Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
Mbona huo uzi khs TANAPA/NCAA/TAWA jana tumeshaujadili kwa Sana tu boss.Return Of Undertaker,
Tatizo sio waandishi wa Habari, Tatizo ni wananchi wa hizi nchi, kutwa kujadiri mambo yasio ya msingi na Ndo mana kila siku viongozi wanatuendesha watakavyo maana mijadala mingi ni mambo ya kipuuzi.
Hata Moderators wa humu wanachangia, ni kuendekeza threads za kipuuzi tu, Eti sijui pombe sijui joyce mukya sijui watu wa kusifu na kuabudu.
Jana kulikuwa na uzi kuhusu mabadiriko ya sheria kufanya mamlaka za usimamizi wa sehemu zetu za utalii kunyang’anywa mamlaka yao ya kukusanya fedha na nikaelezea ni kwa jinsi gani mapendekezo yale yataua sekta ya utalii. Moderators sijui wameufutilia wapi ule uzi.
Waafrika tunashida kubwa sana no wonder wazungu wanatudharau na kutufanyia vioja.
Bajeti za Afrika Mashariki zilisomwa kwa pamoja siku ya Alhamisi lakini magazeti na vyombo vya habari vya Tanzania havijajadili bajeti ya mtanzania bali kuanzia bungeni hadi mtaani mjadala ukuwa wa mbowe na masihala na mjadala wa bajeti unaohusi maisha ya watanzania ukawekwa kapuni.
Kwa nchi za Kenya na Uganda vyombo vyao vilijikita kwenye bajeti na kuangalia inamanufaa gani kwa mataifa yap na kwa mwananchi wa kawaida na kumpa raia summary ya mambo makuu ya bajeti na ajipange vipi tofauti na kwetu
Mjadala unaendelea Star TV
Ukweli ni kuwa bajeti ile ilikuwa ni kampeni ya ccm, kiasi kwamba hakuna mtu yoyote serious anaweza kuifuatilia bajeti ya aina hiyo. Kuna wanaccm wengi humu mitandaoni nimewaambia waone ni jinsi gani ccm inavyoharibu mambo ya msingi, kwa kumsifu Magufuli ndani ya vitu vya msingi. Matokeo yake, hata wanaccm wenyewe wamejikuta hawaijadili tena bajeti, maana haina mvuto kwa watanzania.
Uko sahihi, lakini naona pia jamii inajadili udaku zaidi. Kwa kawaida uzi haukai front page kwa ubora wake, bali kadiri unavyochangiwa ndio unavyokua juu. Uzi wako bado utakuwa humu humu ndani, lakini hauna wachangiaji. Na tatizo kubwa limetokana na kuua hamasa ya mijadala, na uhuru wa vyombo vya habari. Kwa sasa mada yoyote inayoamsha ufahamu wa wananchi dhidi ya utashi wa serikali hiyo haikubaliki, na mijadala inayoisifu serikali ambayo ndio inayoruhusiwa, haina mvuto kwa wananchi.
Pamoja na ukanjanja wa waandishi wetu lkn kwa hili nawatetea, bajeti gani kila kituo inasifia Magufuli, waandike nini sasa.
Ile ilikuwa ni bajeti ya Magufuli siyo ya wananchi.
Aliyekudanganya kuwa Tanzania ya sasa ina Journalists ni nani Ndugu? Tanzania ya sasa ninavyojua ina PR Journalists tu na si Critical Journalists.
Nchi imeharibika kishenzi siku hizi sijui mambo yatakuwaje miaka mingine mitano?Tumepoteza mwelekeo
Kwanini hali iko hivyo?Aliyekudanganya kuwa Tanzania ya sasa ina Journalists ni nani Ndugu? Tanzania ya sasa ninavyojua ina PR Journalists tu na si Critical Journalists.
Kwanini hali iko hivyo?