Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 242
- 1,141
Kampuni ya ZESCO Limited inatarajiwa kuanzisha ratiba mpya ya kukata umeme kwa maeneo ya makazi huko Lusaka licha ya uwepo wa wasiwasi kutoka kwa wadau kuhusu mpango huo wa kukata umeme wa masaa 8 kila siku.
Msemaji wa kampuni hiyo, Matongo Maumbi, anasema mpango wa kukata umeme, ulioanza tarehe 11 Machi 2024, ni hatua muhimu ya kushughulikia upungufu wa umeme wa taifa uliosababishwa na uwezo mdogo wa uzalishaji.
Matongo ameongeza kuwa kukatika kwa umeme kwa nyumba za makazi kwa awamu inalenga kupunguza usumbufu huku ikidumisha utulivu wa gridi na kwamba ratiba mpya inatarajiwa kuanza kutumika tarehe 1 Aprili 2024.
Amebainisha pia kuwa kila eneo litapata kukatika umeme mara mbili kwa masaa manne kila awamu moja, ambayo itafanyika wakati wa mchana.