Jiji la Dar es salaam linatakiwa kuwa na stendi 7 au 8

Jiji la Dar es salaam linatakiwa kuwa na stendi 7 au 8

Kwa nini yasianzie stendi ya Magufuli ?
Ni utaratibu au mazoea.
Pia na wao Mabus makubwa kupunguza gharama (wafanyakaz /mafuta/tozo getini/fremu kulipia). Na muda + Foleni .(katikati ya mji kuna foleni zisizotabirika).

Kwahiyo wakaona ni vyema Stand kubwa za Mikoani zijengwe midomon ya barabara zinazoingia/kutoka Dsm kwenda Mikoani. Na Mabus yaanzie safar zao hapo.

Gari itoke garage. Iende ofisin kwake ikapakie mizigo na kukaguliwa, iende Stand magufuli, iende stand mbagala, ienze safar ya Mtwara.
Sasa Hapa tayar masaa 4 ishatumika. Na hata safar Haijaanza
 
Kwa nini hakuna magari ya kwenda Mbagala yanayoanzia Tegeta au Bunju ??
Ni utaratibu wa Logistic.
Na Serikali imeona haina haja na ndio maana hawajatoa vibali vya route za magar haya.

Hii gar inapita Wilaya 4.
Si itapiga route 3 tu kwa siku.
 
Ni utaratibu au mazoea.
Pia na wao Mabus makubwa kupunguza gharama (wafanyakaz /mafuta/tozo getini/fremu kulipia). Na muda + Foleni .(katikati ya mji kuna foleni zisizotabirika).

Kwahiyo wakaona ni vyema Stand kubwa za Mikoani zijengwe midomon ya barabara zinazoingia/kutoka Dsm kwenda Mikoani. Na Mabus yaanzie safar zao hapo.

Gari itoke garage. Iende ofisin kwake ikapakie mizigo na kukaguliwa, iende Stand magufuli, iende stand mbagala, ienze safar ya Mtwara.
Sasa Hapa tayar masaa 4 ishatumika. Na hata safar Haijaanza
Gari za kwenda Mtwara na Lindi zinazotaka kuanzia safari zao na kumalizia safari zao stendi ya Magufuli zinaruhusiwa kufanya hivyo ?
 
Ni utaratibu wa Logistic.
Na Serikali imeona haina haja na ndio maana hawajatoa vibali vya route za magar haya.

Hii gar inapita Wilaya 4.
Si itapiga route 3 tu kwa siku.
Serikali huwa inatumia vigezo gani kuona kuna haja ya kuwepo route mbalimbali mfano ya Tegeta -Mbagala ?

Kama gari imeamua kwa hiyari yenyewe kupita wilaya 4 na kupiga route 3, 2 au hata 1 tu kwa siku kuna shida gani? Tatizo litakuwa nini ?
 
Gari za kwenda Mtwara na Lindi zinazotaka kuanzia safari zao na kumalizia safari zao stendi ya Magufuli zinaruhusiwa kufanya hivyo ?
Gari yako Ikiingia Stand kubwa lazima ilipie Tozo getini, iwe na ofisi, iwe na wafanyakazi , italipia pango.
Itapoteza muda na mafuta zaid.

Kwahiyo bora watu wayafute huko yaliko.

Uzur Dsm kuanzia saa 9 usiku usafiri wa Umma uko. Kwahiyo gar za saa 12 asubuh. Hata kama unatoka tegeta. Unaliwah Mbagala
 
Gari yako Ikiingia Stand kubwa lazima ilipie Tozo getini, iwe na ofisi, iwe na wafanyakazi , italipia pango.
Itapoteza muda na mafuta zaid.

Kwahiyo bora watu wayafute huko yaliko.
Kama kampuni ya gari inayoenda Mtwara na Lindi iko tayari kulipa hizo gharama zote stendi kubwa ya Magufuli inaruhusiwa kuanzia na kumalizia safari zake katika hiyo stendi??
 
Sasa za ubungo na kinondoni si zitasababisha foleni katikati ya mji. Stendi ziwekwe kwenye barabara zinazotoka nje ya jiji kama mbagara, bunju na mbezi
Basi linalobeba abiria 50 linasababishaje foleni halafu dalaladala mbili na Bajaji zitakazowabeba hao abiria kuwatoa au kuwapelekea huko stendi ziwe hazisababishi foleni??
 
14 August 2026
Chama cha wamiliki wa mabasi nchini (TABOA) watoa kauli juu ya tamko la RC Albert Chalamila

View: https://m.youtube.com/watch?v=OLxS6QmHoVs

#HABARI: Sakata la agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuagiza mabasi yote yasiyokuwa na vibali vya kupakia na kushusha abiria nje ya Kituo Kikuu cha mabasi Magufuli jijini Dar es Salaam Chama cha wamiliki wa mabasi nchini (TABOA) kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa sakata hilo kimetoa tamko na kusema hawakushirikishwa katika mchakato huo na hivyo wanaomba kukutana na mkuu wa mkoa kabla ya jambo lolote kufanyika.Akizungumza na ITV Katibu Mkuu wa chama hicho Bw. Priscus Joseph amesema agizo hilo linahitaji kwanza kufanyika kwa mkutano wa pamoja ili haki itendeke
 
Basi linalobeba abiria 50 linasababishaje foleni halafu dalaladala mbili na Bajaji zitakazowabeba hao abiria kuwatoa au kuwapelekea huko stendi ziwe hazisababishi foleni??
Daladala haziepukiki maana zinatumika mpaka na abiria kwenye mizunguko yao ya mjini. Kuhusu bajaji uangaliwe utaratibu wa kuzipanga. Lakini mabasi ya mkoani haya yanaweza kuwekwa pemembezoni ya mji kwenye bafabara zinazotoka jijini kwenda mikoani bila kuathiri shughuli zingine mjini
 
Dalaladala zinaweza kuepukika, watu wanaweza kupanda taxi, Bajaji, Bodaboda au wakatemea kwa miguu.
 
Na wengine pia vipato vyao havitoshelezi kutoka Kimbiji mpaka Magufuli Stendi.
Hakuna solution inaweza kunufaisha watu wote. Kuna wachache lazima watolewe kafara. Watakaoguswa na athari za ukosefu wa daladala hauwezi kufananisha na wataoguswa na athari mabasi ya mikoani kupelekwa barabara zinazotoka nje ya mji.
 
Tuwatoe kafara wenye magari binafsi tuwazuie kuingia nayo mjini, wawe wanatumia daladala na Bajaji tu kuingia mjini. Mabasi yaruhusiwe mpaka mwisho wa Dar es Salaam, Kigamboni.

Tuwatoe kafara pia wamiliki Malori na yard za mjini.
 
Mbona viwanja vya ndege hatutaki vijengwe kila mahali kuwarahisishia abiria lakini stendi tunataka kila mahali?
 
Back
Top Bottom