Jifunze kilimo cha nyanya

Jifunze kilimo cha nyanya

Ndio ni kweli mm nasimamia upande wa mkulima tu simuangalii mfanyabiashara, ndomana tunauzia shamba kila mtu anakufa na chake

Nikimuuzia mfanyabiashara nyanya pink nampa faida sn alafu mm inanikata
Kuhusu nyanya kuharibika hiyo sio hoja, ndomana tunanunua mbegu za gharama sn sababu zinakaa muda mrefu bila kuharibika, pia kuna dawa za kukomaza matunda uwa tunapiga yani tunda linakomaa haliharibiki

Mfano nyanya ikiwa box 10,000/= mnunuzi akitaka pink lazima aongeze hela ndio nimchumie tofauti na hapo aende zake, wanunuzi wapo wengi

Mm nikipambana nyanya ikifika wakati wa kuvuna sichek na mtu sababu mm ndio nimeumia shamba, sipangiwi nyanya zipi nichume zipi niache

Okay sawa sawa but naamini kuna mwaka utafika utafanya yote yaani utakua unalima na kuuza mwenyewe ili upate faida yote wewe sababu mkulima pia anaweza kua mfanyabiashara sababu hata hao wanaonunua kwenu na kwenda kuuza ni watu kama sisi wakulima wakawaida ndugu yangu why miaka nenda rudi tuwanufaishe wao [emoji1433][emoji1433][emoji1433]
 
Nikiotesha mwezi huu inamana zitaanza kuchumwa mwezi wa 5 , je soko linakuwaje hapo nahis kama vile mavuno mengi yanakuwa sokoni banda ya masika.. Au unasemaje brother??

Kuanzia mwezi wa sita soko linachaguka labda litokee janga kama mvua kuzidi au mvua isiponyesha
 
Kuna kitu nataka kujua kuhusu huyu mdudu kantangaze.. Je nikiwa niko katikati ya msitu sijazungukwa na mkulima mwingine yeyote yaan ful pori alafu hapo katikati ya pori ndio mm nalima heka zangu za nyanya je huyu mdudu anaweza nipata?

Yes huyu mdudu anaweza kukupata pia labda iwe hayuko mazingira hayo but guarantee hakuna na pia with time atakuja sababu wanafahamu chakula kiko wapi
 
Mkuu horticulturalist, hivi recommended spacing ya hizi semi determinate mfano assila, eden, jarrah rz, open field..!ni IPI nzuri Ikiwa 1.utalima bila Matuta, 2.utatumia mifereji, 3.utatumia matuta
 
Okay sawa sawa but naamini kuna mwaka utafika utafanya yote yaani utakua unalima na kuuza mwenyewe ili upate faida yote wewe sababu mkulima pia anaweza kua mfanyabiashara sababu hata hao wanaonunua kwenu na kwenda kuuza ni watu kama sisi wakulima wakawaida ndugu yangu why miaka nenda rudi tuwanufaishe wao [emoji1433][emoji1433][emoji1433]
Tena nikwambie ukiona mfanyabiashara anataka nyanya pink ujue ni galagaja, ana tamaa na anakuona mjinga au hana soko la uhakika anataka kuzurura nazo akitafuta soko kama ana soko la uhakika mwenyewe hazitaki pink
Mfano boss wetu sisi anaitwa dani hataki pink ananunua nyanya tunamaliza kuchuma jioni gari linaondoka muda huohuo linaingia dar usiku ikifika asubuhi nyanya inauzwa sokoni

Pili lazima ujue bei ya nyanya inabadilika kila siku, mfano jumamosi 10 jumapili inaweza kuwa 12 j3 ikawa 15
Sasa ukimuuzia mfanyabiashara nyanya za pink jumamosi kwa 10 yeye anaweza kukaa nazo hadi j3 akauza kwa 15 bei ya shamba hapo hujui sokoni kauza sh ngap
Ndomana nakwambia bora nyanya pink zibaki shamba usikilizie bei
 
Mkuu horticulturalist, hivi recommended spacing ya hizi semi determinate mfano assila, eden, jarrah rz, open field..!ni IPI nzuri Ikiwa 1.utalima bila Matuta, 2. Utatumia mifereji, 3. Utatumia matuta

Njia za kulima ni sababu ya unyeshaji sasa bila mfereji au matuta utatumia njia gani ya unyeshaji?

Mfereji pima mfeje hadi mfereji cm 140 mpaka 150 upandaji nyanya hadi nyanya cm 50 na mstari hadi mstari ni cm 150 (ikiwa umepanda mistari miwili kwenye mfereji au mmoja yote inahesabika kama mstari mmoja)

Matuta upana wa tuta ni mita moja na mfereji kati ya tuta moja mpaka lingine ni sm 50.

Juu ya tuta nyanya unaweka sm 50 mche hadi mche na kwenye tuta ukiweka mistari miwili weka sm 75 kati yake au sm 50 ukipanda zigzag juu ya tuta.
 
kuna sehemu nimepita jamaa analima nyanya aina ya assila kilimo cha mvua kawaida bila Matuta(single row). katika spacing zifuatazo..!1.30*60, 2.60*75, 3.60*90,..!Naomba kujua mahusiano ya hizo spacing na mavuno..!
 
kuna sehemu nimepita jamaa analima nyanya aina ya assila kilimo cha mvua kawaida bila Matuta(single row). katika spacing zifuatazo..!1.30*60, 2.60*75, 3.60*90,..!Naomba kujua mahusiano ya hizo spacing na mavuno..!

Ukiongeza spacing mimea inakua michache means mavuno yanapungua ingawa in other side utakua na healthy crop but hata ufanyaje mmea unakikomo cha uzaaji kulingana na aina kama unatoa matunda mia hata uweke umbali wa mita tano itatoa tu hayo hayo mia.
Pia kilimo cha mvua ni cha zamani sana now kua na uhakika wa maji kabla ya kufanya kilimo
 
IMG_2508.jpg
34ed90e2ab7cbb0b82068eccc3a4a664.jpg


Hakika kama unaitaka mali utaipata shambani,hii ndio gamhar rz
 
Wadau kuna mtu ashawahi kufanya tomato cloning? yaan unakata suckers au vikonyo unaviotesha the unakua mche wa nyanya? Na je production yake ni kama ya parent plant?
 
Wadau kuna mtu ashawahi kufanya tomato cloning? yaan unakata suckers au vikonyo unaviotesha the unakua mche wa nyanya? Na je production yake ni kama ya parent plant?

Yes nimewahi,chache kwanza zinashika and uzao sio mzuri sana bora kama unalima kwenye green house badi ile nyanya ndefu shina unalifukia baada ya hatua kadhaa linatoa mizizi upya inakaa hata two years
 
Mvua inaponyesha tu ni dawa gani inatumika kuzuia ukungu kwenye nyanya?

Kama ulishapiga dawa ya ukungu basi haina tatizo itakinga ukungu ila kama hukua umepiga ndani ya siku tano kabla ya mvua kunyesha basi inakulazimu upige daw yenye kiuatilifu cha kukinga na kutibu mfano:

1. Ivory 72, ebony 72, ridomil gold
2. Ortiva, othelo
3. Linkmil
4. Othelo top
5. Milraz
6. Infinito etc
 
Ugonjwa huu hapo juu unamaliza nyanya zangu. Dawa gani nitumie jamani? Nyanya zinaoza chini na kuanza kuiva.
 
Back
Top Bottom