Uchaguzi 2020 Jiji la Mbeya, Hata kama mnampenda Mbilinyi (Sugu) msimchague. Ili mpate maendeleo chagueni CCM

Wenye mawazo kama yako wapo hivi;
 
Kama ulichoandika hapa, ndicho Rais anafanya, kwamba anasusia maeneo flani ya nchi, kisa ni wafuasi wa chama cha upinzani, basi huyo Rais ni MPUMBAVU. Ila kama umeandika hapa, kwa ujinga wako mwenyewe, unafaa kukamatwa na kuwekwa ndani kwa masaa yasiyopungua 8760.
 

Kadanganye mafala, maendeleo sio hisani ya rais, sana sana hapa umeishia kuonyesha udhaifu wa rais kuwa hajui jukumu la urais ni nini, kwamba anaona maendeleo anaweza kuyapeleka kwa hisani sehemu anazoabudiwa. Zaidi 75% ya nchi hizi ni masikini, je kote huko rais haabudiwi ila Mbeya tu ndio kunamkwaza rais? Kama umekula hela ya Tulia Akson kuwa unaweza kumpigia debe huku mitandaoni, basi rudisha hela ya bibi wa watu maana hapa ni kama unachoma mahindi kwa tochi.
 
Mbeya ni kama maji, usipoyanywa utayaoga, usipoyaoga utayafulia na usipoyafulia utayajengea. Mbeya imejaaliwa radhi yenye rutuba, iko kwenye location ya mpaka na nchi zingine, ina wasomi na watu wenye msimamo.

Hata ukikimbiza hayo unayoyaita maendeleo wananchi wa Mbeya hawawezi kuwa omba omba kama wa Singida, Shinyanga na Dodoma. Unaanzaje kutojenga barabara ya kwenda mkoa unaolisha nchi kwa mchele, mahindi, vizazi, mdizi na maharage?

Kuisusia Mbeya ni kuwasusia Watanzania. Ila kumbuka ni raha kuwa mwana Mbeya kwa vile wanajitambua, siyo mapompooma.
 
Mbona dodoma kuna hali mbaya hadi njaa ikidondoka wanakula mafunza? Kule handeni kila wakati wa njaa wanavamia maembe mabichi na kote huko ccm ndo imetamalaki au huko nako wanaamini ccm ndo itawapelekea maendeleo? Majimbo mengi ya ccm ndiyo yenye umasikini wa kutisha unaitwa kwa kisukuma 'mkunula' kwanza mleta mada hujafikia level ya kuongea chochote mbele ya watu wa mbeya city
 

Simple thing ni kwamba, wambie chama chako wafute mfumo wa vyama vingi, mbona ni ishu ndogo sana?
 
Akili zako naona bado hujaenda kuzichukua ulipo ziacha pale lumumba kwa chakubanga
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Majitu mfano wa mleta mada yanapaswa kupuuzwa tu ,hivyo kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaeleweka wazi kuwa mbunge pekee HALETI maendeleo, ila anashirikiana na wananchi kuhamasisha maendeleo kwa kuikumbusha serikali na kufuatilia nini kilipaswe kifanywe, ndio kusema mbunge anawasemea wananchi.

Swali langu ni Mh. Sugu amehamasisha mangapi na amesaidia mangapi kufanyika. Kwa ajili ya maendeleo ya wana Mbeya? Vipi hali ikoje tangu alipoanza na hadi sasa? Majibu ya maswali haya ndiyo picha halisi kua anafaa au imetosha awaachie wengine!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…