Naomba nitoe mchango wangu,,,,ndoto waweza zielezea kwenye uhalisia,vizuri kabisa. Changamoto ni ipi?Mimi nalala bila sauti za music wala taarifa ya habari, na mazingira yangu ni ya ukimya hata wakati wa mchana tu,
Bado swali langu ni; Unaweza kuelezea ndoto ambazo zinakuja kwenye uhalisia ?
Au hadi nizielezee hizo ndoto utaelewa nini hasa namaanisha ?
Nguvu zetu za kiroho ziko masafa ya chini,ndio maana akili ikiwa live(imeamka) inakumbuka nusu nusu au haikumbuki kabisa kuhusu nini kimeotwa.
Nijuavyo mpaka sasa...ndoto hutokea pale akili inapokuwa imelala(zile njia 5 za fahamu,ngozi,ulimi,masikio,macho na pua). Ndoto ni muda ambao mwili wa roho umetawala dimba,hausumbuliwi na akili imejaa illusion (ufeki).
Hakuna ndoto ya uongo,matukio ya kindoto ni kweli tupu,ile ni roho yako mwanadamu/kiumbe. Ni muda ambao roho inakuonesha yaliyopita,yaliyopo na yajayo. Issue ni kwamba tumetawaliwa sana na nafsi(akili) so tumevunja/hatuendani na kanuni za kiroho/kimasafa...ndio maana tunasahau sana tuyaotayo.
Kwenye ule utatu babkubwa.....MWILI,NAFSI NA ROHO huyu ndugu yetu nafsi anatuangusha sana,anashindwa kumjua vizuri roho na kumfuata. Sisi ni ROHO mwili na nafsi ni vitu vya kupotea. Bodi na engine vitakwenda lakini nguvu iliyosababisha viwepo itabakia.
Zingatia...nguvu haitengenezeki/ haiharibiki na wala haifi. Huamka na kulala basi. Tujifunze kuiamsha daima,ili tuitumie ipasavyo,NI ZAWADI YETU NA INDANI MWETU.