KUTOKA MAKTABA
Tufahamu kwa kina utekelezaji wa miradi ya kutatua kero ya maji katika mji mkuu wa kibiashara wa Dar es Salaam nchini Tanzania
13.01.2022
Mradi wa Maji Kigamboni utakamilika Aprili 2022, na tunategemea kuanza kazi ya ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji kwa wananchi mapema wiki ijayo" Mhandisi Cyprian Luhemeja, Afisa Mtendaji Mkuu -DAWASA
MSUMBA ON
JANUARY 15, 2022
Ujenzi wa tanki lenye ujazo wa lita milioni 15 Mradi wa DAWASA Kigamboni, Dar es Salaam Tanzania
Na Fredy Mshiu - DAWASA
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imesema, mradi wa maji Kigamboni wenye lengo la kutatua changamoto ya maji kwa wananchi utakamilika Aprili mwaka huu.
Haya yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cpyrian Luhemeja alipotembelea na kukagua mradi huo katika siku ya tatu ya ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi ya majisafi na usafi wa mazingira.
"Tulikubaliana na mkandarasi kukamilisha ujenzi wa tanki lenye ujazo wa lita milioni 15 ifikapo mwishoni mwa Januari 2022, na maendeleo yake sio mabaya na mwisho wa Januari tunategemea kukamilisha," amesema Mhandisi Luhemeja.
Mhandisi Luhemeja amempongeza mkandarasi anaetoa maji visimani kwa kukamilisha ununuzi wa pampu tatu za kusukuma maji, huku akimuagiza kuongeza kasi katika mchakato wa manunuzi ya pampu za kutoa maji visimani kupeleka kwenye tenki.
"Namuagiza mkandarasi kukamilisha manunuzi hayo mapema ifikapo mwezi wa pili mwaka huu ili kukamilisha mradi huu, endapo ifikapo mwezi wa nne mkandarasi hajamaliza mradi tutamwondoa," amesisitiza Mhandisi Luhemeja.
Katika hatua nyingine, Mhandisi Luhemeja ameeleza hatua ya pili ya mradi ni kupeleka maji Kongowe kwani ni karibu na maji yapo ya kutosha huku hatua ya tatu itahusisha kupeleka maji Mbagala ambapo yote haya yatafanyika ndani ya mwaka huu kabla ya Disemba.
Shughuli ya usambazaji wa mabomba kupitia mradi huu wa maji Kigamboni inatarajiwa kuanza Jumatatu tarehe 17 Januari mwaka huu huku Afisa Mtendaji Mkuu, Mhandisi Luhemeja akielekeza Menejimenti ya DAWASA kuhakikisha wanaendeleza mapambano kukamilisha mradi huu ndani ya muda
TOKA MAKTABA :
Matengenezo ya bomba kubwa la maji yaendelea Kawe-Tegeta
Kazi ya Kuunganisha Bomba la Maji kutoka mtambo wa uzalishaji wa Ruvu Chini ukiendelea katika eneo la Wazo Tegeta.Matengenezo ya Bomba hili ndiyo yaliyopelekea kuzimwa kwa mtambo wa uzalishaji maji wa Ruvu Chini ambapo kwa muda wa saa 48 huduma ya maji itakosekana katika jiji la Dar Es Salaam na Bagamoyo.ibAfisa Mtendaji mkuu wa DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza juu ya matengemezo hayo alipotembelea katika eneo hilo kujionea shughuli zinavyoendelea.