Jifunze TENSES hapa

Jifunze TENSES hapa

Tuweke jambo sawa kidogo hapa. Katika sarufi (grammar) wakati (time) si sawa na njeo (tense). Wakati (time) ndiyo hugawanyika mara tatu, yani, uliopita, uliopo na ujao lakini njeo (tense) ni lile umbo la kitenzi(verb) ambalo hujidhihirisha kwa namna mbili kuu, umbo linaloonesha wakati wa sasa na lile la wakati uliopita.Tukichambua maumbo haya kwa kila muktadha, yani , uliopo ama uliopita, tutapata maumbo tofautitofauti kadiri mzungumzaji anavyotaka kuwasiliana. Hivyo, neno TALK linaweza kuwa talked, talking ,talk(s) n.k.

Kumbuka hali ya kitenzi kuwa katika wakati uliopita ama wa sasa haina uhusiano wa moja kwa moja na wakati(TIME).Tazama mifano ifuatayo:

If I were a woman, I could bear children.(Je, unadhani huu ni wakati gani, uliopita ama wa sasa? Je, hizo tense ni wakati gani, were/could?) Tazama mfano unaofuata:

Could you give me a pen? (Unadhani huu ni wakati gani, tensi gani?, Je nikikwambia hivi maana yake ninakwambia jambo lililopita? Hapana hii ni sasa, present lakini kitenzi cha wakati uliopita.

Kwa kifupi, katika mifano yote hiyo hapo juu vitenzi vinaonesha wakati uliopita lakini lakini wakati ni wa sasa hivi.

Kwa minaajili hii, Kiingereza hakina umbo maalumu kuashiria future tense. Wengine husema hakina future tense, bali kina wakati ujao tu. Waingereza wao hutumia tense mbalimbali kueleza masuala ya wakati ujao. Tazama mifano michache hapa chini:

1. I am going to marry her next week.(going to)
2.I will go to school on Saturday.(will)
3.Exams start this weekend.(present tense)
4. I am about to finish my studies.(about to)
5. I am visiting my mum this evening.(present continuous)

Mifano hii inathibitisha kuwa hakuna umbo maalumu kudhihirisha future tense katika English. Na hii inathibitisha tense si sawa na time(wakati), kwani utaona hapo present tense imetumika kuelezea masuala ya wakati ujao na kule mwanzoni tuliona maumbo ya wakati uliopita yametumika kueleza matukio ya present time.

Mkanganyiko huu unatusumbua sana sisi ambao tunajifunza Kiingereza kama lugha ya pili. Na ukisoma kw akuchambua kama hivi, ndiyo unachanganyikiwa kabisa. Usomaji mzuri ni ule wa kupewa muktadha(context) , kisha unapewa kanuni indirectly na kuoanisha na muktadha uliopewa. Kwa mfano, unataka kujifunza wakati ujao, utapewa kisa cha Jolita anataka kuoa mwakani. Utawasikiliza kisha utaona miundo wanayotumia na wewe kuweza kuiga huku mwalimu akisiriba kwa kanuni.

Ninawasilisha

Mkuu kabla hujajikita kwenye michanganyo ya namna hiyo, kitu cha kwanza muhimu ni kujua basics za tenses.

Kwa sababu kama hujajua hizo basics hiyo mifano yako itakutoa kabisa kwenye reli.

In fact Future Tenses ni kizungumkuti kwa learners, so si mbaya tukajua zile basics.

Maana uzuri wa sentence zote hizo zinaweza kuandikwa in a simple sentences na zikabeba ujumbe ule ule na ukawa grammatically okay.
 
Mtenda au mtendewa yote sawa
My mother bought me a book (mtendewa)
My mother beat me (mtendwa)

Hapana ndugu, mtenda
Hata darasani watu kama wewe walikuwepo, ila ni ushamba fulani hivi

Mimi si mshamba kwa muktadha huu ndugu. Humu mtandaoni kuna kila binadamu. Hivyo, unaona nimecheka hivyo nikijua huyo mtu anatania. Nami nikacheka kiutani vilevile. Uzuri humu pia hakunizuii kuonyesha hisia zangu.

Kumbuka mtu aliomba msaada, hivyo anaemsaidia nilitegemea pengine awe anaefahamu. Pata picha huyo mtu anachukua kama ilivyo. Na huyo aliyemjibu hakutoa tahadhari zozote.
Hivyo, nilitafsiri kuwa anaejibu anafurahisha. Ukitazama si huyo tu, fuatilia post kadhaa hapa ni za masihara.

Sema bongolala kama wewe umekaa kichukichuki, chochote unaona umedhihakiwa. Watu wameandika utani kibao hapa, hakuna aliyeshambulia. Na ninaamini wapo wanaojua lakini wanajua mambo ya mtandao wanapotezea.

Wewe ni tundu la choo, msaada wako ni kupokea tu kinyesi.
 
Ahsante kwa kunitukana ila naomba unifafanulie kitu hapo kwenye mtenda. Kwenye hizo sentensi mbili nilizoandika yupi ni mtenda?
 
Mkuu kabla hujajikita kwenye michanganyo ya namna hiyo, kitu cha kwanza muhimu ni kujua basics za tenses.

Kwa sababu kama hujajua hizo basics hiyo mifano yako itakutoa kabisa kwenye reli.

In fact Future Tenses ni kizungumkuti kwa learners, so si mbaya tukajua zile basics.

Maana uzuri wa sentence zote hizo zinaweza kuandikwa in a simple sentences na zikabeba ujumbe ule ule na ukawa grammatically okay.

Watanzania wengi tumefundishwa kwa staili hii, kukaririshwa kanuni. Ndiyo maana unaona hata hapa mimi na baadhi tunajidai kuandika kuhusu English kwa Kiswahili.Tuambie tuandike haya kwa Kiingereza uone. Hivyo, katika ufundishaji wa lugha, staili hii ya kumpa mwanafunzi kanuni kwa staili hii haishauriwi. Kanuni ziendane na maisha halisi lugha inapozungumzwa. Ndiyo maana ukienda sehemu wanapofuata kanuni, utakuta vitabu vinamuongoza mwalimu na mwanafunzi kwa kusikiliza, kusoma, kuandika na kuongea. Sisi tunapewa tu hizi kanuni, hatupewi mazingira sahihi ya kutumia. Kibaya zaidi hatuna pa kufanyia mazoezi.
 
[emoji16][emoji16][emoji16] mwalimu kaenda kuchukua mshahara tumebaki wanafunzi tunadiskasi

Ticha aliweka tangazo ili twende twisheni, nimefanya follow-up ya link aliyoweka nikaona ni ukaribisho wa kwenda kusoma kwake.
 
Mimi hizi would, should na could huwa zinanichanganya kwa kweli. Hebu toeni mfano anuai hapo wadau. Ahsante.
 
Back
Top Bottom