JIFUNZE: Tengeneza Mwili wa chini bila kuingia Gym

Asante sana mkuu, labda kwa kuongezea uelewa wako nikitumia whey protein ili mwili ukae vizuri nichanganye na steroid au mega mass?
Kwa uelewa wangu kwa mhitaji wa mwili wa level ya Jason Statham kwenye Transporter 1 whey protein pekee inatosha unachotakiwa kufanya ni mazoezi ya uhakika.


Kama unataka kuwa na mwili wa levo ya Michael Jai White changanya na mega mass.


Kama unataka kuwa na mwili levo ya Phil Heath changanya na steroids.


NB.
Hizo supplements siyo replacement ya chakula usiache kuendelea kula na kunywa maji.

Steroids zimepigwa marufuku nchi nyingi na katika baadhi ya michezo ukigundulika umetumia unaondolewa kwenye mchezo husika. Nchi zingine hupati steroids mpaka uandikiwe na daktari na sidhani kama Tz zipo (kama upo Tz).

Kwa kadri nionavyo steroids zina madhara ambayo hayaepukiki ingawa inasemwa ni mpaka ukiwa unaabuse.

Fuatilia side effects ya mega mass utakayokua unatumia na namna ya kuziepuka kama ni risk sana nashauri achana nazo.

Picha zimetoka mtandaoni.
 
mkuu hivi kutengeneza mazoezi ya chini kupitia gym kama yapi
 
mkuu hivi kutengeneza mazoezi ya chini kupitia gym kama yapi
Haya mazoezi niliyoonesha hapa, tofauti yake na ukiyafanyia gym ni kwamba ukiwa gym utakua umebeba uzito mabegani hivyo utafanya kama hapa ila ukiwa una mzigo.

Ukimaliza hayo matatu unafuatia calf raise (gym zingine nilikuta wanaita donkey raise na wanaifanya tofauti), leg press, leg extension na leg curls.

Watu wengine huendesha baiskeli kabla au baada, hayo mazoezi nimepangilia kuanzia utakachoanzia na utakachomalizia.
 
nataka chura wangu akae mkao mzuri pia aongezeke kidogo na tumbo liishe mkuu.pia mikono ipungue nifanyeje?
 
nataka chura wangu akae mkao mzuri pia aongezeke kidogo na tumbo liishe mkuu.pia mikono ipungue nifanyeje?
Kuhusu tumbo, kuna uzi niliwahi kuuanzisha bonyeza username ya Castr cheki nyuzi ambazo zimeanzishwa na Castr utakuta uzi unasema 'Unataka tumbo flat na six packs...'

Kuhusu chura, mimi ni me hivyo sijawahi kuprove kama mazoezi yanayokua promoted yanamkuza na kumtengeneza chura kama yanafanya kazi kweli, ingawa fitness gurus wanaonyesha kua mazoezi hayo yapo.

Kwenye mikono sijaelewa, kwamba ni mikubwa ukilinganisha na mwili wako? Au ina nyama zinazoning'inia?
 
ok mikono ni mimene sana
 
ok mikono ni mimene sana
Napendekeza mazoezi ya kupunguza mwili. Kwa kuyafanya utakua unaondoa fat ya tumboni na hiyo iliyo kwenye mikono, hivyo utakua unafikia malengo yako yote mawili.

Napendekeza kujog, kuruka kamba, kuendesha baiskeli, cardio na kuhakikisha diet yako inaendana na malengo yako.

Kama ni beginner anza pole pole na utaongeza ukubwa wa mazoezi unayofanya kadri utakavyozoea.
 
castr leo nimepiga push up zile pana,nimepiga 30 awamu ya kwanza nikapumzika dakika 3 nikapiga 20 baada ya hapo nikapiga kumikumi na kutimiza miamoja,baada ya dakika 5 nikachukua roller yangu a.k.a kitairi nimekwenda mara 30 yaani kila set ni kumikumi.
 
Mkuu hongera kwa mwanzo wenye nguvu kama huo, maintain hiki unachokifanya kwa muda kisha punguza muda wa kupumzika mpaka utakapoweza kufanya seti na raundi ambazo nilizionesha.

Nakugarantii mabadiliko.
 
Mkuu na kareti uko vizuri? Combat? Mm hii minyama bila ujuzi siyataki, au sheria ya ugaidi inakataza?
 
Mkuu na kareti uko vizuri? Combat? Mm hii minyama bila ujuzi siyataki, au sheria ya ugaidi inakataza?
Hapana sijawahi kufanya mafunzo ya karet, nilifanya boxing zamani.

Ila unaweza kua fit bila hata kutaka kujua ngumi au ukajua ni uchaguzi wako, na kadri ninavyojua sheria haikatazi.
 
Hii ipo vizur sana
 
Tafadhali usiniquote na kuniuliza juu ya hii mada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…