Jihadhari: Utapeli mpya kwenye ununuaji wa ardhi

Na kisheria Hawa wenyeviti wa mitaa hawatambuliki kwenye kusimamia mauziano ya ardhi, labda wawe Kama mashaidi tu
Sahihi kabisa, nadhani hadi watakavyopigwa vya kutosha ndipo wataelewa. Niliwahi kulisisitiza hili suala humu JF nikashangaa watu wananirushia mawe๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Na
Na kisheria Hawa wenyeviti wa mitaa hawatambuliki kwenye kusimamia mauziano ya ardhi, labda wawe Kama mashaidi tu
Usipowashirikisha watakuletea zwengwe kwenye ujenzi ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ
 
Shukrani mkuu, siku nikipata vichenji vya kununua kiwanja nitafata huu muongozo.

Kwa sasa bado nipo kwa mzee ndambile hapa, nafaidi maisha na chumba chake cha kodi elfu 25.
 
Shukrani mleta mada nimejifunza kitu kikubwa sana hapa Mungu akubariki sana kwa upendo wako. Ni upendo tu uliokusukuma ukaja hapa jamvini ukatuelimisha juu ya utapeli mpya mjini kwani ungeweza tu kukaa kimya halafu watu wakaendelea kuumizwa.
 
UZI MZURI SANA HUU, UTAWAFUNGUA MACHO WATU WENGI
 
Mkuu naomba nidokeze baadhi ya hatua za kisheria za kununua ardhi hapa nchini kwetu Tanzania kwa wakati huu?
 
Mkuu naomba nidokeze baadhi ya hatua za kisheria za kununua ardhi hapa nchini kwetu Tanzania kwa wakati huu?
Mkuu nimezidokeza zote pamoja na tahadhali za kuchukua. Soma tena huu uzi utaelewa na kama hutakua umeelewa utaniuliza
 
Mkuu nimezidokeza zote pamoja na tahadhali za kuchukua. Soma tena huu uzi utaelewa na kama hutakua umeelewa utaniuliza
Naomba muongozo sa namna ya kumjua mmiliki wa halali wa kiwanja kisicho kua na hati yani squatter na namna ya kumjua mmiliki halali wa shamba lenye hati ya wizara yani kufanya offical search bila kua na uhanja ujanja maana siku hizi mpaka wafanyakazi wa wizara wamekua wakishiriki kwenye utapeli
 
Mkuu haya mambo ni techniques tu na ndio maana hapo katika kichwa niliandika kuwa "..KUPUNGUZA UTAPELI..." kimsingi kumaliza utapeli ni ngumu kidogo lakini kwa upande wa ardhi iliyopimwa ni rahisi zaidi na kikubwa kama wewe huna uzoefu ama ufahamu wowote juu ya masuala haya tafadhali tumia mawakili wakusaidie.

Kwa upande wa squatters hii itategemeana na mazingira na historia ya eneo husika. Na ndio maana nilisema juu kule kwamba ukinunua squatter hakikisha unawapata wamiliki wa pande zote zinazopakana na eneo lako kwani hao huwa na uwezekano mkubwa wa kumfahamu mmiliki ama muhusika wa ardhi husika.

Pia hata kama umepitia kwa dalali hakikisha hela yake humpi wewe bali akachukue upande wa muuzaji yaani hata kama mlikubaliana lakini wewe unganisha hela husika kwenye mkataba wa mauziano na achukue huko kama gela yake unaona itakuuma sana endapo mkataba utabatilishwa.
 
Hayo mambo siyajui na sifahamu namna ya kuyazuia. Lakini mwiba ulipoingilia ndipp utatokea๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ