Jihadhari: Utapeli mpya kwenye ununuaji wa ardhi

Jihadhari: Utapeli mpya kwenye ununuaji wa ardhi

Bexb

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2016
Posts
715
Reaction score
1,619
Habari ya wakati huu wakuu.

Nimewiwa kushare hili suala ambalo kwa hapo awali nilipokutana nalo nilijua hutokea kwa bahati mbaya hadi hapo wiki iliyopita nilipojua vinginevyo.

Huu ni utapeli wa kuibiwa kwa kutumia sheria yaani unaibiwa wakati wewe ukiamini kuwa umenusurika kuibiwa😂😂😂 na hufanyika zaidi katika ardhi ambayo haijapimwa japo hata kwenye maeneo yaliyopimwa hutokea japo kwa uchache.

KINACHOFANYIKA.
Kwenye ardhi ya wanafamilia/wanandoa huwa kuna utaratibu wa kufuata pale unapotaka kuuza na kuna taratibu zikikiukwa basi huweza kubatilisha mchakato mzima wa mauzo ukaonekana ni batili (null and void).

Sasa unakuta kuna kiwanja kinauzwa bei nzuri tu kutokana na eneo kilipo kumbe ni mali ya pamoja ya wanandoa (Matrimonial property) lakini hutokea mwenza mmoja ndie anauza (mara nyingi huwa baba) na katika mauzo hayo basi hupendelea kufanyia/kusimamiwa na serikali ya mtaa ambapo huwa hakuna ile 'ruhusa ya mwenza' katika mkataba.

Baada ya kuwa mmekubaliana bei, huyu muuzaji huja na hoja hii NA HAPA NDIPO UTAPELI HUJA, atakwambia na kukushawishi muandike kiasi kidogo sana cha fedha uliyolipa as if ana uchungu sana na hela zako😂 mfano, kama mmekubaliana ni 15M basi atakwambia muandike 5M ama chini zaid ili tu kusema wapunguze makato kwenye mamlaka na wewe mnunuaji unajaa.

Basi mtamaliza hayo malipo yenu kisha kila mmoja anashika njia yake na ukumbuke hapo imelipa 15M ila kwenye mkataba wako umendika 5M 😂😂😂😂.

Baadae mwenza huibuka na kuweka pingamizi na kufungua madai ya kuwa mauzo hayakua halali na hivyo mkataba huo ni batili na mkipelekana kwenye mabaraza hata hadi mahakamani basi mwenza huyo hushinda na ndio huja kile kipengele cha kuwa basi urudishiwe hela yako na hapo ukumbuke mkataba wako uliweka 5M badala ya 15m, ba si yule aliyekuuzia hurejesha hela ya kwenye mkataba kiroho safi mbele ya mamlaka husika.

Hapo ndio kwisha habari yako.
Hizi issues nimekutana nazo 4 zote zimetokea Kigamboni, so jihadhali sana na hili suala.

Imenibidi kukueleza kwa urefu ili uwe makini zaidi.
 
Unachotakiwa ni kuwalipa kupitia accoubtbya Benki
Labda haujaelewa mantiki ya mtoa hoja.

Siyo kwamba mkataba wa mauziano ukibatilishwa watakukana moja kwa moja kuwa haujawapa kitu, hapana.

Kwenye mauziano ya awali, mwenye kiwanja atakushawishi wewe mnunuzi muandike umenunua kwa kiwango cha chini ili kuepuka kutoa gharama kubwa ya mgao wa % ya fedha za manunuzi kwa mwenyekiti na kamati yake.
 
1. Ardhi ni lazima kuwe na kiapo cha Spouse Consent kama anasema Hana lazima aweke kiapo kuwa Hana Mume au Mke...Kiapo kinapatika mahakamani au Kwa Wakili.
2. Malipo yote ya Serikali yanalipwa Kwa Control Number mwenyekiti akikuambia Nataka 10% akupe control number ulipe.
3.Malipo yote yafanyike electronic Bank au Weka Hela Tigo Pesa Nk.
Tatizo hatupendi kuuliza na kupata elimu...Sikuhizi ukigoogle taratibu za kununua Ardhi utapata majibu.
Nenda ofisi ya Ardhi karibu yako uliza taratibu utapata msaada.
 
Unachotakiwa ni kuwalipa kupitia accoubtbya Benki
Kwahiyo ukiwalipa 5m kupitia akaunti ya benk badala ya 15m nini kitabadilika ikiwa kwenye mkataba umesaini 5m?

Hoja ni kuandika bei halisi kwenye mkataba haijalishi umelipa mkononi au benk!
 
Labda haujaelewa mantiki ya mtoa hoja.

Siyo kwamba mkataba wa mauziano ukibatilishwa watakukana moja kwa moja kuwa haujawapa kitu, hapana.

Kwenye mauziano ya awali, mwenye kiwanja atakushawishi wewe mnunuzi muandike umenunua kwa kiwango cha chini ili kuepuka kutoa gharama kubwa ya mgao wa % ya fedha za manunuzi kwa mwenyekiti na kamati yake.
Na kisheria Hawa wenyeviti wa mitaa hawatambuliki kwenye kusimamia mauziano ya ardhi, labda wawe Kama mashaidi tu
 
Back
Top Bottom