Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nina hasira na viongozi kwasababu mji ni mchafu.Mbona Kama vile una hasira na Mtu mmoja hivi
Unatoa mbao huko unakuja kuzitua barabarani. Utakua una akili wewe?shindwa na ulegee kwa kuja kuziba rizki za watu hizo mbao ziende wapi sasa?
We ndio uitakii mema Dodoma. Tunakosoa viongozi wajirekebishe we unatoa porojo zako. Kwahiyo kama huko Kariakoo ni kubaya na Dodoma kuwe hivyo? Hata hivyo huko unapoongelea kuna afadhali kuliko mlipo jaza mambao yenu kutuharibia mji tu hapa. Mtsyuuuu.huu ni mwendelezo wa kuikataa dom bila mashiko hivi kati ya maeneo ya msikiti wa gadaff na pale kariakoo kuanzia china plaza yote hadi msimbazi wapi pachafu? wapi pana msongamano kiasi unajikuta ukiwa umesimama unahs upo unasubri gari ipite uvuke kumbe ushakalia ofis ya mtu na wateja wanataka huduma.
Hii ndio africa tena Tanzania ukileta uzungu kila kitu utakiona kichungu.😂😂😂Jiji la Dodoma ni lichafu. Barabara zimejaa udongo na matope utafikiri hazijawekwa lami. Tope kama tuko shambani jamani. Mvua imenyesha kidogo maji yamekwama kwenye barabara hamna proper drainage system. Pembezoni mwa barabara hapajasakafiwa vizuri au kuoteshwa majani ili kuzitunza barabara hizi.Kingo zake zinameguka kila kukicha.
Taka hazijazolewa muda mrefu. Niliona zikizolewa mara moja tu kwa kutumia yale magari ambayo yako wazi(Suma jkt) yakipita mji mzima unanuka.
Sokoni ndio usiseme. Masoko yote Dodoma ni mabaya. Watu wapo ofisini hawawajibiki. Wanasubiri nini?
Maeneo ya Uwanja wa Jamhuri kumejazwa mbao kila mahali ule msikiti wa Gaddafi umezibwa hauonekani. Mbao zinafanyanini barabarani? Hivi nyie viongozi mnaakili kweli? Mji mchafu
sana.Maafisa mazingira kazi yenu imewashinda.
Ccm wana mirunda ina bendera zao jiji zima utafikiri kichaa ndio amesimika. Kiufupi ni uchafu. Mnashindwa kuweka kitu chenye mvuto?
Mkurugenzi, jiji limekushinda. Wewe na mkuu wa mkoa kazi yenu kuropoka tu hamna mikakati. Jiji gani hili?
Barabara zipi? Hizi ninazozijua mimi? Huhuhu.Huku wanasema hivi
Manispaa ya Jiji la Dodoma hongereni kwa upandaji wa miti Kando ya barabara lakini nawaomba muanzishe hata misitu minne kwa utunzaji wa mazingira
Nawapongeza Sana viongozi wote waliobuni zoezi la upandaji miti pempezoni mwa barabara mmfanya jambo zuri katika kutunza mazingira. Ni mwanzo mzuri lakini hii hatua haitoshi kama kweli mnania nzuri ya uhifadhi wa mazingira. Ombi langu anzisheni misitu hata minne kulizungukua Jiji la Dodoma...www.jamiiforums.com
Kwanza namshangaa raisi. Alivyokuja juzi alipita wapi? Au ndio analewa sifa?Wako busy kusifia na kuabudu aliyewateua hadi wanakosa muda wa kutazama mazingira yao.
Kwanza utakuta hao watendaji husika hawaishi Dodoma makazi yao ni Dar weekend wanakimbizana kwa misafara kwenda Dar kuwahi papa za kidimbwi.
Tuanze kutoa tuzo za mji mchafu kushinda yote Tz.
Dodoma ilianza vizuri. Lakini siku za hivi karibuni mambo yanazidi kuwa mabaya.Dodoma ingetakiwa iwe safi na kpangiliwa vizuri sana kulinganisha na Dar ambapo palikosewa mifano ka majiji mengine yaliyohsmishwa kama Abuja, Yamasoukro, Pretoria
Hamna lolote la uzungu wala uafrika. Ni uzembe tu.Hii ndio africa tena Tanzania ukileta uzungu kila kitu utakiona kichungu.😂😂😂
Hovyo sana sisi.
Jiji ni title tu haina bearing kivile. Lakini cha msingi waache kuzembea Dodoma sio ya kuwa hivi leo hii. Huko nyuma walijitahidi lakini sasa ni majanga.Hata kama mtapingana na mtoa mada/mimi! Bado ukweli unabaki pale pale; Dodoma haina hadhi ya kuitwa Jiji kutokana na kukabiliwa na Changamoto nyingi!
Ila sikatai; iwapo Serikali itaendelea kuimarisha miundombinu mbalimbali, kwa baadaye Mji utabadilika. Ila kwa sasa hapana aisee.
Usitake kujifariji kwamba kwakuwa Dar ni chafu zaidi (si kweli kwa hali ilivyo sasa)basi Dodoma haina shida. Sipo hapa kushindana. Dodoma haikuwahi kuwa chafu hivi na mambo yanazidi kuwa mabaya.Hatupingani nae mkuu.. tatizo ni kweli lipo lkn sio kwa ukubwa wa namna hiyo.. hebu nitajie miji ambayo haina changamoto ya uchafu tz hii.. then niambie kuna mji unaongoza kwa uchafu na harufu mbaya kuzidi Dsm?? Kama kigezo ni hicho unachosema wewe basi na dsm hastahili kabisa kuwa Jiji..
unaijua historia ya biashara ya mbao pale na uwepo wa msikiti mahali pake au unaropoka? km umekuja jana 😷mdomo wako kuna watu watakucheka,,Unatoa mbao huko unakuja kuzitua barabarani. Utakua una akili wewe?
WEWE ndio huitakii mema Dodoma. Unataka Dodoma iendelee kuwa chafu kwasababu ya harufu ya ferry? Kwahiyo harufu ya ferry inauhusiano gani Dodoma? Hivi huwa mnatumia akili kweli?😄😄😄 yaani dar wanaibeba sana ila ukweli wanaujua maeneo ya aghakani kule ferry unahisi kutapika tu harufu na shomboshombo sijui hawalioni hilo.
wanapinga dom kwa chuki si kingine
Na uzembe ndio huo ututambulisha Uafrica wetu. Hakunaga jambo tunafanyaga likanyooka.Hamna lolote la uzungu wala uafrika. Ni uzembe tu.
waache watu watafte mkate wa sikuWe ndio uitakii mema Dodoma. Tunakosoa viongozi wajirekebishe we unatoa porojo zako. Kwahiyo kama huko Kariakoo ni kubaya na Dodoma kuwe hivyo? Hata hivyo huko unapoongelea kuna afadhali kuliko mlipo jaza mambao yenu kutuharibia mji tu hapa. Mtsyuuuu.
unadandia tren kwa mbele huelewi nilichomquotes bosi hebu tulia basi.WEWE ndio huitakii mema Dodoma. Unataka Dodoma iendelee kuwa chafu kwasababu ya harufu ya ferry? Kwahiyo harufu ya ferry inauhusiano gani Dodoma? Hivi huwa mnatumia akili kweli?
Huhuhu kumbe we ni mtu wa mbao? Nimegusa penyewe. Acha kudanganya, historia gani? Unajifanya unaijua Dodoma kuliko mimi? Tetete! Ungekuwa unaijua ungetetea uozo hapa? Pale sio mahala pa mbao.unaijua historia ya biashara ya mbao pale na uwepo wa msikiti mahali pake au unaropoka? km umekuja jana 😷mdomo wako kuna watu watakucheka,,
hiyo biashara iko mda sanaaaa tena ni wastaarabu kuliko biashara za aina nyingine hutaki kakae mlimani kwa waziri mkuu kule.
tena usirudie kuingilia biashara za watu wengine zimetulea heshimu kbs .
Unapajua kwetu? Unajua tofauti ya vumbi la Dodoma ambalo lipo siku zote na udongo uliojaa barabarani utafikiri hamna lami?Unateseka ukiwa wapi??
Ok unaweza kutupa mbinu ya kulitenganisha vumbi na ardhi ya dodoma? Ile ni asilia ya eneo hilo, mengine ni kuwa mchawi tu.
Toka huko rudi kwenu.
Naelewa vizuri ulichomquote. Labda kama wewe hujui namna ya kuandika vizuri ureflect mawazo yako.unadandia tren kwa mbele huelewi nilichomquotes bosi hebu tulia basi.
km vipi kasimame pale makutano gadaff alafu shika mice utangaze hili tangazo lako