Jiji la Dar es Salaam ni uchochoro wa silaha zilizozagaa Nchini

Jiji la Dar es Salaam ni uchochoro wa silaha zilizozagaa Nchini

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Dodoma. Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, George Simbachawene amesema Jiji la Dar es Salaam ni uchochoro wa silaha zilizozagaa nchini.

Amesema kuna kata moja katika Jiji hilo la kibiashara ndio inaongoza kwa vibali vya kuruhusu watu kumiliki silaha na jambo linalomshangaza ni wahusika kutofuatilia sababu ni zipi. Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Juni 18, 2021 mkoani Dodoma wakati akizindua bodi mpya ya tatu ya shirika la uzalishaji mali la Jeshi la Polisi na kuagiza kuisimamia sekretarieti ya polisi kwa madai kuwa utendaji kazi wao haumfurahishi.

Licha ya kutoitaja kata hiyo, amesema imebainika silaha nyingi zilizozagaa nchini vibali vyake vimetolewa kwenye kata hiyo na kusainiwa na mtendaji mmoja lakini mamlaka hazijaeleza kwa nini iwe hivyo.

"Silaha hizo hazipo Dar es Salaam pekee, Morogoro, Dodoma, Kilimanjaro na maeneo mengine wanazo silaha walizopata huko hii ni hatari sana," amesema Simbachawene.

Amebainisha kuwa hakuna utaratibu mzuri katika udhibiti na utunzaji wa silaha nchini na kumwagiza mkuu wa upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kufanya uchunguzi wa jambo hilo. Akijitolea mfano amesema anamiliki silaha mbili lakini hajawahi kuulizwa kwa njia yoyote kama amelipia au zinafanya kazi gani.

Chanzo: Mwananchi
 
Haya mambo mengine, kiongozi anatakiwa ayafanyie kazi na watendaji, halafu akipata ufumbuzi fulani, aje na taarifa kafanya nini kuboresha hali.

Waziri akipiga kelele nchi imejaa silaha, kauli hiyo inaweza kujenga hofu mbaya inayoweza kuwa hatari kuliko silaha zenyewe.

Habari hiyo inaweza kutumiwa vibaya na maadui zetu kukuza taswira mbaya ya nchi, wakasema "Tanzania si nchi salama, hata Waziri wao kakubali imejaa silaha".

Hawa mawaziri wanahitaji kozi elekezi mpaka leo au vipi?
 
Haya mambo mengine, kiongozi anatakiwa ayafanyie kazi na watendaji, halafu akipata ufumbuzi fulani, aje na taarifa kafanya nini kuboresha hali.

Waziri akipiga kelele nchi imejaa silaha, kauli hiyo inaweza kujenga hofu mbaya inayoweza kuwa hatari kuliko silaha zenyewe.

Habari hiyo inaweza kutumiwa vibaya na maadui zetu kukuza taswira mbaya ya nchi, wakasema "Tanzania si nchi salama, hata Waziri wao kakubali imejaa silaha".

Hawa mawaziri wanahitaji kozi elekezi mpaka leo au vipi?
Una akili nyingi sana we jamaa, maajabu kauli kama hizi zinatolewa na Waziri mkongwe na mwandamizi tena anaesimamia Wizara nyeti, yaani anaona hapo katibu tatizo kweli yaani kulalamika, Yaani mtu aliyepewa dhamana ya kusimamia Usalama wetu na mali zetu ndio anabwabwaja namna hii sasa ipo siku atatangaza zilipo Hamala za kutunzia silaha za Jeshi la Polisi
 
Hata kama zimetolewa kisheria?
"Wizara ya mambo ya ndani'' halafu mambo yake yanatamkwa nje nje tu!. Kama waziri unaona huwezi kuhimiri kuongea na watendaji wako kiundani (siri) better you step down. Ndyo, wakati mwingine ninyi mawaziri mnatudestract from the issues na hivyo tunapaswa kuwataka kuwajibika. Kwani kama unamiliki silaha mbili unataka sisi wananchi tufanye nini?. Tuje kukunyang'anya au unatakaje sasa?. Haujui anaepaswa kukagua hizo silaha zako hadi uje kulalamika kwetu?. Kwani utoaji wa kibali cha kumiliki silaha ukoje au haujui kwa hiyo unataka sisi RAIA tukusaidie au vp?. Unataka kuwa yule Mzee wa kubeba ilani au unatakaje?.
 
Ni kweli kabisa... Nadhani system haipo sawa, au haipo kabisa...
 
IGP amesema wiki chache zilizopita kwamba anataka kuona watu wananunua silaha kujilinda

Unazisema vibaya silaha,wewe unaweza kupigana Kung Fu ukishambuliwa na vibaka?
 
Mbona yeye Amamiliki silaha 2?
Kama zinamilikiwa kisheria kosa ni nini
Kama hazileti uhatarishi wa raia ubaya ni nini?

AIJIPII alishangazwa watu hawana silaha , hata panga wanamiliki Masofo ,ameshangaa wanajilindaje?
 
Back
Top Bottom