Braza huu ugonjwa unaitwa STEM ROT (usifananishe na ROOT ROT)
Hutokea mazao yoteee.
Kwenye mahindi huitwa STALK ROT.
Hata Mimi kwenye shamba la parachichi uliingia (kwenye miche niliyopanda mwaka huu).
Ugonjwa huu ni wa fungus Jamii (Genus) ya Phytophthora.
Phytophthora ni fungus wa ajabu sana.
Mpaka sasa hivi wanasayansi washagundua species 150 na wanaamini kuna species 200 - 500 bado hazijagundulika.
Na mmoja wa species ya huyu fungus ni yule anaeleta early na late bright.
Sasa changamoto ni kwamba kwa huu ugonjwa wa stem rot ni SOIL BORNE DISEASE.
Kuna njia nyingi ya kuuzuia japo HAKUNA DAWA ZAIDI YA KUMFANYA TU ASIENDELEE KUZALIANA (Kutoa spore).
Kuna njia nyingi za Mechanical... Biological na Chemical.
Mi nilitumia zote na nilivyopanda miche mipya niliona MICHE MIPYA HAIHATHIRIKI TENA..!!!
Nakushauri tumia google kusoma STEM ROT.
Mi nilitumia google nikakuta research nyingi zilinisaidia kuutibu.
Nakukumbusha ni SOIL BORNE DISEASE.
Na huweza kuletwa shambani (kusambazwa) shamba kwenda shamba kwa njia nyingi kama palizi kipindi magugu ni mabichi, upepo kusafirisha mbegu zake (spores)...Maji kusafiri shamba moja hadi jengine... Na nyengine kibao.
Wapo wanaosema hauna dawa kwasababu, ni kama ROOT ROT; Hakuna mkulima aliyefanikiwa kuuondoa shambani ukatoka completely.
Mi nilitumia Copper.. Sulphur na Phosphorus NAAMINI wamesepa...!!!!
#YNWA
View attachment 1446394
Wrote from Anfield..!!!