Infinite_Kiumeni
JF-Expert Member
- Jan 23, 2023
- 382
- 687
Natamani ningetumia muda mwingi zaidi pamoja naye. Natamani ningekua namsikiliza na kuongea naye. Natamani ningemtongoza mapema kabla jamaa hajamchukua. Saivi yupo na bwana mwingine. Hiyo ni mifano tu ya majuto. Ukiona unatumia “nge” sana ujue upo kwenye majuto.
Ni kweli umri unaenda lakini haupo unapotaka. Lakini hata ukisema hivyo kiasi gani haisaidii.
Sababu huwezi rudisha muda nyuma. Ila kwa kuwa upo hai leo ni nafasi mpya Mungu amekupatia ili ushughulikie uliyokosea. Unapokaa kujuta maana yake hautumii vizuri huu muda Mungu amekupatia.
Makosa yapo tu. Hakuna mwenye kinga ya kukwepa makosa. Ingekuepo mi ningekua wa kwanza kuichukua. Sababu nimefanya mengi. Lakini hiyo ndo njia pekee ya kujifunza. Sababu, unapata mrejesho wa kitu gani hakifai na ukiache. Usiogope kumtongoza mwanamke ukihofia utakosea. Usiogope kuonesha msimamo wako ukihofia utaachwa. Ukifanya hivyo na ukakosea utakua umejifunza.
Usipoteze muda kujuta ndugu yangu. Usijitukane au kujiumiza kwa kukosea kitu. Japo tumezoeshwa tangu shule kwamba ukikosea we ni mbaya na unaadhibiwa. Lakini nje ya shule, makosa ni shule yenyewe. Hivyo, usikubali hiyo shule ikupite kwa kukalia majuto.
Pia, usikubali mtu akushushe kwa makosa uliyofanya. Wala kukusema vibaya. Mwambie tu “makosa yameshatokea haisaidii kubishana, cha msingi ni kusonga mbele na kuchukua somo”.
Kama hujawahi kukosea. Ujue kuna sehemu unakosea. Ujue haukui bali upo sehemu hiyo hiyo. Ujue haujaribu vitu vipya. Ukweli ni kila mtu anafanya makosa. Iwe kazini au nyumbani. Wengi wanajifanya hawakosei na inakufanya ujione vibaya ukikosea. Jiwekee kwamba chochote utakachokosea utapata somo la kujifunza.