jamani na mimi utanifungishaMahitaji
1)Tambi 500g
2) maji 3-4cups
3)sukari 1 cup
4)1/4 hiliki iliyotwangwa
5)tui la nazi 1 cup
6)samli 1 tablespoon.
7)Arki ya rose au flavor yoyote unayopendelea
Namna ya kutaarisha
1)changanya maji,sukari,hiliki na tui la nazi kwenye sufuria
2)weka kwenye moto mdogo mdogo hadi vichemke
3)vunja vunja tambi na uweke
4)pika hadi tui la nazi likauke
5)pakaza samli juu yake
6)washa oven 300°-350° then oka mkae wako....hakikisha unawiva vizuri...
7)mkate wa tambi tayari kwa kuliwa...
mpenzi na mimi nipikie basiAhsante...Enhee mtam:smile-big: crispy on top and soft in the middle...delicious!!!Karibuni tule!
Afadhali umenitia moyo best....
mimi nimejaribu vitumbua mara kadhaa....
mara wananiambia vile vikaangio havijazoea mata sijui nini. kwa kifupi huwa naishia kuchemsha uji kwenye mafuta.....
nikaamua kujiachia zangu
asante kwa ushauri but believe me huwa vinakuwa vimeumuka, sijui hayo majanga yanatokea wapiDada Fixed Point,
Tia Hamira vizuri (Hamira 1 teaspoon)
Kisha weka sehemu ya joto ili uimuke (inavyo onyesha unavipika kabla havija umuka).
Shukran.
Asante nilikua na hamu sana ya kupika hii kitu!b blessed, japokuwa nahisi nitakua na maswali mawili matatu
Uliza tu usijali..
Ok, ujazo wa kikombe ni wa robo kilo? Na hicho kiwango ni serving ya watu wangapi?
Acha tu tukucheke khaaaaaaa
Kisa cha kunicheka ni nini?...
asante kwa ushauri but believe me huwa vinakuwa vimeumuka, sijui hayo majanga yanatokea wapi
ha ha haaa, jichekee mwaya......Kanichekesha fixedpoint.kasema yeye kaishia kuchemsha uji kwenye mafuta
Huu mkate nilishapika ukawa hivyo ila haukuiva alafu ulikuwa na harufu ya amira hata sikujua kosa no nn cjarudia tena
Uliweka hamira nyingi? Na moto ulikua mkali