Jifunze kilimo cha nyanya

Mkuu hivi nikilima kipindi gani nitavuna kipindi nyanya sio nyingi sokoni, na nikitumia drip irigation kulima enea la bustani la nyumbani la mita 30 kwa 30,itanigharimu shilingi ngapi kuweka mfumo wa umwagiliaji wa drip.
Si zaid ya laki 5
 


TUNASHUKURU SANA KWA ELIMU KUBWA, NAOMBA KUFANHAMU KAMA UNATUMIA PIA SAMADI KATIKA KUPANDA HIYO MICHE YA NYANYA.
 


TUKISHUSHA HESABU MAMBO YATAKUWA HIVI
20 10,000 200,000
60 10,000 600,000
120 10,000 1,200,000
180 10,000 1,800,000
240 10,000 2,400,000
180 10,000 1,800,000
120 10,000 1,200,000
60 10,000 600,000
20 10,000 200,000

10,000,000 hii ni jumla ya mauzo ya michumo yote

lakini kazi hii inatakiwa kujitoa sana, mda wa kutosha, pesa na weledi.
 
TUNASHUKURU SANA KWA ELIMU KUBWA, NAOMBA KUFANHAMU KAMA UNATUMIA PIA SAMADI KATIKA KUPANDA HIYO MICHE YA NYANYA.
Mbolea ni lazima, kuna mbolea za chini za kupandia na kukuzia ukishapanda miche shambani
Pia kuna mbolea za juu tunaita booster
 
Hayo ni makadirio, itategemea ubora wa shamba,huduma na mbegu utakayotumia kupata hizo boksi

Pia itategemea na bei ya boksi kuna kipindi inazidi hiyo 10,000 na kuna kipindi inashuka hadi 7000
 
Habari wanajamvi, nimelima nyanya msimu huu na nimepanda mbegu inaitwa Mwanga, naomba kujuzwa ubora wake kwa anaye ifahamu.
 
Shamba bora la nyanya linatakiwa liweje mkuu? Au pale unaposema ubora itategemea na shamba langu unakuwa na maana gani?
Ubora wa shamba ni udongo, kila zao na udongo wake kuna udongo mzuri wa nyanya. Ukiwa na shamba lenye udongo mzuri kinachofata umelilimaje? Yani ulisafishe vzr alafu ulime kwa trekta baada ya hapo upige shimo vzr

Kwakifupi huo ndio ubora wa shamba.
 
Ubora wa shamba ni udongo, kila zao na udongo wake kuna udongo mzuri wa nyanya
Ukiwa na shamba lenye udongo mzuri kinachofata umelilimaje? Yani ulisafishe vzr alafu ulime kwa trekta baada ya hapo upige shimo vzr

Kwakifupi huo ndio ubora wa shamba

Shukrani kwa Jibu zuri, na pia usinichoke kwa kuwa nina lengo la kujua na kufanikiwa zaidi katika kilimo cha nyanya, Hapo kwenye udongo ni udongo gani ndio unafaa zaidi kwa kilimo cha nyanya?
 
Shukrani kwa Jibu zuri, na pia usinichoke kwa kuwa nina lengo la kujua na kufanikiwa zaidi katika kilimo cha nyanya, Hapo kwenye udongo ni udongo gani ndio unafaa zaidi kwa kilimo cha nyanya?

Kwa kiswahili tuna kichanga,mfinyanzi na tifutifu ambapo ni sawa na kusema sand,clay and silt kwa lugha ya kigeni sasa kuna udongo unaitwa loamy soil huo ndio unafaa zaidi kwa kilimo lakini sasa kiswahili chake sikifahamu vyema ila kwa ufupi unakua na mchanganyiko mchanga, tifutifu na mfinyanzi haujapishana sana na udongo wa msituni ukinyesha maji yanakaa ila si kama mfinyanzi na hayapotei kama kichanga kilivyo, kwa kua unasifa ya mfinyanzi basi pia unauwezo wa kuzuia madini mengi hivyo unakua na madini pia na hata ukiweka mbolea unaona kweli imefanya kazi,pia sio mgumu umejiachia kama tifutifu ila haupotezwi kwa upepo.

Pendelea sana kumwaga samadi shambani kwako na hata mazao ukivuna yalimie humo huko na trekta inafaida sana ya kutunza ardhi yako na kuiboresha kua loamy soil.
 
Shukrani kwa Jibu zuri, na pia usinichoke kwa kuwa nina lengo la kujua na kufanikiwa zaidi katika kilimo cha nyanya, Hapo kwenye udongo ni udongo gani ndio unafaa zaidi kwa kilimo cha nyanya?
Nyanya inafanya vzr kulimwa kwenye udongo wa mfinyanzi na tifutifu, nyanya haifanyi vzr kwenye udongo wenye kichanga

Na ikiwa shamba lako lina kichanga basi unatakiwa upige shimo lefu kwenda chini hadi uupate udongo mweusi

Madhara ya kulima nyanya kwenye kichanga nyanya hazizai sn na zinawahi kuisha yani unaweza kuchuma mara tatu ukakuta nyanya zimeisha shambani
 

Aisee Shukrani saana kwa maelezo mazuri, sasa hapo kifuatacho ni utekelezaji tuu.
 

Shukrani mkuu kwa maelezo yaliyonyooka japo jina lako ni Yumbayumba. Ngoja nikusanye nguvu ili nami nianze kulima hiyo nyanya inayoitwa Asila, kwa sasa wacha kwanza nikomae na hizi mbegu za kawaida maana hii Asila itanitoa Damu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…