Naweza kutumia slp la taasisi au company na nikapigiwa simu nikachukue mzigo wangu au hiyo mizingo italetwa kwenye company au taasisi niliyopo direct..?Cable ilikuja kwa Singapore post,kwenye tracking ilionyesha kwanza ilipita Posta ya Kenya then ndio ikaja posta ya Tanzania.
Cover na tampered screen zimekuja na China post kwenye tracking vyote vya China post vimefika Tanzania na ku clear customs tarehe 8 so vilichukua siku kumi hiyo ya singapore post ilifika tarehe 11.
Posta sikupata shida wamenitumia message tarehe 13 yenye namba, nikafika pale nikamtajia Mmama yule namba niliotumiwa kwenye message ya simu akaniletea mizigo yangu bundled pamoja.Nikamuonyesha KITAMBULISHO Akatafuta vikaratasi vyote nikasign aka verify kwenye computer nikapata mizigo yangu.
Cover iligharimu 1.05 $, wire ni 4.37$, na tampered screen 3.11 (hii ghali kidogo lakini nilikubali tu maana niliyo nunua eBay ilikuja imevunjika )Shipping iligharim ngap.
Kwenye ofisi bidhaa wanakuletea nimeshuhudia kwenye ofisi ya Bro wangu sijui kama wanaenda kila ofisi.Naweza kutumia slp la taasisi au company na nikapigiwa simu nikachukue mzigo wangu au hiyo mizingo italetwa kwenye company au taasisi niliyopo direct..?
Nimekuja hapa kutoa experience yangu ya Aliexpress nadhani labda itawasaidi, sasa tarehe 29 niliamua kujitosa aliexpress maana kuna bidhaa niliziona eBay sema bei ilikuwa juu kidogo sasa nikadownload application yao ya Android, nikasign up (ilichukua dakika chache sana) nikaanza kwa kununua tempered screen protector, cover ya simu, pamoja na cable usb type c to USB ya kawaida (maana Dar nzima nimeikosa).
Sema ukweli nimepapenda aliexpress maana kwanza wanapayment system yao wenyewe ya Alipay haina shida unajaza tu card number basi simple, pili kwenye review watu wanapost hadi picture so unajua kifaa unacho agiza kutafananaje, tatu bidhaa unaweza kutrack kwenye mobile app pale pale nne buyers wako
fasta sana kujibu matatizo uliyonayo.
Sasa kwenye bidhaa yani nilivyo Agiza na kulipia shipping (ya juu ilikuwa 3$) vyote vimefika Dar tarehe 11 mwezi huu so vilichukua siku 12 na posta wakanitumia message nikachukue.
So kama kuna mtu alikuwa anaogopa ondoa shaka cha msingi soma review za seller, angalia rating na nunua bidhaa yenye buyers wengi kidogo.. Ndio hayo tu.
Wanayo depending na seller 45 days na 60 days. Ali pay haina tofauti na PayPal.Hawa wana hata buyers protection km paypal vile
Jamani samahani kwa usumbufu .nilikua nauliza jinsi ya kupata verification code kutoka paypal ambayo hutumwa benki mana nimejaribu kuchukua benki statment transaction ya paypal walio kata 1$ haijaonekana ila nilipo ingiza mastercard kwenye paypal nilipokea ujumbe kua pesa imekatwa .nimejaribu kuwauliza CRDB hawajaiona .natumai ombi langu litajibiwa
Naomba mtu anayejua portal ya BancABC ninayoweza kuingia na ku-access card yangu. Yaani kuangalia salio na kuona transaction nilizofanya kupitia card yangu. Kwa mfano ya UBA najua ni Login naomba kujua ya BancABCBANC ABCni 15000 na unakatwa kiasi unacholipia tu hakuna makato ya transaction wala nini,mfano,unanunua bidhaa yenye thamani ya Usd 120 utakatwa Usd 120 tu
w