Jifunze mapishi na namna mbalimbali za kupika mkate

Jifunze mapishi na namna mbalimbali za kupika mkate

I swear ungekuwa hujaolewa ningeleta posa kwenu asap

mapishi yoote unayoweka humu unanigusa pale pale
mkate huu ndo ugonjwa wangu..

yaani chai ya mchaichai na mkate wa kumimina na katlesi asubuhi dah...

acha kabisa
 
Hahahahahaha The Boss...na chai ya tangawizi jeeee?
 
Last edited by a moderator:
Toobah! Kuna mkate wa tambi? Manake hii kazi ya kupika nihakikishe paw haibwi imeshanichosha. Haya darasa jipya farkhina.

@fized point, mchanganyiko unatia maji mengi. Na kwenye kikaango haujaweka mafuta ya kutosha. Tia kijiko kizima cha kulia chakula kikaangoni na moto uwe mkali kiasi.

Shoga angu upo mkate wa tambi nitaweka recipe yake soon inshallah..
 
Last edited by a moderator:
Toobah! Kuna mkate wa tambi? Manake hii kazi ya kupika nihakikishe paw haibwi imeshanichosha. Haya darasa jipya farkhina.

@fized point, mchanganyiko unatia maji mengi. Na kwenye kikaango haujaweka mafuta ya kutosha. Tia kijiko kizima cha kulia chakula kikaangoni na moto uwe mkali kiasi.

Upo best mkate wa tambi,kwa mara ya kwanza niliula Marangu aliupika dada mmoja kutoka Unguja sema alikuwa hapendi kutoa ujuzi kwa wengine,nilidesa hivyo hivyo na huwa naupika na wapare wangu wanakula tu ila mimi najua bado sijaupatia hasa ukawa kama nilioula! farkhina atupe tu maujuzi watu wakajing'ate na kutoka vitambi.
 
Last edited by a moderator:
I swear ungekuwa hujaolewa ningeleta posa kwenu asap

mapishi yoote unayoweka humu unanigusa pale pale
mkate huu ndo ugonjwa wangu..

yaani chai ya mchaichai na mkate wa kumimina na katlesi asubuhi dah...

acha kabisa

Wengine tumejizoelea viazi vitamu vya kuchemsha na karanga!
 
Mahitaji

Mchele kikombe 1
Tui la nazi kikombe 3/4- 1
Hamira 1 teaspoon
Hiliki kiasi
Ute wa yai 1
Sukari 3/4 kikombe

Namna ya kutaarisha

1)Roweka mchele usiku 1
2)Saga kwenye blenda mchele,hamira,tui la nazi,hiliki hadi viwe laini..
3)weka sehemu ya joto ili uimuke..
4)washa oven moto kiasi 300-350°..mimina sukari na ute wa yai kwenye mchanganyiko wako then changanya vizuri...
5)weka sufuria jikoni mafuta kidogo yakipata moto mimina mchanganyiko wako
6)baada ya dakika 5-10 mkate ukishaanza kushikana funika kwa ufuniko then weka kwenye oven hadi uwive na kuwa rangi ya brown
7)subiria mkate upoe ndipo uukate vipande vipande
8)mkate wa kuminina tayari kwa kuliwa..

Hongera sana, bila shaka mmeo anaenjoy mapishi yako. Vitafunwa vya kupikia nyumbani vina raha yake.
 
Back
Top Bottom