Jiji la Dodoma ni chafu!

Jiji la Dodoma ni chafu!

Dodoma ilianza vizuri kwa mpangilio na ilikopi mji wa Lilongwe Malawi ambako enzi hizo CDA walikuwa wakienda kuangalia mpangilio wa maeneo na ujenzi wa nyumba, kwenye ujenzi vifaa vya ujenzi vilikuwa havitozwi ushuru hivyo vilikuwa vikitoka ulaya vinapelekwa Dodoma bila ushuru na bei ilikuwa ya chini sana, lakini viongozi wa CDA wakaanza kuviiba na kuvipeleka Dar kuviuza kwa bei kubwa, serkali ilipowakamata ikaondoa mpango huo na kuivunja CDA. Ilipoivunja CDA ramani yote ya mpangilio ikasambaratishwa watu wakaanza kupimiwa viwanja ndani ya maeneo yaliyojengwa mfano kituo cha mafuta Shabibby na Area C na D ndiyo ukawa mwisho wa ustaarabu na bustani ya CDA kwa ajiri ya kupanda miti na maua ya kulipendezesha jiji ikafa.
Very very sad to hear this.

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Kwani Ndugai anasemaje??
"Nimekosa mimi"
"Nisamehe mimi"
"Nimekosea sana"
Mama"tokaaa🤥
 
Dom enzi hizo Shilam discotec NK town pale ilikua balaa,Area C,D kwa washua sikuwai kuona uchafu.
Nzuguni nimeenda kuchimba dhahabu huko nna miaka 16.
Chamwino Ikulu nilifika pale kuandaa mazingira na msafara wa BM unakuja nyuki wakatuvamia tukapigwa sindano haswa.
Lile jumba lilikua gofu tu porini huko
Jiwe alikaa magu akapiga foto nalikumbuka.
Nilikua nashinda pale naota jua week 2-3
Dodoma ni mji mkuu wa Tanzania alisema Dr Remmy.
KaudO,CDA nyumbani mkuu wa mkoa alikua David herella sijui
Kama ni uchafu wakuja wameleta palikua safi sana.
 
Dar es salaam ndio jiji kongwe na kubwa katika eneo hili, Dodoma ndio inajengwa tena kwa masterplan iliyobuniwa miaka ya sabini, kwanza na sasa baada ya msukumo wa awamu ya tano tunategemea kuona usasa zaidi!, lakini bado Dodoma inapwaya. Angalau basi tungeona mabanda yaliyojaa pale njia nne yakiondolewa kupisha kitu kinachofanana na mji wa kisasa.... Hola!!. Uchafu kwa Dodoma haupaswi kuwa jambo la kujifunza kutoka Dar es salaam au kwingine kokote kuliko na vijiji vikubwa... Dodoma inatakiwa kuwa ya mfano katika nyanja zote zinazotafsiri hadhi ya kuitwa jiji.
Kweli kabisa. Sijui wenye mamlaka wanashida gani.
 
Muogope Mungu ndugu yaani ufananishe China Plaza na zile mbao zilizojazana nje ya msikiti wa Gadafi kweli? Kwa idadi ya watu sikatai kkoo watu nyomiii ila haikeri km pale mpangilio mbovu sana tena sana
Ndugu huyo muuza mbao anajitahidi kwa hali yeyote vile kutetea uozo wake. Mwenyewe nimemshangaa sana. Kariakoo inavurugu lakini bado utaona mpangilio na miundombinu mizuri.
 
Tembelea ihumwa kuna madimbwi kama ya kufugia kambale Dodoma kuitwa jiji ni matumizi mabaya ya kiswahili upepo ukianza kuvuma bora kuishi Argesa Somalia!
Hahaha jiji ni title tu. Majiji pia huwa ni machafu.
 
unaijua historia ya biashara ya mbao pale na uwepo wa msikiti mahali pake au unaropoka? km umekuja jana 😷mdomo wako kuna watu watakucheka,,


hiyo biashara iko mda sanaaaa tena ni wastaarabu kuliko biashara za aina nyingine hutaki kakae mlimani kwa waziri mkuu kule.


tena usirudie kuingilia biashara za watu wengine zimetulea heshimu kbs .
Tena hiyo biashara yangu ya mbao mahali hapo naifanya kistaharabu,watuache na biashara yetu ya mbao tupatr rizik.
 
Back
Top Bottom