Jifunze kumuacha aende

Jifunze kumuacha aende

Umetafsiri clip ya T.D.Jakes ya LET THEM WALK....umeongezea nguruwe tu kunogesha [emoji2]
 
Dah umenikumbusha tukigombana na my boyfriend lazima nimuulize ana conclude vipi,ili akisema tuachane ye ndo awe responsible for his words[emoji23] .....

Na mara nyingi hatoi conclusion...utasikia tu "me sipend tugombane sema sometimes ue unaangalia"

Btw ikitokea tukaachana kumwacha aende itakua ngum kumeza...
Mazoea yana tabu[emoji22]
 
Nakumbuka siku nyingi saaaana. Tulipendana, alinifanyia visa, ila ilikua ngumu kumwacha aende.
One day nikasema ntalazimisha mapenzi hadi lini? Nikaona hakuna future mbeleni, ikabidi NIMWACHE AENDE, na alijua nampenda sana cwez kwenda, lakini ikabidi tu NIMWACHE AENDE, hakuamini lakini ndo hvo NILIMWACHA AENDE...........
Asante Mungu kuniepusha na huyo mtu aliyejifanya ni handsome hakataliwi na mtu,
 
Marufuku kukata tamaa,acha aende zake. Kama ipo ipo tu.
 
Nakumbuka siku nyingi saaaana. Tulipendana, alinifanyia visa, ila ilikua ngumu kumwacha aende.
One day nikasema ntalazimisha mapenzi hadi lini? Nikaona hakuna future mbeleni, ikabidi NIMWACHE AENDE, na alijua nampenda sana cwez kwenda, lakini ikabidi tu NIMWACHE AENDE, hakuamini lakini ndo hvo NILIMWACHA AENDE...........
Asante Mungu kuniepusha na huyo mtu aliyejifanya ni handsome hakataliwi na mtu,

Inafanana sana na yangu, alijua nampenda sana kwhy akawa ananisumbua sana. Basi siku moja niliamka tu asb nikajisemea its over now,let him go! Badae akanipigia simu nikamwambia mm nimechoka,tafuta mtu mwingine. Akajibu kwa dharau akijua labda natafuta kiki ya kubembelezwa ila haamini hd leo.
 
ETI MUACHE AENDE KUMBE UNA KIBAMIA NA HATA UJITUMI KUPIGA MECHI VIZURI.....ACHA WAJIFARIJI...MUACHE AENDE
 
Hii nimeitoa mahali… Soma itakusaidia Sanaa!

• Kamwe usihisi kama ulimwengu ndio unakaribia mwisho pale akupendae anapokuacha.

MUACHE AENDE !

• Kujaribu kumlazimisha mtu akupende ni sawa na kujaribu kumlazimisha Nguruwe kutambua usafi na uzuri. Usimlazimishe akupende, mwache mwenyewe akupende, kama hakupendi...achana nae..

MWACHE AENDE !

• Wewe ni wa thamani mno kulilia penzi. Mtu ambae anakupenda kweli atakuheshimu na hataku 'treat' kama uchafu. Kama atakuchukulia wewe kama uchafu...

MUACHE AENDE !

• Usipoteze muda wako wa thamani kujaribu kumshawishi au kuomba mapenzi. Mtu mwingine pembeni anakupenda wewe kwa dhati, ila wewe uko busy mno kumuogesha nguruwe! Kwanini?

MUACHE AENDE !

• Usikasirike pale mtu wako anapompenda mwingine tofauti na wewe. Siku zote hua ni vigumu kumshawishi NYANI kwamba Asali ni tamu kuliko ndizi...

MUACHE AENDE !

• Mwanamke/mwanaume yeyote anaekuchukulia kirahisi siku zote atachukulia faida kwako, atakugeuza atakavyo kama chapati akijua hufurukuti, yeye sio Mungu wa kukufanya atakavyo...

MUACHE AENDE !

• Kuna watu hawatakupenda hata kama utajitoa kiasi gani kwao. Ni sawa tu. Kukukataa kwao haimaanishi kwamba una kitu kibaya, bali ni maana kwamba hawako kwa ajili yako. Usilazimishe duara kuwa pembe tatu...

MUACHE AENDE !

CHA KUJIFUNZA

• Hauwezi badilisha maoni mabaya ya watu juu yako, ila unaweza ukazuia maoni yao mabaya yasikubadilishe wewe kama wewe!

• Acha kichwa chako kiongoze moyo wako kukuondoa katika mahusiano sumu. Lengo la mahusiano sio kuleta mafadhaiko ila ni kuongeza furaha juu ya ile uliyokuwa nayo mwanzoni ulipokuwa haupo ktk mahusiano.

NI NGUMU SANA ILA KWA MUSTAKABALI WA FURAHA YAKO YA SASA NA YA BAADAE ME NAKWAMBIA MUACHE AENDE MPE NA NAULI KABISA!

Kama ipo ipo tu...!
 
Hili bandiko limenigusa sana, na mimi nafkria kufanya uamuzi huu japo kinachonikera je ni nitaachana na wangapi? Je na mwingine nitakaye mpata hali ikiwa hivi italeta picha gani kwenye jamii?
 
Back
Top Bottom