Jifunze Jinsi ya kufanya Manunuzi kwa Ebay mtandaoni

Jifunze Jinsi ya kufanya Manunuzi kwa Ebay mtandaoni

Mkuu nashukuru kwa maelezo uliyotoa kutokea mwanzo mpaka mwisho hapa ulipofikia. Ni kweli watu wanang'ang'ania CDRB lakini mimi nilienda ABC na kununua VISA kwa U$20 kama gharama ndiyo basi tena hadi itakoisha muda wake. Kwa maana hawana monthly charges wala fee charge kama ukinunua online. Ni wazuri kiukweli.

Kitu kilichonifanya mpaka nachangia ni kuwa niliagiza battery mbili toka China lakini jamaa akatuma mpaka tracking no lakini Singapore Post wakapoteza mzigo kwenye distpating process. Seller akatuma nyingine kwangu baada ya kumjulisha mbona sioni updates yoyote. Akanitumia tena kupitia China Post na tracking no nyingine na sasa naambiwa zimeshasafirishwa Bongo.

Sema nimeshituka sana baada ya kuambiwa uwizi ulipo Posta zetu. Na mimi nilikuwa nafanya kama jaribio ili niagize video camera kubwa ambayo nipo tayari kulipia kodi.

Ngoja nisubiri kamanitazipata week hii ili nije nitoe ushuhuda juu ya Posta za Tanzania.
mkuu huko ABC vertification code unaipataje ikiwa AC huna maana umenunua card tu.
Ebu nitoe tongotongo.
 
Ndiyo lakini kutoa ni kwa banki zote ambazo zina support Viza na Mastercard.

Kuweka ndiyo lazima uweke kwenye matawi yao tu.


Mkuu huko ABC vertification code unaipataje ikiwa AC huna maana umenunua card tu. Ebu nitoe tongotongo.
 
Mimi nimefungua account na nimepata card ya visa travel kwa $ 30 bancAbc. So minimum amount ni $30

mkuu huko ABC vertification code unaipataje ikiwa AC huna maana umenunua card tu.
Ebu nitoe tongotongo.
 
bank statement nitaipataje ikiwa sina ac yao maana nimenunua card tu.
Ebu funguka vyema mkuu.

We nenda wambie unataka bank statement Najua umenunua Card lkn haimanishi hauwezi kuweka/kutoa pesa wala haimaniishi hauwezi omba bank statement.

Card hiyo ina operate sawa na card nyingine tu zaidi tu kwenye kuweka pesa unatumia card number.
 
bank statement nitaipataje ikiwa sina ac yao maana nimenunua card tu.
Ebu funguka vyema mkuu.

Kama unaweza deposit pesa kwa kutumia card namba, mi nahisi hiyo ndo acc number yako. Nadhani hizo ni mbinu za kibiashara kuvutia wateja(kuwa wanakuuzia card tu),

huenda wanashughulikia wenyewe kukufungulia acc. Endapo unaweka pesa kwao ili ufanye manunuzi online, basi hata bank statement utaipata.

Ni mawazo tu, nawasilisha.
 
Kuhusu verification code, Hii inapatikana kwenye bank statement yako mara baada ya kununua kitu online. Haya ni maelezo niliyopewa benki ya ABC nlitaka kujua kuhusu verification code.

Jamaa pia alinionyesha hiyo verification code.

Thats is all
 
Siku hizi biashara zimerahisishwa sana na maendeleo ya mtandao wa intaneti unaowezesha watu kuuza na kununua vitu na huduma kupitia mtandao. Kwa sababu ya maendeleo haya, mara nyingi tunapokuwa tunatumia mtandao wa internet tunakutana na vitu mbali vizuri kama vile software, vitabu, nguo, saa, magari au hata kozi ya kusoma kwenye mtandano.

Mara nyingi vitu hivi huwa na bei nzuri sana ambayo huvutia kununua. Shida kubwa na yenye mantiki inayojitokeza ni usalama wa pesa zetu na akaunti zetu za benki tunapofanya manunuzi kwenye mtandao. Mimi binafsi ni mnunuaji wa kwenye mtandao hivyo nitakwenda kuelezea vitu vya muhimu vya kufanya kabla hujatoa namba ya kadi yako ya benki kwenye matandao.

1. Tafuta Debit card au Credit card

Debit card ni kadi inayokuwezesha kununua vitu kwenye mtandao kwa kutumia pesa iliyo kwenye akaunti yako ya benki. Na Credit card inakuwezesha kununua kwa kukopa kwenye benki unayotumia halafu wanakukata kidogokidgo kwenye mshahara wako au namna yoyote ambayo mtakubaliana na benki. Kadi hizi ni kama Tembo card visa na Tembo card master card za CRDB Bank;

benki zingine kama NBC, Stanbic Bank na BARCLAYS Bank pia zinatoa Kadi Za namna hiyo. Baada ya kupata kadi yako unatakiwa uende kwenye benki yako wakairuhusu kuweza kufanya manunuzi kwenye mtandao.

2. Jiunge na tovuti ya Paypal.

Paypal ni tovuti inayoongoza duniani kwa kusimia malipo ya kwenye mtandao. Kazi yake kubwa ni kutunza taarifa zako muhimu za benki ili wamachinga wa kwenye mtandao wasizizoee hovyo. Hivyo basi ukitumia paypal, unasajili na kuweka namba yako ya visa au master card.

Baada ya hapo unaweza kuweka pesa kwenye account ya paypal au ukaziacha kwenye akaunti yako ya benki. Unapofanya manunuzi Yule muuzaji anapewa pesa na Paypal sio wewe moja kwa moja ili kulinda taarifa zako za benki.

3. Nunua kwenye tovuti iliyo na mfumo wa kutuma taarifa zako kwa usalama.

Kwa ajili ya usalama kuna teknologia inaitwa SSL(Secure Socket Layer). SSL inafanya kazi ya kusafirisha taarifa zako katika hali ya mkanganyiko ili mtu yoyote mhalifu asiweze kuzielewa, zikifika zianaundwa tena ili muuzaji aweze kuzielewa.

Teknologia hii inatumika pia kutuma email, blackberry wakiwa ni vinara wa kutunia teknologia hii. Ili kujua kama tovuti inatumia hii teknologia utaona alama ya kufuli kwenye anuani ya tovuti husika ikishafunguka. Angalia kwenye sehemu ya kuandikia anuani, kushoto au kulia.

4. Tumia tovuti inayoaminika


Unaponunua kitu kwenye mtandao kwanza kabisa hakikisha hiyo tovuti inafahamika, kama haifahamiki hakikisha kuwa imethibishwa na na mashirika yakuhalalisha biashara za kwenye mtandao kama BBB (Better Business Bureau), utaona nembo ya haya mashirika chini kwenye tovuti ya muuzaji.

5. Nunua kwa muuzaji anayekubaliwa na weteja wengi.

Utajuaje kama muuzaji anakubalika sokoni na anauzoefu wa kuuza vitu kwenye mtandao? Rahisi! Kwa mfanounataka kununua saa Ebay au kitabu cha electrniki (PDF) kwenye Amazon, chini ya hiyo bidhaa iliyoichagua utaona maoni ya watu walionunua kabla yako.

Ni vizuri ukatumia muda wa kutosha kusoma maoni ya waru wengi kabla hujaendelea za zoezi la manunuzi. Njia nyingine ya kupata maoni ya watu ni kutumia tovuti kama Yelp, Google+, Yahoo directory au Yellow pages iwapo muuazaji atakuwa amejiunga nazo.

6. Chagua namna ya kutumiwa mzigo wako.

Unatakiwa kuchagua namna kutumiwa mzigo wako ambayo itakuwa rahisi kwako kuupata. Gharama za kutuma mzigo zitaoneshwa pale kwenye mtandao na muda wa kufika kwa kila gharama. Kwa Tanzania unaweza kutumia DHL, UPS au shirika lolote unaloliamini.

7. Hakikisha muuzaji anahudumia eneo ulilopo.

Baadi ya wauzaji huchagua nchi au miji wanayoweza kutuma mizigo na wengine huuza dunia nzima. Taarifa hizi huwekwa chini ya bidhaa unayotaka kununua , hii itakusaidia kuokoa muda kuondoa usumbufu usio wa lazima.
 
Nataka kununua ipad air. Nimemuuliza muuzaji njia gani atatumia akasema 'express international'. Ndo nini hiyo? DHL? Je, UPS mzigo nachukulia posta?
 
Ok wauzaji Wengi toka US hawana option ya kutuma huku Africa, cha kufanya ni kama una mtu kule iende kwake na mara nyingi within US inakuwa free shipping then huyo mtu wako afanye utaratibu wa kukutumia huku
 
wakuu ishu ya kuuza online na kupokea hela kwa sie wajasiriamali wa bongo bado haijawa active???????????
 
wakuu ishu ya kuuza online na kupokea hela kwa sie wajasiriamali wa bongo bado haijawa active???????????

unaweza kufanya hivyo. Kibisa! Na ni rahisi, naweza kukusaidia kuset up hivyo kitu. Muda si mrefu nitaandika makala ya jinsi ya kuuza vitu kwenye mtandao.
 
wakuu ishu ya kuuza online na kupokea hela kwa sie wajasiriamali wa bongo bado haijawa active???????????

Kupokea hela Tanzania lazima utumie US Mastercard Services ambazo ku sign up tu unapata 25$ lkn payout ni mpaka ifikie 100$
Na hela ya kutoa hela ATM za mastercard ni 1% ya hela unayo cashout.

Na kwa mwaka unalipa 25$ za service kutumia service yao ambayo iko fair iwapo hiyo acct itakua inakuingiza hela nyingi
Maelezo zaidi angali Chati niloweka chini.

Hiyo sio shida faida yao ni nn hawa jamaa?

1.Unafanya maombi ya BURE ya Master Card ambayo inakua ya US kupitia hapa US Mastercard Services

2.Maombi yanachukua mda kidogo lazima uwe mpole kabla hawajakukubalia

3.Wakiyakubali maombi yako utatumiwa Master card yako kupitia FEDEX/DHL

4.Hatua ya pili uta activate card kwenye website yao

5.Baada ya hapo fungua PayPal account kisha weka details za Master card uliyotumiwa

6.Kishautakua unalipwa na kupokea malipo bila shida yoyote

5.Lakini bei zao kutoa hela katika ATM yoyote e.g NBC,CRDB,BARCKLAYS,STANBIC e.t.c makato yao ni kama ifatavyo


[TABLE="class: fees-table"]
[TR]
[TH]Item[/TH]
[TH]Price (USD)[/TH]
[TH]Unit[/TH]
[TH]How Applied[/TH]
[/TR]
[TR]
[TD="class: title, colspan: 4"]Card Account[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: item"]Annual Account Maintenance[/TD]
[TD="class: price"]$29.95[/TD]
[TD="class: unit"]Per year[/TD]
[TD="class: how-applied"]From available balance - each year[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: seperator, colspan: 4"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: item"]Card Replacement[/TD]
[TD="class: price"]$12.95[/TD]
[TD="class: unit"]Per card[/TD]
[TD="class: how-applied"]One Time - when issuing a replacement card[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: seperator, colspan: 4"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: title, colspan: 4"]ATM/Cash Withdrawals or Transactions *[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: item"]ATM Withdrawal or POS/Bank Teller Cash Disbursement[/TD]
[TD="class: price"]$3.15[/TD]
[TD="class: unit"]Per Trx[/TD]
[TD="class: how-applied"]When withdrawal or disbursement is requested
(*surcharge may also be applied by your ATM/POS service provider)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: seperator, colspan: 4"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: item"]ATM Decline Fee
[/TD]
[TD="class: price"]$1.00[/TD]
[TD="class: unit"]Per Trx[/TD]
[TD="class: how-applied"]When withdrawal request is declined
(*surcharge may also be applied by your ATM service provider)[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: seperator, colspan: 4"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: item"]ATM Balance Inquiry Fee[/TD]
[TD="class: price"]$1.00[/TD]
[TD="class: unit"]Per Trx[/TD]
[TD="class: how-applied"]When ATM balance inquiry is made
(*surcharge may also be applied by your ATM service provider)[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Mkuu njuwa Wa mavoko saluti sana Ila Jana nimejusajuli ebay pamoja na huduma ya paypal ingawa bado haijawa activated Sasa kuna buyer nimemtumia meseji hajibu Sasa sina uhakika km kweli hajibu au kuna namna unafanya ili uweze kuona meseji zake.
 
mkuu njuwa Wa mavoko saluti sana Ila Jana nimejusajuli ebay pamoja na huduma ya paypal ingawa bado haijawa activated Sasa kuna buyer nimemtumia meseji hajibu Sasa sina uhakika km kweli hajibu au kuna namna unafanya ili uweze kuona meseji zake

Kuna differences za timezome wengine uchukua hata 72Hrs hawajajibu
 
Back
Top Bottom