Jifunze kilimo cha nyanya

Naomba namba kiongozi
 
Niliona kwamba nyanya unaweza vuna katika stage tatu zikishakomaa na zinabadilika rangi kwa mtiririko huu Green, Pink na Red kutokana na mwonekano huo sasa unavuna. Je, mkuu kuna wanaovuna zikiwa bado hazijapata wekundu?

Nyanya ni kweli zikikomaa zina hizo stage 3 ulizozitaja.
  • Green ni nyanya mbichi hazifai kuchumwa
  • Pink sisi tunaita mapera hizi pia uwa hatuchumi labda bei iwe kubwa sn siku hiyo ndio utachuma hadi mapera
  • Red ndio nyanya zinazotakiwa kuchumwa
Swala la kusema eti tuchume mapema sababu zinaenda mbali hiyo haituhusu, atajua mwenyewe mnunuzi, huwa tunauza nyanya shambani na tunachuma red tu, atajua mwenyewe anapeleka wapi.

Kuna madhara makubwa ukichuma hadi mapema

Kwanza ujue nyanya zinaongezeka kila mchumo sasa ukichuma hadi mapera inamaana unapunguza mavuno ya mchumo ujao na unapunguza michumo pia.

Kwa kifupi utakuwa unamfurahisha mfanyabiashara huku unajimaliza wewe mwenyewe.
 
Morogoro wilaya gani mkuu? Je, ni kilimo cha mvua au umwagiliaji? Msimu ni lini?
Tuna misimu miwili, wa kwanza huu wa masika tunalima mwezi wa tatu

Wa pili ni wa kumwagilia huu unaanza mwezi wa sita
 
Kunashamba nimepata hapa morogoro karibu na mto ngerengere
 
Kunashamba nimepata hapa morogoro karibu na mto ngerengere

Heka wanauza 350,000/=
Naombeni ushauri nichukue?
Wanasema mto huwa unakauka kipimdi flan hivyo wana tengeneza malambo hapo kwenye mto wanaanza kulimia maji ya nkuwa kwenye mchanga chini
 
Heka wanauza 350,000/=
Naombeni ushauri nichukue?
Wanasema mto huwa unakauka kipimdi flan hivyo wana tengeneza malambo hapo kwenye mto wanaanza kulimia maji ya nkuwa kwenye mchanga chini
Udongo wake upoje? Kuna vitu vya kuzingatia wakati wa kununua shamba usiangalie maji na bei tu
 
Udongo wake ni kichanga na mfinyanzi katikati ya izo dongo mbili. Huyo mtu analimaga hoho na nyanya na ngogwe
 
Udongo wake ni kichanga na mfinyanzi katikati ya izo dongo mbili. Huyo mtu analimaga hoho na nyanya na ngogwe
Mm sijaliona shamba siwezi kukushauri ununue au usinunue ila uwa tunakodi kwanza ukiridhika nalo ndio unanunua

Tafuta mtu muaminifu anayelijua shamba vzr ndio atakushauri
 
Mm sijaliona shamba siwezi kukushauri ununue au usinunue ila uwa tunakodi kwanza ukiridhika nalo ndio unanunua

Tafuta mtu muaminifu anayelijua shamba vzr ndio atakushauri
Shughuli ipo kwenye kukodi alafu uweke hela zako hapo kwenye kungoa visiki, kusafisha shamba. Alafu unaacha baadaye unasepa kwingine.. Sema lakini kuna kijana mmoja hapo pembeni kuaza nyanya heka mbili kapiga 24million . Na aridhi ina rutuba kwa kuwa ilikuwa pori muda mrefu.. Jamaa anakwambia wala hakuweka mbolea zaidi ya dawa kadhaa tu za kuzuia wadudu..
 
Kuna kuna limwa mahindi zaidi ila wachache walio na maeneo pepmbezon mwa mto ndio wanalima mbogo mboga
Kama wanalima zaidi mahindi basi hilo shamba lina kichanga kingi halifai kwa kilimo cha nyanya ndomana wanalima mbogamboga

Hata na ww ukinunua itabidi ulime mazao hayohayo wanayolima wao
 
Kama wanalima zaidi mahindi basi hilo shamba lina kichanga kingi halifai kwa kilimo cha nyanya ndomana wanalima mbogamboga

Hata na ww ukinunua itabidi ulime mazao hayohayo wanayolima wao
Hivi shamba linalo faa kwa nyanya linatakiwa kuwa na udongo gani??
 
Hivi shamba linalo faa kwa nyanya linatakiwa kuwa na udongo gani??
Nyanya inahitaji udongo wa mfinyanzi, kwanza unatunza maji pia una rutuba

Kama shamba lina kichanga utafosi kulima nyanya ila huwezi kupata matokeo mazuri
 
Kwanza ungetakiwa ujue unataka kulima nini ndio ujue shamba gani ununue, shamba la nyanya na la mahindi tofauti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…