Simu yangu ya htc ilipasuka kioo, nikatafuta weee, mwisho kuna mtu humu jukwaani akanitajia fundi yupo posta anaitwa sele. nikaenda kufika kaniambua kioo kipo ila bei laki, haipungui wala nini, nikaona pagumu.
Mwezi uliopita nikaamua nijaribu ebay nikakuta vioo kibao nikachagua model yangu, nikalipia kwa paypal, kama elfu 36 tu na free shipping.
Baada ya wiki 3 nimekipata kioo.
Kwa wale wanaohofia kuibiwa au kutapeliwa, mie nimepata bidhaa niliyonunua, nanyi msisite kununua.
JIBU:
UncleUber replied; mzigo wako utaupokelea posta au mahala popote ambapo utakuwa umeomba mzigo wako upelekwe; mfano unaweza(kama umelipia gharama za kuuleta kwa njia husika) kuja DHL au USPS n.k utaukuta kwenye ofisi husika, mara nyingi uwa wanakupigia simu kifurushi chako kikifika (hata posta wanapiga simu)