Jifunze mapishi na namna mbalimbali za kupika mkate

kwnza nakushangaa sana ujuee yaani hapa tunapika mkate wewe umeleta abari za kunanhilu acha watu tupike mkate bana!!!

btw propose leo nikupikie nn kwa ajili ya new yr eve.

nb unapikiwa kama mtu baki si kama swtlo sawa??

Haaaaa haaaa nimeipenda hii . . . . Kaizer Mchuchu ndo unaondoka huo . . . . step by step . . . hadi utaishia. Chezeya Superman weye! Hamna cha Kungwi wala Kigoli wala Mwali!
 
Last edited by a moderator:
uzuri kelele za chura hazimnyimi tembo kunywa maji atiiii.

Toka lini Mwizi akakubali kuwa ni Mwizi bila kubambwa. Tushukuru tu tego halikufanya kazi! Poa kufa na tai shingoni mi bana naondoka na Mkate sitaki.
 
Ubarikiwe sana! Na kuna ule mkate wa bakhresa una ladha nzuri na mlaini mapishi yake yanakuaje? Kuna kitu wanaongeza?
Wabheja sana.
 
Last edited by a moderator:
Ubarikiwe sana! Na kuna ule mkate wa bakhresa una ladha nzuri na mlaini mapishi yake yanakuaje? Kuna kitu wanaongeza?
Wabheja sana.

ila bakhressa anatengeneza aina tofaut za unga wa ngano kwaajili ya mapish tofauti. ukipata home baking four ni tofauti na golden baking flour na ni tofauti na ule wa maandazi, mikate na ni tofauti na wa keki. nilichogundua kwa wao hutumia aina ya unga wa ngano ule wa mkate wenyewe nafkiri kuna vitu ule unga umeongezwa ama la basi ni shayiri .sasa sina hakika sana na aina ya unga unaotumika.

lakin pish hili la mkate ukilimudu vyema basi mkate wake huwa na ladha tamu sana na ni mlain kuliko hata huo wa bakhressa.
 
Tatizo huku kwetu mikani hatuna selection ya unga, ykienda dukani sanasana utapata product za pembe. Ok na kuhusu mayai kwenye mkate mkate unaweza kukaa muda gani bila kuharibika ikiwa umeutia mayai? Maana nipika keki ya mayai ikabidi niwa4s waile yote siku yapili nilihisi kuharibikiwa..
 
Daaaah nami nimejifunza kidogo!

Asante mwl
 
Mahitaji

Mchele kikombe 1
Tui la nazi kikombe 3/4- 1
Hamira 1 teaspoon
Hiliki kiasi
Ute wa yai 1
Sukari 3/4 kikombe

Namna ya kutaarisha

1)Roweka mchele usiku 1
2)Saga kwenye blenda mchele,hamira,tui la nazi,hiliki hadi viwe laini..
3)weka sehemu ya joto ili uimuke..
4)washa oven moto kiasi 300-350°..mimina sukari na ute wa yai kwenye mchanganyiko wako then changanya vizuri...
5)weka sufuria jikoni mafuta kidogo yakipata moto mimina mchanganyiko wako
6)baada ya dakika 5-10 mkate ukishaanza kushikana funika kwa ufuniko then weka kwenye oven hadi uwive na kuwa rangi ya brown
7)subiria mkate upoe ndipo uukate vipande vipande
8)mkate wa kuminina tayari kwa kuliwa..
 
Attachments

  • 1385406258832.jpg
    23.4 KB · Views: 742
  • 1385406276350.jpg
    21.2 KB · Views: 720
ha haaa, msinicheke jamani, haya mapishi na yale ya vitumbua nimechemsha mbaya.... nitajaribu kwa kufwatilia haya maelezo yako.
kwa nini nikipikaga huu mkate au vitumbua vyangu havigandi, yaani vinachemka tuuu kama uji, lol!

Hakuna kuchekana hapa best,mi vitumbua sijawahi kujaribu kabisa ila mkate nishajaribu. Wakati naanza nilichotoa Mungu ndio anajua ila sikuchoka mpaka kikaeleweka!
 
Hakuna kuchekana hapa best,mi vitumbua sijawahi kujaribu kabisa ila mkate nishajaribu. Wakati naanza nilichotoa Mungu ndio anajua ila sikuchoka mpaka kikaeleweka!
Afadhali umenitia moyo best....
mimi nimejaribu vitumbua mara kadhaa....
mara wananiambia vile vikaangio havijazoea mata sijui nini. kwa kifupi huwa naishia kuchemsha uji kwenye mafuta.....
nikaamua kujiachia zangu
 
Mkate unavutia machoni wallahi waonekana mtam dah!
 
ha haaa, msinicheke jamani, haya mapishi na yale ya vitumbua nimechemsha mbaya.... nitajaribu kwa kufwatilia haya maelezo yako.
kwa nini nikipikaga huu mkate au vitumbua vyangu havigandi, yaani vinachemka tuuu kama uji, lol!
Usivunjike moyo shosti endelea kujaribu tu!mapishi mengine mpaka uyajaribu mara kadhaa ndo yanakubali...na ukikosea aina ya mchele tu au kuchujua huo unga haviwi!
 
Afadhali umenitia moyo best....
mimi nimejaribu vitumbua mara kadhaa....
mara wananiambia vile vikaangio havijazoea mata sijui nini. kwa kifupi huwa naishia kuchemsha uji kwenye mafuta.....
nikaamua kujiachia zangu
Wanadai kikaango ukikiunguzia machicha ya nazi kinakuwa sawa,sijui pana ukweli hapo?
farkhina naomba ya mkate wa ufuta na mkate wa tambi.
 
Last edited by a moderator:
ha haaa, msinicheke jamani, haya mapishi na yale ya vitumbua nimechemsha mbaya.... nitajaribu kwa kufwatilia haya maelezo yako.
kwa nini nikipikaga huu mkate au vitumbua vyangu havigandi, yaani vinachemka tuuu kama uji, lol!

Hahahahaha moto weka mdogo mdogo then usiweke mimaji mengi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…