Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Malalamiko kuwa vita vya kukomboa majimbo ya Ukraine sasa yako wazi kutoka kila upande.Kutoka kwa raisi wa Ukraine,makamanda wake ,askari wa kawaida na hata kutoka nchi za NATO ambazo zilichangia silaha nyingi kufanikisha hatua hiyo.
Kama alivyotabiri generali mstaafu wa Marekani bado kuna ukweli mwengine ambao umefichuliwa na askari wenyewe waliopelekwa mstari wa mbele kushirikia ukombozi huo.Wanasema kusonga mbele hata mita mia basi ni kazi kubwa.
Inajulikana kuwa katika vita kweli kunatumika mabomu ya kutegwa ardhini lakini hawakuwahi kufikiria kuwa Urusi ingetumia utitiri wa mabomu waliyokutana nayo. Hali hiyo inafanya kazi ya kutegua ili kutengeneza njia ya kupitwa na askari wa miguu iwe ngumu kupita kiasi.
Kawaida mabomu ya aina hiyo huzikwa chini mstari baada ya mstari lakini safari hii urusi imeyasia kama vile mpunga,unakutana nayo kila hatua .Vile vile kawaida yanakuwa ni aina za chuma ambayo huteguliwa na vikosi maalumu kwa kutumia metal detectori,; Lakini safari hii mabomu hayo ni ya plastic na yana sura nyingi mno kuanzia kama chupa za maji au vipande vya pipi.Wateguaji mabomu wenyewe wamekuwa wakiripukiwa na vibomu hivyo vinavyokata miguu yao.Vikundi vya uokozi navyo vinapokuja kuokoa wenzao nao yanawakuta kama ya wenzao.
Ili kutengeneza njia ya upana wa mita chache kupitika na kifaru kimoja kisogee mita chache mbele basi inaweza ikachukua siku kadhaa.
Pamoja na hivyo hiyo njia iliyosafishwa kwa shida Urusi baadae huwa wanairushia makombora ambayo yanatapakaza vibomu vyengine kuwafanya waliosonga mbele washindwe kurudi nyuma wakati huo huo wakiwalenga kwa shabaha kutoka helkopta zinazopiga kutoka mbali na mstari wa vita.
Haja ya askari kusonga mbele karibu na ngome za warusi imekuwa ya kuwahofisha sana askari wa Ukraine kwani kila wanapofanya hivyo ni kama kwamba wamejitenga na kukosa usaidizi wa wenzao.
Hofu iliyotanda sasa kwa jeshi la Ukraine ni kushindwa kutoa picha ya mafanikio ya haraka kwa NATO ili kuvutia misaada mipya ya silaha.