haya jamani leo ni siku nyingine ambayo ninataka tupike mkate kwaajili ya familia.
mkate
mkate ni chakula ambacho huliwa wakati wa kufungua kinywa.hupikwa kwa kutumia unga wa ngano ama wa muhogo lakin huwa na kiasi kukubwa cha wanga na hivyo unapotumiwa kama kifungua kinywa hukusudiwa kumpatia mlaji nguvu na joto mwilini.
sasa tuangalie jinsi ya upish wa mkate.
mahaitaji:
a) unga wa ngano kg 1 (kwa familia yenye watu wengi let say 4)
b)hamira gm 50
c)mayai 4
d) chumvi kijiko kimoja cha chai
e)sukari nijiko 2 vya chakula
f) maziwa fresh robo l500 ml kama unauwezo kama la basi tumia maji.
njia.
1) chekecha unga wa ngano kwenye chekeche ili kuondoa particles kubwa pamoja na kuingiza hewa ndani ya chembe za unga.
2) weka hamira chumvi pamoja na suukari kisha koroga kwa mkono hadi uchanganyike vizuri kabisa.
3) koroga mayai yako 4 pembeni kwenye bakuli kisha mimina koroga yachanganyike ndipo uyamimine kwenye mchanganyiko wako uyachanganye kwa mikono.
4) tia maziwa kwenye mchanganyiko wako na kisha ukande unga kwa vidole vyako hadi ulainike uwe kama wa kupikia chapati. hakikisha wakat unaukanda usizidishe maji manake kadiri unga unavyozidi kuumuka ndivyo unavyozidi kuwa laini. wakati wa kukanda kunja vidole vyako vinne na uvitumie kukandia unga usitoboe unga kwa vidole kwani hautaukanda zaidi ya kuutoa hewa tu.
5) chukua chombo chako cha kukokea kipake blue band kwa ndani kisha kata unga kwa size ya chombo chako na uutengeneze kwa umbo la tin yako ndipo uuweke. kama huna baking tins za mkate waweza kutumia hata tin ya cake ila uzikate kwa maumbo ya mstatili. kama nacho hiki huna basi tumia sufuria yako ipake blue band ukate unga kwa umbo la viduara uueke ndani visiwe vikubwa sana yawe na umbo dogo la wastani tu.
6) washa oven yako kwa nyuzi joto 120 dk kabla, kisha weka chombo chako cha kuokea na funga mlango. subiria baada ya dk 30 mkate wako utakuwa umesha iva. ii kujua kama umeiva vizuri chukua kitu chenye ncha kali choma kwenye mkate basi kile chombo kikitoka kikavu jua mkate wako uko tayari.
zima jiko na toa mkate wako nje uweke pakavu ili upoe. kumbuka kwamba mkate kwa ajili ya afya hufaa uliwe siku moja baada ya kuokwa. hapa ahauwa na ladha nzuri zaid na huwa umesha lainika vya kutosha. usiufunike mkate wako kama bado haujapoa usije ukajaa mvuke. na usiuweke kwenye unyevu.
mkate huu waweza kuutumia kutengenezea sand wich ama kuliwa jinsi ulivyo tu.
haya basi nawatakieni mapish mazuri kwaajili ya sikukuu ya x-mass na mwaka mmpya.
mke mwezangu
AshaDii nakuomba uwaekee ile picha ya mkate tunayopikaga nyumbani kwajili ya chai