Jifunze kumuacha aende

Jifunze kumuacha aende

ni vile watu huwa hawaelewi tu..as long as unadate na binadamu mwenzio na sio malaika basi mitafaruko lazima iwepo..kukimbilia kuachana sio suhulisho la matatizo ya mahusiano..kikubwa ni kukaa Chini na kurekebishana.
Upo sahihi kwa upande...

Nilivomuelewa mleta mada yapo ya kuvumiliana na kuchukuliana lakini inapofika point ya mwisho unaona unatumia muda mwingi kuumia kwenye uhusiano uliopo badala ya furaha 60% huna budi kumwacha aende...

Kuna watu wanapendwa hawapendeki hapo utang'ang'ania na kusema unapigania penzi au nikujibebesha gunia la misumari tu?

Tujifunze kuacha u ng'ang'anizi... Ushaona mtu haridhiki nawe mpe uhuru wa kua na anaeridhika nae kiroho safi tu
 
Mim nilimuacha akaenda ila wazazi na ndugu zake wanasikitika sana wanasema hayupo mahali sahihi na wanaomba suluhu daily ila kwa alichonifanyia nahisi kama moyo umegoma kumsamehe cz alifanya kosa nikamsamehe akaona sjasamehe kwa dhati akarudia kosa lile lile la kucheat nikammwaga mazima.
 
Ukweli roho inanisonona
Tena moto hadi sijapona
Ila naamini Mola ataniona
Nitakuja pata wakuniponya
Ila tu chonde ma nikuombe
Usiniseme vibaya
Tena nakuombea kuongezewa
Kwa Mola mwaya

Alfajiri huwa ni kitendawili
Nafikiri pindi tukiwa wawili
Tena nakiri inanitesa mwili
Bora tu niache
Nibaki mwenyewee [HASHTAG]#Mustapha[/HASHTAG]
 
JIFUNZE KUMUACHA AENDE
• Kamwe usihisi kama ulimwengu
ndio unakaribia mwisho pale
akupendae anapokuacha.

MUACHE AENDE !
• Kujaribu kumlazimisha mtu
akupende ni sawa na kujaribu
kumlazimisha Nguruwe kutambua
usafi na uzuri. Usimlazimishe
akupende, mwache mwenyewe
akupende, kama hakupendi...

MWACHE AENDE !
• Wewe ni wa thamani mno kulilia
penzi. Mtu ambae anakupenda
kweli atakuheshimu na hataku
'treat' kama uchafu. Kama
atakuchukulia wewe kama uchafu...

MUACHE AENDE !
• Usipoteze muda wako wa
thamani kujaribu kumshawishi au
kuomba mapenzi. Mtu mwingine
pembeni anakupenda wewe kwa
dhati, ila wewe uko busy mno
kumuogesha nguruwe! Kwanini?

MUACHE AENDE !
• Usikasirike pale mtu wako
anapompenda mwingine tofauti na
wewe. Siku zote hua ni vigumu
kumshawishi NYANI kwamba Asali
ni tamu kuliko ndizi...

MUACHE AENDE !
• Mwanamke/mwanaume yeyote
anaekuchukulia kirahisi siku zote
atachukulia faida kwako,
atakugeuza atakavyo kama chapati
akijua hufurukuti, yeye sio Mungu
wa kukufanya atakavyo...

MUACHE AENDE !
• Kuna watu hawatakupenda hata
kama utajitoa kiasi gani kwao. Ni
sawa tu. Kukukataa kwao
haimaanishi kwamba una kitu
kibaya, bali ni maana kwamba
hawako kwa ajili yako. Usilazimishe
duara kuwa pembe tatu...

MUACHE AENDE !
CHA KUJIFUNZA
• Hauwezi badilisha maoni mabaya
ya watu juu yako, ila unaweza
ukazuia maoni yao mabaya
yasikubadilishe wewe kama wewe!
• Acha kichwa chako kiongoze
moyo wako kukuondoa katika
mahusiano sumu. Lengo la
mahusiano sio kuleta mafadhaiko
ila ni kuongeza furaha juu ya ile
uliyokuwa nayo mwanzoni
ulipokuwa haupo ktk mahusiano.

NI NGUMU SANA ILA KWA
MUSTAKABALI WA FURAHA YAKO YA
SASA NA YA BAADAE ME NAKWAMBIA
MUACHE AENDE MPE NA NAULI
KABISA!
 
Back
Top Bottom