Jifunze kuendesha (ku-control) nafsi ili kujikomboa katika vifungo na kuwa msaada kwa wengine

Mkuu,

Kwa vile sayansi haina majibu ya kila kitu, nikikwambia mimi ndiye Mungu muumba wa kila kitu, ndiye niliyeumba ulimwengu, na kila kitu kilichomo ndani ya ulimwengu, ila jambo hilo huwezi kulijua tu, kwa sababu lipo nje ya sayansi, utakubali? Utakubali maneno yangu kama yanaelezea jambo la ukweli mimi ndiye Mungu muumba vyote?
Sayansi hii tuliyonayo duniani ni tone tu la elimu katika bahari ya elimu aliyonayo MUNGU. Kuna mambo mengi anaweza kuyafanya kinyume na hii elimu ndogo aliyotupatia wanaadamu.
 
Mbona hujanijibu swali langu sasa?

Nakwambia mimi ndiye Mungu niliyeumba ulimwengu na vyote vilivyomo.

Unakubali?
 
Mkuu,

Kwa vile sayansi haina majibu ya kila kitu, nikikwambia mimi ndiye Mungu muumba wa kila kitu, ndiye niliyeumba ulimwengu, na kila kitu kilichomo ndani ya ulimwengu, ila jambo hilo huwezi kulijua tu, kwa sababu lipo nje ya sayansi, utakubali? Utakubali maneno yangu kama yanaelezea jambo la ukweli mimi ndiye Mungu muumba vyote?
Sita kubali mpaka unithibitishie katika namna ambayo itazidi upeo wa kibinadamu.

Mkuu Kiranga kujua maandiko na taratibu nyingine mbalimbali za kidini hiyo ni hatua moja kumjua MUNGU ni hatua nyingine.

Sasa hawa unaowaona wanahubili, unakuta msomi mzima proffessor anaudhulia ibada sio kwamba aliamua tu kuamini kichwa kichwa hapana wengi wao waliona ishara, na wengine hari waliyonayo kiuchumi kiafya ilifanikiswa na MUNGU.
 
Unaelewa kwamba ukishataka uthibitisho umeingia kwenye sayansi tayari?

Na unaelewa kwamba uthibitisho kama Mungu yupo ndio kitu ninachong'ng'ania hapa?

Na unaelewa kuwa ukishakubali kwamba "kuna mambo yamepita sayansi, hayawezi kuthibitishwa na sayansi" ushanipa nafasi mimi kusema mimi ndiye Mungu, na uthibitisho wa hilo umepita uwezo wako wa kufikiri, hivyo mimi ni Mungu, ila wewe huwezi kuelewa tu?

Yani hiyo hiyo principle yako ya kwamba kuna mambo yako nje ya sayansi, na hayana uthibitisho, na mimi naweza kuitumia kuhalalisha ujinga wowote.

Naweza kukuambia kuwa mimi ni Mungu, hilo lipo nje ya sayansi, na wewe huwezi kuelewa hilo.

Ukipinga nakwambia unaona, nikisema huwezi kuelewa, na kweli, hujaelewa.

Hapo vipi?
 
Nimekulewa vizuri mkuu... Sasa mimi kama mimi siwasemei wengine, nimetambua/nimegundua kua Mungu Ana deal na mtu mmoja mmoja, atajidhihirisha kwako ukiwa wewe pekeako, Sasa kwa hari kama hiyo nafsi yako inagundua na itakiri kua hapa sijafanyiwa utapeli wala janjajanja za kibinadamu(tricks) utahisi kabisa kua hapa nipo live.

Nadhani hii ndio sababu ya Mungu kuongea na Mtu husika kuliko kundi la watu, Alijua kunawapotoshaji wazee wa propaganda na fitina watawatoa watu mchezoni,

_20240314_232201.JPG

Unaelewa kwamba ukishataka uthibitisho umeingia kwenye sayansi tayari?
Sayansi haijazidi upeo wa kibinadamu mimi nimesema uthibitisho utakaozidi upeo wa kibinadamu.
Naweza kukuambia kuwa mimi ni Mungu, hilo lipo nje ya sayansi, na wewe huwezi kuelewa hilo.
Nitakuomba unipe ishara itakayo ashiria kua kweli hiyo ipo nje ya uwezo wa kisayansi.
 
Nimekulewa vizuri mkuu... Sasa mimi kama mimi siwasemei wengine, nimetambua/nimegundua kua Mungu Ana deal na mtu mmoja mmoja, atajidhihirisha kwako ukiwa wewe pekeako, Sasa kwa hari kama hiyo nafsi yako inagundua na itakiri kua hapa sijafanyiwa utapeli wala janjajanja za kibinadamu(tricks) utahisi kabisa kua hapa nipo live.

Nadhani hii ndio sababu ya Mungu kuongea na Mtu husika kuliko kundi la watu, Alijua kunawapotoshaji wazee wa propaganda na fitina watawatoa watu mchezoni,

View attachment 2934666

Sayansi haijazidi upeo wa kibinadamu mimi nimesema uthibitisho utakaozidi upeo wa kibinadamu.

Nitakuomba unipe ishara itakayo ashiria kua kweli hiyo ipo nje ya uwezo wa kisayansi.
Mkuu,

Unataka kusema Mungu ni mbaguzi, ana choyo cha kujithibitisha, anatubania, anachagua watu fulani anajithibitisha kwao wamjue bila shaka, wengine anawapotezea?

Huyo ndiye Mungu mnayesema ana upendo wote? Unajua hiyo dhana inam contradict Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote?

Unataka nikupe ishara itakayothibitisha kweli hiyo ipo nje ya uwezo wa kisayansi.

Wewe unaweza kuthibitisha kuna Mungu yupo nje ya uwezo wa kisayansi? Unaweza kutoa ishara ya kuthibitisha hilo?

Mbona naona kama unanipa mtihani ambao wewe mwenyewe hujaupita?
 
angetoa tumbo ili tumuabudu vizur, njaa zinatufanya tusione uwepo wake unatuleta dunian tukuabudu mbinguni malaika hawamtoshi kwa nn tumuabudu kwenye shida maelezo yasiwe mengi kiufup mungu wa kwenye vitabu hayupo
Mkuu,

Mungu huyo mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Huyo Mungu, kidhahania, ni Mungu mwenye tabia poa sana huyo Mungu ni wa peace and love, hana tatizo na kiumbe chochote huyo, yani fikiria wema wowote unaoweza kufanyika, wema wake ni mara infinity ya huo, angekuwa kweli yupo, asingeumba ulimwengu unaoruhusu njaa iwepo.

Huyo Mungu angekuwa yupo na kaumba ulimwengu, mabaya yote yasingewezekana kufanyika, kila kiumbe kingemjua Mungu bila utata. Ulimwengu usingeweza kuwa na tatizo lolote.

Hivyo, kuwepo kwa njaa ni uthibitisho huyo Mungu hayupo.
 
Kwaio nani aliumba ulimwengu ! Na vilivyomo
 
Kwa nini swali linakuwa "nani"? Huoni kuwa swali lenyewe kwanza limekuja na kasumba ya kujiegemeza kuwa ulimwengu uliumbwa na fulani, tumtafute tu tumjue huyo fulani ni nani?

Kama jibu liko upande tofauti kabisa, na ulimwengu haujaumbwa na fulani yeyote je?
 
Na Mimi naendelea kukuuliza, Wewe unasema hakuna Mungu. Na Mimi nakuuliza ulimwengu huu tuliopo nani aliuumba au ulitokeaje( Kama neno "nani" unaona linakukera),, vilivyomo ikiwemo na baba wa babu yako, babu yako mzaa baba yako, baba yako Hadi wewe mmetokeaje au mmetokea wapi
 
Mkuu,

Mungu huyo mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Huyo Mungu, kidhahania, ni Mungu mwenye tabia poa sana huyo Mungu ni wa peace and love, hana tatizo na kiumbe chochote huyo, yani fikiria wema wowote unaoweza kufanyika, wema wake ni mara infinity ya huo, angekuwa kweli yupo, asingeumba ulimwengu unaoruhusu njaa iwepo.

Huyo Mungu angekuwa yupo na kaumba ulimwengu, mabaya yote yasingewezekana kufanyika, kila kiumbe kingemjua Mungu bila utata. Ulimwengu usingeweza kuwa na tatizo lolote.

Hivyo, kuwepo kwa njaa ni uthibitisho huyo Mungu hayupo.
Tatizo lako Kiranga ni moja tu! Unaunda taswira ya Mungu kwa jinsi unavyomtaka wewe awe!! Yaani unampangia Mungu awe vile unavyotaka wewe. Jambo hilo haliwezekani kamwe!

Mungu ni mtawala,mfalme,tajiri na si muhitaji wa chochote kutoka kwa viumbe.Uwepo wake yeye haukutegemei wewe bali uwepo wako wewe ndio unamtegemea maamuzi yake YEYE.

Ukishalijua hili ndio utaelewa sifa zake Mungu.

Mungu ni mwenye huruma na hakuna mwenye huruma zaidi yake YEYE na vilevile ni mkali wa kuadhibu kwa maana ya hakuna mwenye adhabu kali zaidi yake YEYE.

Mungu ndiye anayegawa Riziki kwa viumbe wake kwa maana hakuna mtoa riziki zaidi yake yeye na huigawa riziki kwa amtakae na kwa kipimo anachokitaka YEYE kutakana na elimu na hekima yake YEYE. Vilevile ameipanga riziki kwa madaraja...kuna ambao amewapa daraja la juu hapa ulimwenguni kwa maana ya utajiri, na kuna ambao amewapa madaraja ya kati na vilevile wapo aliowapa madaraja ya chini. Ameweka mfumo huu kwa elimu na ujuzi wake ili maisha yetu yapate kusonga kwa kutegemea na kutumikiana sisi kwa sisi..kwa maana maskini atamtumikia tajiri ili apate ujira wake ambayo ndio hiyo RIZIKI na vilevile maskini atamuingizia faida tajiri wake ambayo pia ndio RIZIKI.

Huu ni mfumo wa maisha aliouweka Mungu hapa duniani ukiwa kama ni mtihani kwa kila kiumbe ili aone ni nani atakaemuamini na kutenda mema ili mwisho wa siku aje kumlipa malipo MAKUBWA zaidi ambayo ni maisha ya raha za milele ndani ya Pepo. Na yule atakaefeli mtihani eake hapa duniani kwa maana hakuamini na hakutenda mema basi atakumbana na adhabu kali ya moto wa Jahannam.
 
Hakuna kiumbe kisichomjua MUNGU hapa duniani isipokuwa ni ukaidi tu wa nafsi ila ndani kabisa unajua kuwa hivi vitu havikutokea tu duniani kwa bahati mbaya, yupo aliyeviunda mpaka vikawa.

Jeuri ya afya,Shibe na pumzi uliyopewa bure na Mungu ndiyo inayokuzuzua mpaka unamkana.

Jambo la ajabu sana unasema Mungu mwenye huruma sana hayupo ili hali ushahidi halisi upo ndani ya nafsi yako ....yaani licha ya MUNGU kukuatia pumzi bure,afya bure,ugali wako wa kila siku bure, mke bure, watoto bure,mali bure n.k bila ya kutoa senti tano yako bado unamkana waziwazi kuwa hayupo na wala hajakupatia hizi neema zinazokutia Kiburi , cha ajabu zaidi huruma yake Mungu ni kwamba bado anaendelea kukupatia hizi neema licha ya kuwa unamkana.

JE HAUTAFAKARI ? Kiranga

Je wewe una huruma ya kumhudumia mtoto wako mwenyewe uliyemzaa, yaani unampatia mahitaji yake yote ila mwisho wa siku anakukana mbele ya kadamnasi kuwa wewe sio BABA yake na wala hujamsaidia chochote. Kisha siku ya pili unaamka na unaendelea kumpatia mahitaji wake ya kila siku ila inapofika jioni tena anakukana?

Unayo hii huruma? Jibu ni hapana ,huna!

Ila MUNGU anayo hiyo huruma..
 
Na Mimi naendelea kukuuliza, Wewe unasema hakuna Mungu. Na Mimi nakuuliza ulimwengu huu tuliopo nani aliuumba au ulitokeaje( Kama neno "nani" unaona linakukera),, vilivyomo ikiwemo na baba wa babu yako, babu yako mzaa baba yako, baba yako Hadi wewe mmetokeaje au mmetokea wapi
Ahaa, hapo ulitokeaje na tumetokeaje ndiyo maswali sahihi.

Hizo habari za nani ni anthropic bias tu.

Kwanza kabisa, sijawahi kusema najua ulimwengu ulitokeaje. Hili suala ni refu sana na bado linachunguzwa mpaka leo. Kwa kweli hata hiyo dhana ya kutokea nayo inajadilika na kupingika, kwa maana ya kwamba kwa kutegemea na unamaanisha nini kwa neno "ulimwengu" ( Kiswahili hakina maneno yanayoendana na sayansi ya sasa), kutegemea na unamaanisha universe au multiverse, hakuna sababu ya ulimwengu kuwa na mwanzo.

Kwamba hiyo dhana ya kitu kuwa na mwanzo nayo ni bias ya mawazo yetu sisi ambao tunazaliwa na kufa na kila kitu tunachokijua kina mwanzo na mwisho, tunafikiri ulimwengu nao ni lazima uwe na mwanzo.

Ukiangalia sayansi kama za quantum loop, kitu A kinaweza kuwa chanzo cha kitu B, na kitu B kikawa chanzo cha kitu A, kukawa hakuna mwanzo hapo, ni mzunguko tu wa cause and effect, cause A ikasababisha effect B, na effect B ikawa cause ya A. Hakuna mwanzo hapo.

Lakini, kwa vyovyote vile, haya ni mambo ya kuyachunguza na kuyaelewa zaidi. Na njia ya kuyachunguza ni sayansi. Siyo haya mambo ya ramli za waganga wa kienyeji na habari za jadithi za kiroho ambazo hazina uthibitisho au hata logical consistency tu.

Tunaweza kujua kuwa jibu fulani si sahihi, hata kabla ya kujua jibu sahihi ni lipi.

Tunaweza kujua ulimwengu huu haujaumbwa na Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, hata kabla ya kujua ulimwengu huu umetokeaje au kama umetokea at all.

Tunaweza kujua kuwa, katika base ten math, square root ya 2 haiwezi kuwa kubwa kuliko 2, hata kabla ya kuijua square root ya 2.

Tunaweza kujua kuwa mtoto mchanga wa miezi 6 leo hawezi kuwa mama mzazi wa mwanamme mwenye miaka 30 leo.

Katika kutafuta jibu sahihi, kuna kitu kinaitwa "elimination method", kabla ya kupata jibu, tunaangalia, jibu sahihi liko wapi? Kulia au kushoto? Tukiona ni lazima lipo kulia, tunaachana na kushoto. Tukijua kwamba square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2, tunatafuta square root ya 2 kwenye namba zilizo ndogo kuliko 2 tu, zote zilizo kubwa kuliko 2 tunaziacha.

Tukijua kuwa binti mchanga wa miezi 6 leo hawezi kuwa mama mzazi wa mwanamme mwenye miaka 30 leo, tunamuondoa huyo binti wakati tunamtafuta mama mzazi wa huyo mwanamme, hata kabla ya kumpata huyo mama mzazi.

Hivyo hivyo pia, tukijua kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hawezi kuwapo (proof by contradiction, problem of evil, Epicurean paradox), tunaweza kuendelea kutafuta ulimwengu umetokeaje, kama umetokea at all, au watu wametokeaje, bila kujihangaisha na theories za huyo Mungu, kwa elimination method.

Tunaweza kujua jibu fulani si sahihi kabla ya kujua jibu sahihi.

Kujua jibu fulani si sahihi ni elimination ya jibu hilo kutoka majibu sahihi, tunaendelea kutafuta jibu sahihi liko wapi bila ya kujishughulisha na hilo jibu lililojulikana kuwa si sahihi.
 
Tatizo lako Kiranga ni moja tu! Unaunda taswira ya Mungu kwa jinsi unavyomtaka wewe awe!! Yaani unampangia Mungu awe vile unavyotaka wewe. Jambo hilo haliwezekani kamwe!

Mungu ni mtawala,mfalme,tajiri na si muhitaji wa chochote kutoka kwa viumbe.Uwepo wake yeye haukutegemei wewe bali uwepo wako wewe ndio unamtegemea maamuzi yake YEYE.

Ukishalijua hili ndio utaelewa sifa zake Mungu.

Mungu ni mwenye huruma na hakuna mwenye huruma zaidi yake YEYE na vilevile ni mkali wa kuadhibu kwa maana ya hakuna mwenye adhabu kali zaidi yake YEYE.

Mungu ndiye anayegawa Riziki kwa viumbe wake kwa maana hakuna mtoa riziki zaidi yake yeye na huigawa riziki kwa amtakae na kwa kipimo anachokitaka YEYE kutakana na elimu na hekima yake YEYE. Vilevile ameipanga riziki kwa madaraja...kuna ambao amewapa daraja la juu hapa ulimwenguni kwa maana ya utajiri, na kuna ambao amewapa madaraja ya kati na vilevile wapo aliowapa madaraja ya chini. Ameweka mfumo huu kwa elimu na ujuzi wake ili maisha yetu yapate kusonga kwa kutegemea na kutumikiana sisi kwa sisi..kwa maana maskini atamtumikia tajiri ili apate ujira wake ambayo ndio hiyo RIZIKI na vilevile maskini atamuingizia faida tajiri wake ambayo pia ndio RIZIKI.

Huu ni mfumo wa maisha aliouweka Mungu hapa duniani ukiwa kama ni mtihani kwa kila kiumbe ili aone ni nani atakaemuamini na kutenda mema ili mwisho wa siku aje kumlipa malipo MAKUBWA zaidi ambayo ni maisha ya raha za milele ndani ya Pepo. Na yule atakaefeli mtihani eake hapa duniani kwa maana hakuamini na hakutenda mema basi atakumbana na adhabu kali ya moto wa Jahannam.
Tatizo lako huelewi tofauti kati ya mimi kuunda taswira ya Mungu ninayemtaka mimi na mimi kutumia tabia za Mungu mlizozisema nyie wenyewe mnaomuamini Mungu na kuonesha logical inconsistencies na contradictions tu.

Hakuna niliopoweka taswira na tabia za Mungu ninazotaka mimi. Nimenukuu tu tabia za Mungu ambazo zinatajwa na waumini. Nikaonesha makosa ya dhana ya Mungu huyo kuwepo.

Mimi si niliyesema Mungu ni mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.

Waumini ndiyo mmesema hivyo.

Mimi ninachosema ni kwamba, kama kweli Mungu ni mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, Mungu huyo kuumba ulimwengu unaoruhusu mabaya kuwepo ni contradiction.

Kwanza kabisa, umeelewa contradiction hiyo?

Unasema Mungu ni mwenye huruma kubwa.

Kwa nini Mungu mwenye huruma kubwa huyo aumbe dunia inayoweza kuwa na ubaya mkubwa kama tunaouona, ikiwa aliweza kuumba ulimwengu ambao hauna mabaya kabisa?

Kwenye jibu lako la kwamba Mungu katupa mtihani. Mungu anayegawa kila kitu, ikiwa ni pamoja na kugawa uwezo wa kumuamini, kwa nini ahitaji kutupa mtihani wa kutupima tunavyomuamini?

Walimu wanatupa mitihaninkwa sababu hawajui uwezo wetu, wanataka kutupima. Mungu anayejua kila kitu, ambaye ndiye katupa uwezo wa kumuamini au kutomuamini, anatupa mtihani ili iweje?

Yani yeye anajua kila kitu, anajua tutakachofanya kabla hatujakifanya. Yeye ndiye katupa uwezo wa kumuamini au kutomuamini, kwa nini aone kutupa mtihani wa mabaya mengi kuwa ni kitu muhimu?

Unaelewa kuwa Mungu huyo unayemsema ni sadistic, si mwenye huruma yote? Huyo ni Mungu anayefurahia maumivu ya viumbe, kakaa anaangakia Simba anavyomka Swala, anafurahia movie aliyoitengeneza, wakati angeweza kutengeneza movie ambayo Simba na Swala wanakaa pamoja poa tu.

Yani Mungu huyo anakunyima neema ya kumjua, halafu anakupa mtihani wa kumjua, halafu ukishindwa kumjua, anakutupa motoni milele?

Unajua huyo Mungu anakuchoma motoni milele kwa kosa alilolisababisha yeye, wewe hata hujaomba kuzaliwa kwenye ulimwengu ambao yeye kauumba ambao unaruhusu mabaya, umejikuta umezaliwa tu?

Unajua kwamba kati ya Mungu aliyeumba ulimwengu unaoruhusu mabaya kuwepo na mtu aliyejikuta tu kazaliwa katika huo ulimwengu, akafanya mabaya, huyo Mungu ndiye ana kosa kubwa hapo, kwa sababu yeye ndiye muumbaji wa ulimwengu unaoruhusu mabaya, bila yeye kuuumba ulimwengu unaoruhusu mabaya hakuna kiumbe ambacho kingeweza kufanya baya lolote?
 
Hakuna kiumbe kisichomjua MUNGU hapa duniani isipokuwa ni ukaidi tu wa nafsi ila ndani kabisa unajua kuwa hivi vitu havikutokea tu duniani kwa bahati mbaya, yupo aliyeviunda mpaka vikawa.

Jeuri ya afya,Shibe na pumzi uliyopewa bure na Mungu ndiyo inayokuzuzua mpaka unamkana.

Jambo la ajabu sana unasema Mungu mwenye huruma sana hayupo ili hali ushahidi halisi upo ndani ya nafsi yako ....yaani licha ya MUNGU kukuatia pumzi bure,afya bure,ugali wako wa kila siku bure, mke bure, watoto bure,mali bure n.k bila ya kutoa senti tano yako bado unamkana waziwazi kuwa hayupo na wala hajakupatia hizi neema zinazokutia Kiburi , cha ajabu zaidi huruma yake Mungu ni kwamba bado anaendelea kukupatia hizi neema licha ya kuwa unamkana.

JE HAUTAFAKARI ? Kiranga

Je wewe una huruma ya kumhudumia mtoto wako mwenyewe uliyemzaa, yaani unampatia mahitaji yake yote ila mwisho wa siku anakukana mbele ya kadamnasi kuwa wewe sio BABA yake na wala hujamsaidia chochote. Kisha siku ya pili unaamka na unaendelea kumpatia mahitaji wake ya kila siku ila inapofika jioni tena anakukana?

Unayo hii huruma? Jibu ni hapana ,huna!

Ila MUNGU anayo hiyo huruma..
Kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kaumba ulimwengu unaoweza kuwa na ukaidi kwenye suala la kumjua Mungu wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao watu wanaweza kumjua Mungu vizuri bila ukaidi?

Unasema Mungu ana huruma kubwa sana.

Lakini, ulimwengu ambao unasema kauumba, una mabaya mengi, watu wanakufa kwa njaa, kwa majanga ya kiasili, kwa vita, kwa umasikini, kwa ujinga, kwa maradhi, mpaka viumbe wanaishi kwa kuwindana na kuuana, mbona dunia tunayoishi haioneshi kuwa imeumbwa na Mungu mwenye huruma kubwa?
 
Unataka kusema Mungu ni mbaguzi, ana choyo cha kujithibitisha, anatubania, anachagua watu fulani anajithibitisha kwao wamjue bila shaka, wengine anawapotezea?
Mkuu mbona Habari njema za Mungu zinahubiliwa karibia duniani kote.

Pia niwewe tu ndio haujataka kumtafuta, kumuomba, kumjua. Mungu anajua unayopitia na unahitaji nini ila anahitaji u tayari/hiyari/utashi wako ku-confirm.
Ili neema inapokushukia utambue utukufu unatoka wapi.

Ukitaka kuthibitisha hili jaribu kumtegemea MUNGU katika maisha yako arafu kwenye yale matatizo yako yanayokukabili muombe Mungu akusaidie, uone maajabu (wakati huo unatakiwa utilie maanani kwamba MUNGU hajaribiwi, Kwahiyo unakua umeamua kuishi kwa mapenzi ya MUNGU, na sio ili uthibitisho)

Mimi ninavyojua Mungu anaweza kufanya hivyo, sio naongea maneno matupu au naamini tu Hapana nishaona ishara kadha wa kadha na pia kuna watu wengine washatendewa haya mambo.
Wewe unaweza kuthibitisha kuna Mungu yupo nje ya uwezo wa kisayansi? Unaweza kutoa ishara ya kuthibitisha hilo?

Mbona naona kama unanipa mtihani ambao wewe mwenyewe hujaupita?
Haya masuala tumeshayajadili post za Nyuma kwa mifano. Labda hukuzingatia.
 
Mkuu mbona Habari njema za Mungu zinahubiliwa karibia duniani kote.

Pia niwewe tu ndio haujataka kumtafuta, kumuomba, kumjua. Mungu anajua unayopitia na unahitaji nini ila anahitaji u tayari/hiyari/utashi wako ku-confirm.
Ili neema inapokushukia utambue utukufu unatoka wapi.

Ukitaka kuthibitisha hili jaribu kumtegemea MUNGU katika maisha yako arafu kwenye yale matatizo yako yanayokukabili muombe Mungu akusaidie, uone maajabu (wakati huo unatakiwa utilie maanani kwamba MUNGU hajaribiwi, Kwahiyo unakua umeamua kuishi kwa mapenzi ya MUNGU, na sio ili uthibitisho)

Mimi ninavyojua Mungu anaweza kufanya hivyo, sio naongea maneno matupu au naamini tu Hapana nishaona ishara kadha wa kadha na pia kuna watu wengine washatendewa haya mambo.

Haya masuala tumeshayajadili post za Nyuma kwa mifano. Labda hukuzingatia.
Unaelewa kwamba, kama Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote yupo, habari njema za Mungu kuhubiriwa "karibu" dunia yote ni ukatili mkubwa?

Kwa nini Mungu huyo hakuweka habari njema zote kwenye DNA zetu kiasi cha kwamba watu wamuelewe Mungu bika kuhitaji mahubiri?

Mahubiri yana matatizo ya tafsiri, matatizo ya lugha, matatizo ya siasa, matatizo mengi sana.

Pia kuna mahubiri kuhusu maelfu na maelfu ya miungu, kupitia maelfu na maelfu ya dini, watu hawajui washije lipi.

Huoni kuwa hilo linaonesha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wote hayupo? Huoni Mungu huyo angekuwepo, angeweka habari zake zote kwenye DNA ya kila kiumbe kwa njia ambayo kila kiumbe kingemjua, kingemjua jwa ukamilifu, bila utata na bila ya kuhitaji mahubiri?
 
Mungu hayupo.

Habari za Mungu kuwapo ni hadithi za kutungwa na watu tu.
Nakubaliana na wewe kabisa hizi habari ni za kutungwa na zilifichwa ila kwa Sasa zinaanza kufunguka na watu wanaanza kuelewa hizi story

Kiufupi,Mungu ni mawazo ya Binadamu tu , Bila Binadamu hakuna Mungu
 
Back
Top Bottom