Dodoma ilianza vizuri kwa mpangilio na ilikopi mji wa Lilongwe Malawi ambako enzi hizo CDA walikuwa wakienda kuangalia mpangilio wa maeneo na ujenzi wa nyumba, kwenye ujenzi vifaa vya ujenzi vilikuwa havitozwi ushuru hivyo vilikuwa vikitoka ulaya vinapelekwa Dodoma bila ushuru na bei ilikuwa ya chini sana, lakini viongozi wa CDA wakaanza kuviiba na kuvipeleka Dar kuviuza kwa bei kubwa, serkali ilipowakamata ikaondoa mpango huo na kuivunja CDA. Ilipoivunja CDA ramani yote ya mpangilio ikasambaratishwa watu wakaanza kupimiwa viwanja ndani ya maeneo yaliyojengwa mfano kituo cha mafuta Shabibby na Area C na D ndiyo ukawa mwisho wa ustaarabu na bustani ya CDA kwa ajiri ya kupanda miti na maua ya kulipendezesha jiji ikafa.