Jifunze Jinsi ya kufanya Manunuzi kwa Ebay mtandaoni

Jifunze Jinsi ya kufanya Manunuzi kwa Ebay mtandaoni

Jaribu kuopitia hee thread vizuri majibu yote yapo humu mkuu ila kwa ufupi kidogo ni kwamba Hii inategemea na sites utakayotumia,cha msingi ogopa kufanya payment kwenye sites zisizo na mfumo ulio organized/centralized kwa ajili ya malipo yaani sites ambazo individual seller anaweza ku access credit card information zako kwahiyo kuna hatari badae akazitumia kwa manufaa yake.
Sites kama Amazon,Aliexpress,Alibaba na nyingine(ambazo bado sijazifahamu) wao wanamifumo yao ya secure payment amazon payments,Alipay,Escrow respectively.
Pia online merchants nyingi kama geekbuying,gearbest,pandawill,banggood nk ni salama kwenye credit card payments nilishawahi kudokoa vitu vya gharama ndogo among hizo sites na sijawah experience tatizo.
The most important thing ni kuangalia reviews kitoka kwa wanunuaji.All the best sorry kwa maelezo marefu
Thank u nmekuelewa sana....
 
Serikali mkurupuko haijawakurupua tu hawa posta waliolala usingizi wa pono ?
 
Naomba kuuliza wakuu, vp kuhusu swala la kodi limekaaje? nataka kununua simu, vp mzigo unapofika, haulipiwi kodi? Lets say nataka kuagiza simu ya $400.
Ukipitishia posta hamna kodi, ila DHL hawaaminiki unaweza lipa kodi au la.
 
Habari wadau.
Mimi nimeshafanya manunuzi kadhaa kupitia Aliexpress na ebay, ebay wanatumia paypal kama mfumo wao ambao certified kwa ajili ya malipo na Aliexpress wanatumia Alipay.
Katika manunuzi yote niliyowahi kufanya mara moja nililetewa kitu ambacho sicho nilichoagiza, cover ya simu ambayo nilinunua kama 1.2 us $ nikaona option ya kurudisha ni gharama kuliko niliyonunulia.
Recently niliagiza Nokia Lumia 1020 kwa AU$(Australian Dollar) 275 ilikuwa 24th may, kupokea nilitegemea iwe 14 June to 28 June.
Hadi Julai 30 nikawa sijapokea simu kwani walitumia Singapore Post kuruma mzigo wangu ambapo hawa jamaa wa Singapore post mizigo hupitia Kenya ndo huja Tanzania.
Nikawasiliana na Seller since mzigo umetumwa kwamba mbona unaenda Kenya akaniambia hiyo ni flight tu ila unakuja Tanzania, mzigo haukufika hadi tarehe tajwa hapo juu.
Nikafungua kesi katika resolution center ya Ebay (Paypal nao wanaresolution center yao kama eBay hawajakuridhisha na maamuzi yao ).
Katika hii kesi mimi nili demand nipate mzigo/nitumiwe tena mzigo, inavyoonekana mzigo ulipotelea Kenya au in between kwani hivi juzi seller ameamua kurudisha hela yote niliyonunulia simu hiyo Nokia lumia 1020 and the case is closed.
So ninachowashauri wenzangu ni kuwa kuibiwa utaibiwa kama hautatumia mfumo wa malipo ambao mtandao husika unakuelekeza kuwa ndio safe na kufanya ufuatiliaji kama vitu vyako haujapokea kwa wakati husika.
Asanteni.
 
Kwa wale mnaonunua vitu amazon nilikua naomba msaada kidogo coz nilitaka kununua kitu flan amazo ila wakaniambia hawafanyi shipping Tz so nkafungua account Comgateway ili nipate US address etc......Sasa nilivyosign up na hawa jamaa kwenye sehemu ya kuandika shipping address najaza vizur form yao lakini iliclick add nothing happens msaada please
 
Sasa nilivyosign up na hawa jamaa kwenye sehemu ya kuandika shipping address najaza vizur form yao lakini iliclick add nothing happens msaada please
Tumia browser nyingine tofauti na unayotumia. Kisha rudia kujaza hizo taarifa zako.
 
nilikua naomba kujuzwa je Kuagiza bidhaa kutoka ebay na muuzaji kunitumia ni salama?
njia ya malipo ya paypal nayo salama?
je wakifanya shipping kutoka china hadi tz nkienda kuchukua kamzigo kangu pale bandarini kurasini kuna gharama ntatozwa hadi ntoke na mzigo?
msaada wenye uzoefu.
 
Jamani nashukuru sana kwa waliotoa maelekezo,nilipata challenge kubwa sana tangu last year kuwezesha DEBIT CARD yangu iweze kufanya online payment,nilianza na NBC nikajaza form wakaniambia tayari lakin kadi yangu ilizidi kuwa declined kila nilipojaribu nikaenda NMB nao wakaleta mbwembwe mara lazma niwe na akaunti ya biashara hatimaye nikafungua acc CRDB jumanne nikaernda kujaza form ya maombi jana nikatumiwa sms kuwa kadi yangu imewezeshwa natakiwa niende kwenye website yao ili nijiunge na huduma ya verified by visa nikakamilisha.Leo asubuhi nimethubutu kuingia aliexpress nikaanza kujaribu USB OTG cable kwa 1.5USD na USB cable nyingine kwa 0.9USD zote zina free shipping nikazilipia badae order zikawa zimeandikwa payment succesful nisubiri 24 hrs for verification,nmimeingia jion hii nikaona payment verified na order imeandikwa awaiting shipment wacha nione kwanza itakavokuwa.Shukrani kwa wote waliotoa michango chanya na kututia moyo amateurs.najaribu ku attach screenshot napata error nikiweza nitaiweka
Vp mzigo ushaupata
Mkuu asante sana kwa feedback.
Nimeona umenunua case ya LG Nexus 5x, vipi simu ulinunulia hapa bongo ama uliagiza online?
Mi niko kwenye harakat za kuiagiza kutoka ebay
 
Nice thread. Asante sana.

Inabidi na Serikali ya Tanzania hasa Posta iwe bora kuruhusu shipping na posting kuwa rahisi. Posta wana tabia ya kuchukua vitu vya watu hasa vidogo vidogo. Ni aibu na wananchi tunaomba mfumo wa posta uwe bora.
 
Nice thread. Asante sana.

Inabidi na Serikali ya Tanzania hasa Posta iwe bora kuruhusu shipping na posting kuwa rahisi. Posta wana tabia ya kuchukua vitu vya watu hasa vidogo vidogo. Ni aibu na wananchi tunaomba mfumo wa posta uwe bora.
Posta wanaweza kukomesha udokozi wa vitu vidogo vidogo na hata vikubwa kwa kuweka mfumo wa uthibiti kama wa DHL na Courier, wao wanarekodi ktk mfumo wa electronic na hivyo kujua mzigo uko wapi na saa ngapi na hali gani.
 
Posta wanaweza kukomesha udokozi wa vitu vidogo vidogo na hata vikubwa kwa kuweka mfumo wa uthibiti kama wa DHL na Courier, wao wanarekodi ktk mfumo wa electronic na hivyo kujua mzigo uko wapi na saa ngapi na hali gani.

Basi ni jambo la hekima wakianza. Posta sioni kama inafanya jitihada. Bora DHL wanajitahidi.
 
Back
Top Bottom