtaani, wamjadili Mbowe

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,885
Bajeti za Afrika Mashariki zilisomwa kwa pamoja siku ya Alhamisi lakini magazeti na vyombo vya habari vya Tanzania havijajadili bajeti ya mtanzania bali kuanzia bungeni hadi mtaani mjadala ukuwa wa mbowe na masihala na mjadala wa bajeti unaohusi maisha ya watanzania ukawekwa kapuni.

Kwa nchi za Kenya na Uganda vyombo vyao vilijikita kwenye bajeti na kuangalia inamanufaa gani kwa mataifa yap na kwa mwananchi wa kawaida na kumpa raia summary ya mambo makuu ya bajeti na ajipange vipi tofauti na kwetu

Mjadala unaendelea Star TV

IMG_20200613_051220.jpg
 
Ukweli ni kuwa bajeti ile ilikuwa ni kampeni ya ccm, kiasi kwamba hakuna mtu yoyote serious anaweza kuifuatilia bajeti ya aina hiyo. Kuna wanaccm wengi humu mitandaoni nimewaambia waone ni jinsi gani ccm inavyoharibu mambo ya msingi, kwa kumsifu Magufuli ndani ya vitu vya msingi. Matokeo yake, hata wanaccm wenyewe wamejikuta hawaijadili tena bajeti, maana haina mvuto kwa watanzania.
 
Jana Paskali Mayalla kuna uzi mmoja tulikutana akasema yeye Ni critic sana wa serikali/Magufuli. Nikamwambia ni critic kweli lakini sio sana. Tena nikwambia ni msifiaji zaidi kuliko mkosoaji. Leo namuona Mosses anamwambia kile kile nilichomwambia jana.
 
Return Of Undertaker,

Tatizo sio waandishi wa Habari, Tatizo ni wananchi wa hizi nchi, kutwa kujadiri mambo yasio ya msingi na Ndo mana kila siku viongozi wanatuendesha watakavyo maana mijadala mingi ni mambo ya kipuuzi.

Hata Moderators wa humu wanachangia, ni kuendekeza threads za kipuuzi tu, Eti sijui pombe sijui joyce mukya sijui watu wa kusifu na kuabudu.

Jana kulikuwa na uzi kuhusu mabadiriko ya sheria kufanya mamlaka za usimamizi wa sehemu zetu za utalii kunyang’anywa mamlaka yao ya kukusanya fedha na nikaelezea ni kwa jinsi gani mapendekezo yale yataua sekta ya utalii. Moderators sijui wameufutilia wapi ule uzi.

Waafrika tunashida kubwa sana no wonder wazungu wanatudharau na kutufanyia vioja.
 
Uko sahihi, lakini naona pia jamii inajadili udaku zaidi. Kwa kawaida uzi haukai front page kwa ubora wake, bali kadiri unavyochangiwa ndio unavyokua juu. Uzi wako bado utakuwa humu humu ndani, lakini hauna wachangiaji. Na tatizo kubwa limetokana na kuua hamasa ya mijadala, na uhuru wa vyombo vya habari. Kwa sasa mada yoyote inayoamsha ufahamu wa wananchi dhidi ya utashi wa serikali hiyo haikubaliki, na mijadala inayoisifu serikali ambayo ndio inayoruhusiwa, haina mvuto kwa wananchi.
 
Magazeti ....vyombo vya habari vingi vinafanya biashara...kwanini nijadili wateja wangu wasichokitaka??

Kisha nimuuzie nani?
 
Return Of Undertaker,

Tatizo sio waandishi wa Habari, Tatizo ni wananchi wa hizi nchi, kutwa kujadiri mambo yasio ya msingi na Ndo mana kila siku viongozi wanatuendesha watakavyo maana mijadala mingi ni mambo ya kipuuzi.

Hata Moderators wa humu wanachangia, ni kuendekeza threads za kipuuzi tu, Eti sijui pombe sijui joyce mukya sijui watu wa kusifu na kuabudu.

Jana kulikuwa na uzi kuhusu mabadiriko ya sheria kufanya mamlaka za usimamizi wa sehemu zetu za utalii kunyang’anywa mamlaka yao ya kukusanya fedha na nikaelezea ni kwa jinsi gani mapendekezo yale yataua sekta ya utalii. Moderators sijui wameufutilia wapi ule uzi.

Waafrika tunashida kubwa sana no wonder wazungu wanatudharau na kutufanyia vioja.
Mbona huo uzi khs TANAPA/NCAA/TAWA jana tumeshaujadili kwa Sana tu boss.
 
Pamoja na ukanjanja wa waandishi wetu lkn kwa hili nawatetea, bajeti gani kila kituo inasifia Magufuli, waandike nini sasa.

Ile ilikuwa ni bajeti ya Magufuli siyo ya wananchi.
 
Bajeti za Afrika Mashariki zilisomwa kwa pamoja siku ya Alhamisi lakini magazeti na vyombo vya habari vya Tanzania havijajadili bajeti ya mtanzania bali kuanzia bungeni hadi mtaani mjadala ukuwa wa mbowe na masihala na mjadala wa bajeti unaohusi maisha ya watanzania ukawekwa kapuni.

Kwa nchi za Kenya na Uganda vyombo vyao vilijikita kwenye bajeti na kuangalia inamanufaa gani kwa mataifa yap na kwa mwananchi wa kawaida na kumpa raia summary ya mambo makuu ya bajeti na ajipange vipi tofauti na kwetu

Mjadala unaendelea Star TV

Aliyekudanganya kuwa Tanzania ya sasa ina Journalists ni nani Ndugu? Tanzania ya sasa ninavyojua ina PR Journalists tu na si Critical Journalists.
 
Ukweli ni kuwa bajeti ile ilikuwa ni kampeni ya ccm, kiasi kwamba hakuna mtu yoyote serious anaweza kuifuatilia bajeti ya aina hiyo. Kuna wanaccm wengi humu mitandaoni nimewaambia waone ni jinsi gani ccm inavyoharibu mambo ya msingi, kwa kumsifu Magufuli ndani ya vitu vya msingi. Matokeo yake, hata wanaccm wenyewe wamejikuta hawaijadili tena bajeti, maana haina mvuto kwa watanzania.
Uko sahihi, lakini naona pia jamii inajadili udaku zaidi. Kwa kawaida uzi haukai front page kwa ubora wake, bali kadiri unavyochangiwa ndio unavyokua juu. Uzi wako bado utakuwa humu humu ndani, lakini hauna wachangiaji. Na tatizo kubwa limetokana na kuua hamasa ya mijadala, na uhuru wa vyombo vya habari. Kwa sasa mada yoyote inayoamsha ufahamu wa wananchi dhidi ya utashi wa serikali hiyo haikubaliki, na mijadala inayoisifu serikali ambayo ndio inayoruhusiwa, haina mvuto kwa wananchi.
Pamoja na ukanjanja wa waandishi wetu lkn kwa hili nawatetea, bajeti gani kila kituo inasifia Magufuli, waandike nini sasa.

Ile ilikuwa ni bajeti ya Magufuli siyo ya wananchi.
Aliyekudanganya kuwa Tanzania ya sasa ina Journalists ni nani Ndugu? Tanzania ya sasa ninavyojua ina PR Journalists tu na si Critical Journalists.
Tumepoteza mwelekeo
Nchi imeharibika kishenzi siku hizi sijui mambo yatakuwaje miaka mingine mitano?
 
Kwa Sasa wanainchi wanajadili na kuchambua hili
 
Dr Mpango kwa zaidi ya saa anasifia Magufuli na kufanya kampeni za ubunge , nani atafuatilia huo ujinga ?
 
Back
Top Bottom