Mkono Mmoja
JF-Expert Member
- Jan 26, 2019
- 3,359
- 6,568
Sayansi hii tuliyonayo duniani ni tone tu la elimu katika bahari ya elimu aliyonayo MUNGU. Kuna mambo mengi anaweza kuyafanya kinyume na hii elimu ndogo aliyotupatia wanaadamu.Mkuu,
Kwa vile sayansi haina majibu ya kila kitu, nikikwambia mimi ndiye Mungu muumba wa kila kitu, ndiye niliyeumba ulimwengu, na kila kitu kilichomo ndani ya ulimwengu, ila jambo hilo huwezi kulijua tu, kwa sababu lipo nje ya sayansi, utakubali? Utakubali maneno yangu kama yanaelezea jambo la ukweli mimi ndiye Mungu muumba vyote?
Mbona hujanijibu swali langu sasa?Sayansi hii tuliyonayo duniani ni tone tu la elimu katika bahari ya elimu aliyonayo MUNGU. Kuna mambo mengi anaweza kuyafanya kinyume na hii elimu ndogo aliyotupatia wanaadamu.
Sita kubali mpaka unithibitishie katika namna ambayo itazidi upeo wa kibinadamu.Mkuu,
Kwa vile sayansi haina majibu ya kila kitu, nikikwambia mimi ndiye Mungu muumba wa kila kitu, ndiye niliyeumba ulimwengu, na kila kitu kilichomo ndani ya ulimwengu, ila jambo hilo huwezi kulijua tu, kwa sababu lipo nje ya sayansi, utakubali? Utakubali maneno yangu kama yanaelezea jambo la ukweli mimi ndiye Mungu muumba vyote?
Unaelewa kwamba ukishataka uthibitisho umeingia kwenye sayansi tayari?Sita kubali mpaka unithibitishie katika namna ambayo itazidi upeo wa kibinadamu.
Mkuu Kiranga kujua maandiko na taratibu nyingine mbalimbali za kidini hiyo ni hatua moja kumjua MUNGU ni hatua nyingine.
Sasa hawa unaowaona wanahubili, unakuta msomi mzima proffessor anaudhulia ibada sio kwamba aliamua tu kuamini kichwa kichwa hapana wengi wao waliona ishara, na wengine hari waliyonayo kiuchumi kiafya ilifanikiswa na MUNGU.
Mkuu wewe ndio haupo...trust meMungu hayupo.
Habari za Mungu kuwapo ni hadithi za kutungwa na watu tu.
Sasa unataka mtu ambaye hayupo aku trust?Mkuu wewe ndio haupo...trust me
Sayansi haijazidi upeo wa kibinadamu mimi nimesema uthibitisho utakaozidi upeo wa kibinadamu.Unaelewa kwamba ukishataka uthibitisho umeingia kwenye sayansi tayari?
Nitakuomba unipe ishara itakayo ashiria kua kweli hiyo ipo nje ya uwezo wa kisayansi.Naweza kukuambia kuwa mimi ni Mungu, hilo lipo nje ya sayansi, na wewe huwezi kuelewa hilo.
Mkuu,Nimekulewa vizuri mkuu... Sasa mimi kama mimi siwasemei wengine, nimetambua/nimegundua kua Mungu Ana deal na mtu mmoja mmoja, atajidhihirisha kwako ukiwa wewe pekeako, Sasa kwa hari kama hiyo nafsi yako inagundua na itakiri kua hapa sijafanyiwa utapeli wala janjajanja za kibinadamu(tricks) utahisi kabisa kua hapa nipo live.
Nadhani hii ndio sababu ya Mungu kuongea na Mtu husika kuliko kundi la watu, Alijua kunawapotoshaji wazee wa propaganda na fitina watawatoa watu mchezoni,
View attachment 2934666
Sayansi haijazidi upeo wa kibinadamu mimi nimesema uthibitisho utakaozidi upeo wa kibinadamu.
Nitakuomba unipe ishara itakayo ashiria kua kweli hiyo ipo nje ya uwezo wa kisayansi.
Mkuu,angetoa tumbo ili tumuabudu vizur, njaa zinatufanya tusione uwepo wake unatuleta dunian tukuabudu mbinguni malaika hawamtoshi kwa nn tumuabudu kwenye shida maelezo yasiwe mengi kiufup mungu wa kwenye vitabu hayupo
Kwaio nani aliumba ulimwengu ! Na vilivyomoMkuu,
Mungu huyo mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.
Huyo Mungu, kidhahania, ni Mungu mwenye tabia poa sana huyo Mungu ni wa peace and love, hana tatizo na kiumbe chochote huyo, yani fikiria wema wowote unaoweza kufanyika, wema wake ni mara infinity ya huo, angekuwa kweli yupo, asingeumba ulimwengu unaoruhusu njaa iwepo.
Huyo Mungu angekuwa yupo na kaumba ulimwengu, mabaya yote yasingewezekana kufanyika, kila kiumbe kingemjua Mungu bila utata. Ulimwengu usingeweza kuwa na tatizo lolote.
Hivyo, kuwepo kwa njaa ni uthibitisho huyo Mungu hayupo.
Kwa nini swali linakuwa "nani"? Huoni kuwa swali lenyewe kwanza limekuja na kasumba ya kujiegemeza kuwa ulimwengu uliumbwa na fulani, tumtafute tu tumjue huyo fulani ni nani?Kwaio nani aliumba ulimwengu ! Na vilivyomo
Na Mimi naendelea kukuuliza, Wewe unasema hakuna Mungu. Na Mimi nakuuliza ulimwengu huu tuliopo nani aliuumba au ulitokeaje( Kama neno "nani" unaona linakukera),, vilivyomo ikiwemo na baba wa babu yako, babu yako mzaa baba yako, baba yako Hadi wewe mmetokeaje au mmetokea wapiKwa nini swali linakuwa "nani"? Huoni kuwa swali lenyewe kwanza limekuja na kasumba ya kujiegemeza kuwa ulimwengu uliumbwa na fulani, tumtafute tu tumjue huyo fulani ni nani?
Kama jibu liko upande tofauti kabisa, na ulimwengu haujaumbwa na fulani yeyote je?
Tatizo lako Kiranga ni moja tu! Unaunda taswira ya Mungu kwa jinsi unavyomtaka wewe awe!! Yaani unampangia Mungu awe vile unavyotaka wewe. Jambo hilo haliwezekani kamwe!Mkuu,
Mungu huyo mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.
Huyo Mungu, kidhahania, ni Mungu mwenye tabia poa sana huyo Mungu ni wa peace and love, hana tatizo na kiumbe chochote huyo, yani fikiria wema wowote unaoweza kufanyika, wema wake ni mara infinity ya huo, angekuwa kweli yupo, asingeumba ulimwengu unaoruhusu njaa iwepo.
Huyo Mungu angekuwa yupo na kaumba ulimwengu, mabaya yote yasingewezekana kufanyika, kila kiumbe kingemjua Mungu bila utata. Ulimwengu usingeweza kuwa na tatizo lolote.
Hivyo, kuwepo kwa njaa ni uthibitisho huyo Mungu hayupo.
Hakuna kiumbe kisichomjua MUNGU hapa duniani isipokuwa ni ukaidi tu wa nafsi ila ndani kabisa unajua kuwa hivi vitu havikutokea tu duniani kwa bahati mbaya, yupo aliyeviunda mpaka vikawa.Mkuu,
Mungu huyo mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.
Huyo Mungu, kidhahania, ni Mungu mwenye tabia poa sana huyo Mungu ni wa peace and love, hana tatizo na kiumbe chochote huyo, yani fikiria wema wowote unaoweza kufanyika, wema wake ni mara infinity ya huo, angekuwa kweli yupo, asingeumba ulimwengu unaoruhusu njaa iwepo.
Huyo Mungu angekuwa yupo na kaumba ulimwengu, mabaya yote yasingewezekana kufanyika, kila kiumbe kingemjua Mungu bila utata. Ulimwengu usingeweza kuwa na tatizo lolote.
Hivyo, kuwepo kwa njaa ni uthibitisho huyo Mungu hayupo.
Ahaa, hapo ulitokeaje na tumetokeaje ndiyo maswali sahihi.Na Mimi naendelea kukuuliza, Wewe unasema hakuna Mungu. Na Mimi nakuuliza ulimwengu huu tuliopo nani aliuumba au ulitokeaje( Kama neno "nani" unaona linakukera),, vilivyomo ikiwemo na baba wa babu yako, babu yako mzaa baba yako, baba yako Hadi wewe mmetokeaje au mmetokea wapi
Tatizo lako huelewi tofauti kati ya mimi kuunda taswira ya Mungu ninayemtaka mimi na mimi kutumia tabia za Mungu mlizozisema nyie wenyewe mnaomuamini Mungu na kuonesha logical inconsistencies na contradictions tu.Tatizo lako Kiranga ni moja tu! Unaunda taswira ya Mungu kwa jinsi unavyomtaka wewe awe!! Yaani unampangia Mungu awe vile unavyotaka wewe. Jambo hilo haliwezekani kamwe!
Mungu ni mtawala,mfalme,tajiri na si muhitaji wa chochote kutoka kwa viumbe.Uwepo wake yeye haukutegemei wewe bali uwepo wako wewe ndio unamtegemea maamuzi yake YEYE.
Ukishalijua hili ndio utaelewa sifa zake Mungu.
Mungu ni mwenye huruma na hakuna mwenye huruma zaidi yake YEYE na vilevile ni mkali wa kuadhibu kwa maana ya hakuna mwenye adhabu kali zaidi yake YEYE.
Mungu ndiye anayegawa Riziki kwa viumbe wake kwa maana hakuna mtoa riziki zaidi yake yeye na huigawa riziki kwa amtakae na kwa kipimo anachokitaka YEYE kutakana na elimu na hekima yake YEYE. Vilevile ameipanga riziki kwa madaraja...kuna ambao amewapa daraja la juu hapa ulimwenguni kwa maana ya utajiri, na kuna ambao amewapa madaraja ya kati na vilevile wapo aliowapa madaraja ya chini. Ameweka mfumo huu kwa elimu na ujuzi wake ili maisha yetu yapate kusonga kwa kutegemea na kutumikiana sisi kwa sisi..kwa maana maskini atamtumikia tajiri ili apate ujira wake ambayo ndio hiyo RIZIKI na vilevile maskini atamuingizia faida tajiri wake ambayo pia ndio RIZIKI.
Huu ni mfumo wa maisha aliouweka Mungu hapa duniani ukiwa kama ni mtihani kwa kila kiumbe ili aone ni nani atakaemuamini na kutenda mema ili mwisho wa siku aje kumlipa malipo MAKUBWA zaidi ambayo ni maisha ya raha za milele ndani ya Pepo. Na yule atakaefeli mtihani eake hapa duniani kwa maana hakuamini na hakutenda mema basi atakumbana na adhabu kali ya moto wa Jahannam.
Kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kaumba ulimwengu unaoweza kuwa na ukaidi kwenye suala la kumjua Mungu wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao watu wanaweza kumjua Mungu vizuri bila ukaidi?Hakuna kiumbe kisichomjua MUNGU hapa duniani isipokuwa ni ukaidi tu wa nafsi ila ndani kabisa unajua kuwa hivi vitu havikutokea tu duniani kwa bahati mbaya, yupo aliyeviunda mpaka vikawa.
Jeuri ya afya,Shibe na pumzi uliyopewa bure na Mungu ndiyo inayokuzuzua mpaka unamkana.
Jambo la ajabu sana unasema Mungu mwenye huruma sana hayupo ili hali ushahidi halisi upo ndani ya nafsi yako ....yaani licha ya MUNGU kukuatia pumzi bure,afya bure,ugali wako wa kila siku bure, mke bure, watoto bure,mali bure n.k bila ya kutoa senti tano yako bado unamkana waziwazi kuwa hayupo na wala hajakupatia hizi neema zinazokutia Kiburi , cha ajabu zaidi huruma yake Mungu ni kwamba bado anaendelea kukupatia hizi neema licha ya kuwa unamkana.
JE HAUTAFAKARI ? Kiranga
Je wewe una huruma ya kumhudumia mtoto wako mwenyewe uliyemzaa, yaani unampatia mahitaji yake yote ila mwisho wa siku anakukana mbele ya kadamnasi kuwa wewe sio BABA yake na wala hujamsaidia chochote. Kisha siku ya pili unaamka na unaendelea kumpatia mahitaji wake ya kila siku ila inapofika jioni tena anakukana?
Unayo hii huruma? Jibu ni hapana ,huna!
Ila MUNGU anayo hiyo huruma..
Mkuu mbona Habari njema za Mungu zinahubiliwa karibia duniani kote.Unataka kusema Mungu ni mbaguzi, ana choyo cha kujithibitisha, anatubania, anachagua watu fulani anajithibitisha kwao wamjue bila shaka, wengine anawapotezea?
Haya masuala tumeshayajadili post za Nyuma kwa mifano. Labda hukuzingatia.Wewe unaweza kuthibitisha kuna Mungu yupo nje ya uwezo wa kisayansi? Unaweza kutoa ishara ya kuthibitisha hilo?
Mbona naona kama unanipa mtihani ambao wewe mwenyewe hujaupita?
Unaelewa kwamba, kama Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote yupo, habari njema za Mungu kuhubiriwa "karibu" dunia yote ni ukatili mkubwa?Mkuu mbona Habari njema za Mungu zinahubiliwa karibia duniani kote.
Pia niwewe tu ndio haujataka kumtafuta, kumuomba, kumjua. Mungu anajua unayopitia na unahitaji nini ila anahitaji u tayari/hiyari/utashi wako ku-confirm.
Ili neema inapokushukia utambue utukufu unatoka wapi.
Ukitaka kuthibitisha hili jaribu kumtegemea MUNGU katika maisha yako arafu kwenye yale matatizo yako yanayokukabili muombe Mungu akusaidie, uone maajabu (wakati huo unatakiwa utilie maanani kwamba MUNGU hajaribiwi, Kwahiyo unakua umeamua kuishi kwa mapenzi ya MUNGU, na sio ili uthibitisho)
Mimi ninavyojua Mungu anaweza kufanya hivyo, sio naongea maneno matupu au naamini tu Hapana nishaona ishara kadha wa kadha na pia kuna watu wengine washatendewa haya mambo.
Haya masuala tumeshayajadili post za Nyuma kwa mifano. Labda hukuzingatia.
Nakubaliana na wewe kabisa hizi habari ni za kutungwa na zilifichwa ila kwa Sasa zinaanza kufunguka na watu wanaanza kuelewa hizi storyMungu hayupo.
Habari za Mungu kuwapo ni hadithi za kutungwa na watu tu.