Maswali yako mengi unayouliza na unayorudia kuuliza sitakueleza kwa kumtumia sayansi psychology au logic Sasa ivi naomba Nitumie BUSARA(WISDOM);
KATIKA ULIMWENGU WA KIROHO NDIO KWENYE SIRI YA HAYA MASWALI NA CONTRADICTION ZOTE
Mkuu unatakiwa uelewa misingi mikuu na namna binadamu aliyoubwa na misingi hiyo inatendaje kazi.
Kama unavyoona binadamu muundo wake umejumuishwa na vitu hivi;
A).LEVEL 1.
1. Mifupa(skeleton)
2. Nyama(skeleton muscles)
3. Mishipa ya fahamu(nerve brain & spinal)
B). LEVEL 2.
1. Mwili (human body)
Mwili unahusisha viungo vyote vya mwili tunavyoviona kwa macho na ndio vinavyotuwezesha kuishi kwenye dunia(designed to conform to the planet earth, ukipelekwa planet nyingine itatokea shida).
2. Nafsi(soul)
Nafsi inahusika na fikra upeo, utashi, hiyari ya mtu. Hapa ndipo kuna minds(conscious unconscious na subconscious)
Katika nafsi, ndio pana darana/link kati ya ulimwengu wa mwili na wa rohoni na hiyo link ni kama chujio ina filter na ku-select mambo yakuwasilishwa rohoni
Yaani kama hauna imani na unachokiomba, unamashaka, hakuna nia ya dhati, unajaribu(inamaana hakuna uhakika). Kwa lugha nyingine yaani hauko serious na Ukitakacho, taarifa zako hazitavuka kwenda ulimwengu wa kiroho yaani hilo sahau kabisa.
SOMA HAPA;
Na ndio maana zamani zilikuwa zinatolewa sadaka za kuchinja wanyama sometimes hata mtu anatolewa hafara moja ya lengo kuu ni kumuandaa kisaikolojia mhusika hata kama alikua anatania automatically anaona kumbe haya mambo yako serious hapo atakua makini sana Sasa mtu akishakua kwenye hali imani yake inaongezeka katika conscious mind yake (
na hata iwe kidogo tu inaweza kuhamisha mlima kama huyo mtu ataamuru hivyo)
Hivyo taarifa zitapokelewa na subconscious mind na hii subconscious mind haipokei tu taarifa ni mpaka uishawishi... Hadi apo taarifa zinakua zimepata kibali kuingia ulimwengu wa kiroho Sasa hapa kwenye hii Junction kuna wadukuzi wanaweza waka-hack taarifa zikaenda kusiko takiwa hii itatokea tu kama hauna ulinzi au nguvu kiroho... Na kwanini wahaki ni kwasababu kuna ulimwengu wa Roho wa NURU na wa giza washirikina wanaweza wakakwamisha maombi yako au baraka zako (nyota)
Kwa wale wanaotegemea binadamu wenzao/waganga wa jadi wa ramli hiki ndio huwa kinafanyika (mechanism behind katika tasnia ya uganga. Ili taarifa zako zimfikie shetani ajue namna ya kukusaidia ni lazima wewe mhusika uziruhusu sasa unaziruhusu vipi na hauna imani ya kutosha ndio yanatengenezwa mazingira ya wewe kua serious na jambo unalolitaka(ndio imani yenyewe hiyo) Mganga naye pasipo kujua anaamrisha tu na mapepo/majini anajikuta anakupa masharti, ugumu na urahisi wa masharti utategemea na uzito/ugumu wa moyo wako kuamini kama jambo lako ni kubwa na unawaziwasi Mganga hataliweza basi majini ya mganga yanamuelekeza mganga kuwa huyo itatakiwa amtoe mama yake(kwanini mama? wewe mwenyewe fikilia kati ya mama na baba yupi anauzito kwako yupi akifa utaumia zaidi)
Sasa mganga akikutajia masharti hayo lazima medula ublongats itikisike na lengo linakua limetimia kuwa wewe mwenye shida nafsi yako imefanikisha kuwasilisha taarifa katika ulimwengu wa Roho wa giza.
Sasa kwa upande wa MUNGU ulimwengu wa ROHO WA NURU aliboresha/ali-update namna ya kuwasiliana nae. Alitambua kua kuna kuna watu watakua na hali tofauti masikini, matajili wengine ni wagumu tu (DNA kizazi cha kwanza kinaweza kua kipore kikarimu lakini kwasababu kunamuungiliano vizazi vinavyofaatia vitakengeuka katika vinasana(Genetic Segregation))
Hivyo basi MUNGU akaja na mpango wa YESU (Hii ni kitaalumu sana ndio maana watu wengi pasipo uwezo wa roho mtakatifu hawaelewi na wanaweza wakaendelea kubisha, very very technical).
Katika hii new testament au new Updated and simplified version) hatuhitaji tena mambo ya kafara. Anatakiwa YESU. Kwanini kwasababu Yesu amekuja na ulinzi security patch level ambayo ukituma maombi kwa MUNGU BABA kwa kuambatanisha na jina la YESU basi taarifa hiyo katika subconscious mind haitadukuliwa na wadukuzi/hacker katika ile link ya kuingia ulimwengu wa Roho wa Nuru.
Sasa Yesu Aliijua kua kuna hii (subconscious mind) link kati ya duniani na Rohoni na Alijua kua mtu ukiwa unajitosheleza kwa mali afya nk kisaikolokjia utakua umebweteka/comfortable hivyo hautakua na nguvu au imani yakuishawishi subconscious mind yako ukuunganishe na ulimwengu wa rohoni.
Na ndio maana alipouliza na matajili kua wao wanatekeleza mapenzi ya MUNGU je wafanye nini cha ziada Yesu akawaambia Wauze mali zao zote, kisaikolojia lengo linakua ni hilo ukikosa mali huwezi kua comfortable na lazima uwajibike kwa majukumu yatakayokukabili na utakua na imani.
Na ndio maana alisema ni vigumu kwa tajiri kuingia ufalme wambinguni kuliko ngamia kupenya kwenye tundu la sindano.
Na saikolojia hii hii ndio inaweza kuelezea kwanini watoto wamatajili walio wengi wanakuaga na changamoto.
SASA KATIKA HAYO MATABAKA MAWILI (MWILI NA NAFSI) NDIO YANACHUNGUZIKA KIMANTIKI NA KISAYANSI.
ILA HILI TABAKA LA KIROHO NI MFUMO TOFAUTI KABISA UFAHAMU WETU KIULIMWENGUNI MWENGUNI AIDHA IWE UNIVERSE AMA MULTIVERSE HAUWEZI KUNG'AMUA.
KWAHIYO KINACHOTAKIWA NI UAMINI(IMANI) TU KAMA NI RIZIKI MILANGO ITAFUNGUKA, UFAHAMU UTAONGEZEKA, KAMA NI KUVUMBUA TECHNOLIGIA MPYA ITAVUMBUKA,NAKADHALIKA LAKINI KUJUA IMEKUAJEKUAJE WALA USIPOTEZE MUDA UTAJUA UKIFIKA HUKOHUKO MUDA UKIFIKA.
3. Roho (spirit(Holly spirit)
HUKU KUKO ABOVE MY PAYCHECK.
Sasa mkuu
Kiranga mimi naona huwezi kutumia elimination method wakati kuna kigezo cha kiroho hujakizingatia.
Na isitoshe kwani mwanasayansi yeye ndio nani Yani!? hadi aseti standards za ulimwengu huu, ye si ni sehemu ya uumbaji wa MWENYEZI MUNGU. kama kuna vitu viko nje ya ufahamu wetu wakubali yaishe... Kama watakomaa basi watakomaa mpaka watakua skeleton makabbulini.
Mwenye kukosoa, kuongeza, kuuliza Karibuni sana.