Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Dodoma. Waziri wa Mambo ya Ndani nchini Tanzania, George Simbachawene amesema Jiji la Dar es Salaam ni uchochoro wa silaha zilizozagaa nchini.
Amesema kuna kata moja katika Jiji hilo la kibiashara ndio inaongoza kwa vibali vya kuruhusu watu kumiliki silaha na jambo linalomshangaza ni wahusika kutofuatilia sababu ni zipi. Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Juni 18, 2021 mkoani Dodoma wakati akizindua bodi mpya ya tatu ya shirika la uzalishaji mali la Jeshi la Polisi na kuagiza kuisimamia sekretarieti ya polisi kwa madai kuwa utendaji kazi wao haumfurahishi.
Licha ya kutoitaja kata hiyo, amesema imebainika silaha nyingi zilizozagaa nchini vibali vyake vimetolewa kwenye kata hiyo na kusainiwa na mtendaji mmoja lakini mamlaka hazijaeleza kwa nini iwe hivyo.
"Silaha hizo hazipo Dar es Salaam pekee, Morogoro, Dodoma, Kilimanjaro na maeneo mengine wanazo silaha walizopata huko hii ni hatari sana," amesema Simbachawene.
Amebainisha kuwa hakuna utaratibu mzuri katika udhibiti na utunzaji wa silaha nchini na kumwagiza mkuu wa upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kufanya uchunguzi wa jambo hilo. Akijitolea mfano amesema anamiliki silaha mbili lakini hajawahi kuulizwa kwa njia yoyote kama amelipia au zinafanya kazi gani.
Chanzo: Mwananchi