Jiji la Dodoma kuwaomba wafanyabiashara kuchangia pesa kwa ajili ya anuani za makazi (postcode) haijakaa sawa

Jiji la Dodoma kuwaomba wafanyabiashara kuchangia pesa kwa ajili ya anuani za makazi (postcode) haijakaa sawa

Raisi Samia Samia amewahi kutueleza pale tunapoona Serikali imekosea basi tuikosoe kwa staha na tushauri nini kifanyike.

Hivyo kwa staha naomba kuishauri Serikali juu ya hili ombi kwa wafanyabiashara kuchangia pesa kwa ajili ya anuani za makazi(postcode).

Sasa hivi Hali iliyopo inaonekana wazi tu kuwa mambo hayajakaa sawa kutokana na huu mfumuko wa Bei unaoendelea na hata wafanyabiashara wameathirika sana na hili na juzi hapa mh.raisi alisema gharama yuingiza kontena imepanda kutoka dola 1500 hadi dola 8000.

Hivyo kwa mfanyabiashara ambae mwanzo ilibidi atumie bil 1 kuingiza makontena yake kadhaa, Sasa hivi itahitaji atumie bil 8 kuingiza makontena hayo kadhaa. Hivyo nae kwa sasa atahitaji pesa nyingi kuagiza mzigo mkubwa kutokana na kupanda sana bei

Lakini pia hili zoezi bajeti yake ilishatengwa, Ila Kama haitoshi basi niwaombe serikali mnaweza kulisogeza mbele.

Nchi imewashinda hawa wachovu🤣🤣🤣
 
Serikali ijikite kwenye kuzifanya anuani zipatikane kielektroniki...

Hivyo vibao viwekwe wakati wa kuporesha njia/barabara za mitaa...
 
Kwanini mchango uwe kwenye nguzo na mabawa yake? Na si vibao pekee.

Moja kwa moja kuna harufu yaupigaji hapo maana wameona kwenye vibao hakuna pesa na nguzo ndio kuna pesa ndio maana wamesisitizia hapo.

Wafanyabiashara wa dodoma naomba muungane kupinga wizi huu.

Kwa maoni yangu barua hiyo ingewahusu makurugenzi wote, mawaziri na manaibu waziri, wabunge, wakuu wa mikoa na wilaya, ma RAS na DAS bila kusahau viongozi wote wa chama cha mapinduzi mbona pesa ingepatikana mapema tu kuliko kulazimisha kuwa omba omba kwa wafanyabiashara.

Hii serikali kuna vitu inafanya pasipo kufikiri, ina maana walivyokuja na mpango huu hawakuandaa bajeti yake??
 
-Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma,Kama itampendeza aombe wajumbe wa mashina na watu waliojigawia mitaa au barabara wachangie gharama,
-wakishindwa majina ya mitaa wapewe watu wenye uwezo wa kuchangia.
-Sehemu nyingi majina ya mitaa yalitolewa na wenyeviti wa Serikali za mitaa,bila kufanya mikutano na wananchi kupata maoni au mapendekezo yao (ushirikishaji wa wananchi).
-Gharama zimekuwa kubwa kwa sababu Kuna mitaa mingine ina nyumba 10, -Serikali ingeweka vigezo,kwa mfano mtaa mmoja uwe na nyumba 100 au 150 mitaa ingepungua.
 
Back
Top Bottom