Na Mimi naendelea kukuuliza, Wewe unasema hakuna Mungu. Na Mimi nakuuliza ulimwengu huu tuliopo nani aliuumba au ulitokeaje( Kama neno "nani" unaona linakukera),, vilivyomo ikiwemo na baba wa babu yako, babu yako mzaa baba yako, baba yako Hadi wewe mmetokeaje au mmetokea wapi
Ahaa, hapo ulitokeaje na tumetokeaje ndiyo maswali sahihi.
Hizo habari za nani ni anthropic bias tu.
Kwanza kabisa, sijawahi kusema najua ulimwengu ulitokeaje. Hili suala ni refu sana na bado linachunguzwa mpaka leo. Kwa kweli hata hiyo dhana ya kutokea nayo inajadilika na kupingika, kwa maana ya kwamba kwa kutegemea na unamaanisha nini kwa neno "ulimwengu" ( Kiswahili hakina maneno yanayoendana na sayansi ya sasa), kutegemea na unamaanisha universe au multiverse, hakuna sababu ya ulimwengu kuwa na mwanzo.
Kwamba hiyo dhana ya kitu kuwa na mwanzo nayo ni bias ya mawazo yetu sisi ambao tunazaliwa na kufa na kila kitu tunachokijua kina mwanzo na mwisho, tunafikiri ulimwengu nao ni lazima uwe na mwanzo.
Ukiangalia sayansi kama za quantum loop, kitu A kinaweza kuwa chanzo cha kitu B, na kitu B kikawa chanzo cha kitu A, kukawa hakuna mwanzo hapo, ni mzunguko tu wa cause and effect, cause A ikasababisha effect B, na effect B ikawa cause ya A. Hakuna mwanzo hapo.
Lakini, kwa vyovyote vile, haya ni mambo ya kuyachunguza na kuyaelewa zaidi. Na njia ya kuyachunguza ni sayansi. Siyo haya mambo ya ramli za waganga wa kienyeji na habari za jadithi za kiroho ambazo hazina uthibitisho au hata logical consistency tu.
Tunaweza kujua kuwa jibu fulani si sahihi, hata kabla ya kujua jibu sahihi ni lipi.
Tunaweza kujua ulimwengu huu haujaumbwa na Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, hata kabla ya kujua ulimwengu huu umetokeaje au kama umetokea at all.
Tunaweza kujua kuwa, katika base ten math, square root ya 2 haiwezi kuwa kubwa kuliko 2, hata kabla ya kuijua square root ya 2.
Tunaweza kujua kuwa mtoto mchanga wa miezi 6 leo hawezi kuwa mama mzazi wa mwanamme mwenye miaka 30 leo.
Katika kutafuta jibu sahihi, kuna kitu kinaitwa "elimination method", kabla ya kupata jibu, tunaangalia, jibu sahihi liko wapi? Kulia au kushoto? Tukiona ni lazima lipo kulia, tunaachana na kushoto. Tukijua kwamba square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2, tunatafuta square root ya 2 kwenye namba zilizo ndogo kuliko 2 tu, zote zilizo kubwa kuliko 2 tunaziacha.
Tukijua kuwa binti mchanga wa miezi 6 leo hawezi kuwa mama mzazi wa mwanamme mwenye miaka 30 leo, tunamuondoa huyo binti wakati tunamtafuta mama mzazi wa huyo mwanamme, hata kabla ya kumpata huyo mama mzazi.
Hivyo hivyo pia, tukijua kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hawezi kuwapo (proof by contradiction, problem of evil, Epicurean paradox), tunaweza kuendelea kutafuta ulimwengu umetokeaje, kama umetokea at all, au watu wametokeaje, bila kujihangaisha na theories za huyo Mungu, kwa elimination method.
Tunaweza kujua jibu fulani si sahihi kabla ya kujua jibu sahihi.
Kujua jibu fulani si sahihi ni elimination ya jibu hilo kutoka majibu sahihi, tunaendelea kutafuta jibu sahihi liko wapi bila ya kujishughulisha na hilo jibu lililojulikana kuwa si sahihi.