Jifunze utofauti uliopo kati ya Coin vs Token kwenye Cryptocurrency

FestoKaguo

Senior Member
Joined
Apr 1, 2022
Posts
128
Reaction score
202
Habari wana JF, ni mda sasa sijapost kitu kuhusu blockchain and cryptocurrency ila leo nikapata idea nikaona nilete uzi mwingine unaoelezea kuhusu blockchain and cryptocurrency. Huenda ukawa unaijua au ushawahi isikia au unaifahamu ila bado kuna vitu vinakuchanganya unashindwa kuvielewa basi stick hapa na upitie hii thread pole pole kwa ajili ya uelewa zaidi.

Thread ya leo nitaelezea utofauti mkubwa uliopo kati ya Coin hapa naongelea Bitcoin, Ethereum, Tron, Ton au Solana na Token mfano Layerzero edge. Tukianza na Coin kwanza inatakiwa tuweze kutambua yenyewe ni kitu gani haswa kwenye ulimwengu wa cryptocurrency.

Tukisema Coin kwenye crypto ni sawa na kusema mfalme wa blockchain au kwa lugha nyingine tunaweza kusema coin ni fedha ya kidijitali inayofanya kazi kwenye blockchain yake yenyewe. Inaweza kutumika kama njia ya malipo, kuhifadhi thamani, na hata kuwa msingi wa blockchain nyingine.

Tukidadavua zaidi unaweza kutumia coin kununua bidhaa au huduma kama unavyotumia pesa za kawaida (fiat) na baadhi ya maduka na makampuni kama Tesla au Microsoft tumeona huwa yanakubali mtu kutumia bitcoin (BTC) kama malipo, Litecoin (LTC) tumeona ikiwa inatumika kwa miamala ya haraka na yenye ada ndogo.

Lakini pia coin inaweza kutumika kama store of value au kutunza thamani ya kitu kwa mda mrefu, ni sawa na jinsi tunavyoona watu wanavyotumia dhahabu. Watu wengi wanainunua bitcoin kama njia ya kuhifadhi thamani kwa sababu max supply yake ni ndogo sana inaishia milioni 21 TU!!! na inatabia ya kupanda na kushuka thamani sokoni

Na kitu cha mwisho Coin zinaweza kutumika kama mtaji wa ujenzi wa blockchain nyingine. Hii inamaanisha kuwa teknolojia iliyotumika kutengeneza coin fulani inaweza kutumiwa kuunda miradi mingine ya blockchain. Tukichukulia mfano blockchain ya Ethereum (ETH), tumeona namna ambavyo inatumika kama msingi wa tokeni na smart contracts nyingi kama USDT, UNI, LINK. Huku blockchain ya Binance Smart Chain maarufu kama Bep20 imekuwa ikitumika kwenye miradi mingi ya Decentralized Finance (DeFi) na tokeni kama PancakeSwap (CAKE).

Nafikiri imeeleweka hapo sasa upande wa coin, sasa nielezee Token kwa ufupi , Kama tulivyoona Coin tumesema ni mfalme wa blockchain basi Token yeye tunaweza kusema ni kama mpangaji kwenye nyumba ya wenyewe! Token huwa haina blockchain yake yenyewe, bali huwa inategemea blockchain nyingine ili iweze kufanya kazi. Tokeni huwa inaundwa kwa madhumuni mbalimbali, kama vile malipo, huduma, utawala, staking, na hata kutumika kwenye manunuzi ya NFTs. Kwa mfano token ya Aave (AAVE) iliundwa kwenye blockchain ya Ethereum ili iweze kutumika kwenye Decentralized Finance (DeFi) ambapo huku watu hupendelea kukopa crypto na kuzirejesha baadae pia wengine hupendelea kufanya uwekezaji (staking) pasipo kutegemea hizi centralized system kama benki. Kwahiyo tukisema token ni sawa na tu na mtu aliyenunua tiketi ya tamasha au mpira wa SImba na Yanga au ina thamani, lakini hutegemea mfumo mwingine ili iweze kufanya kazi!


Kwa mfano hapo kwenye hiyo picha hizo ni list ya coin kwenye cryptocurrency na hizo nilizozungushia rangi ya blue ni blockchain zao kwahiyo ukitaka kumtumia mtu coin ya Cardano utalazimika kutumia network ya Cardano na si vinginevyo.

Hii picha inaonesha token ya USDT ambayo imekuwa launched kwenye blockchain tofauti tofauti haina blockchain yake yenyewe inayoitwa USDT ukifananisha na Bitcoin au Ethereum.

Huu ndio mwisho wa thread yetu natumaini utakuwa umeelewa utofauti mkubwa uliopo ukisikia mtu kasema Bitcoin na Mtu akisema USDT. Kumbuka hii thread nimeiandika kwa ajili ya kuelekeza tu kile ninachokifahamu upande wa cryptocurrency and blockchain hivyo usije ukaniuliza ni Token gani au coin gani naweza kuinunua kwa kipindi hiki hiyo ni mada nyingine na hakikisha umefanya utafiti wako wa kutosha ili kuweza kupata elimu zaidi juu ya cryptocurrency unaweza kunicheki whatsapp 0765772976 kwa ajili ya discussion zaidi
 
Mkuu mm huwa trade memecoin kila siku naingiza almost $100. Nina mwezi sasa nimeanza. Huwa natumia bot inaitwa Trojan bot pamoja na BullX. Ila bado naendelea kujifunza.

Hakika cryptocurrency ukiiotea unanufaika sema wengi wetu tunaogopa.
 
Meme coin nzuri ukiiotea yenye sio Scam sema kutumia Bot sipendelei sana natumiaga sana BullX basi
 
Kwa mfano hapo kwenye hiyo picha hizo ni list ya coin kwenye cryptocurrency na hizo nilizozungushia rangi ya blue ni blockchain zao kwahiyo ukitaka kumtumia mtu coin ya Cardano utalazimika kutumia network ya Cardano na si vinginevyo.
Festo Andrews ahsante kwa bandiko zuri sana, kwa hiyo XRP network yake ni strictly XRP pekee? yaani ukitumia network nyingine umepoteza crptos zako? nauliza maana niliona kwenye Tangem wallet kuwa ukiwa na XRP unaweza tumia network kama hiyo XRP, BNB Smart Chain, Beacon Chain na BNB anyway itakuwa basi niliona vibaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…