Mfano ukiwa unatokea Tarime ukishaona tu kibao pale Bunda cha kwaheri mkoa wa Mara sasa unaingia Simiyu to Mwanza jua ndiyo mwisho wa lami standard sasa ni mwendo wa mitikisiko, mashimo, madaraja ya chuma ya kizamani, marekebisho ya barabara ya yanayofanyika main road zaidi ya miaka mitatu kila siku magari yanapitishwa pembeni ya barabara kwenye madimbwi n.k
kiufupi Mwanza imesahulika mno hapa Tanzania kwenye suala la barabara mpaka wakenya wanapata kiburi cha kulinganisha Kisumu na Mwanza.
Na siyo hivyo tu ni kweli kuwa nyuma ya Kampala ni Mwanza ndilo jiji linalofuatia kwa ukubwa kwa majiji yote yanayopakana na ziwa Victoria lakini ukiilinganisha Mwanza kimiundombinu na Kigali, Kampala, Entebbe, Kisumu ni wazi Mwanza ndiyo inavuta mkia kwenye list.