A
Anonymous
Guest
Halmashauri ya Jiji la Mwanza kushindwa kubadlisha jina la mmiliki wa kiwanja kwenye mfumo, Nilinunua nyumba Mwaka 2024 na kukamilisha taratibu zote za kuhamisha milki Julai, 2024.
Japokuwa kwenye hati linasomeka jina langu, Halmashauri ya Jiji la Mwanza wameshindwa kurekebisha taarifa zangu za umiliki kwenye mfumo wa kielekroniki.
Mwaka 2025 nilifuatilia wakaniambia nipeleke nyaraka husika nikawapa lakini cha kushangaza mwaka huu pia nimeenda kuomba kulipia kodi ya Ardhi lakini waliponiprintia bill bado inasoma jina la aliyeniuzia kama mmiliki wa kiwanja hicho.
Ninaomba maafisa Ardhi Halmashauri ya Jiji la Mwanza wawajibike ipasavyo kutekeleza majukumu yao.
Msajili wa hati alikamilisha kunisajili mimi kwenye hati Mwaka 2024 lakini maafisa Ardhi ambao wanapaswa kubadlisha taarifa hizo kwenye mfumo hawajabadilisha mpaka sasa.
Inavyoonekana hawajabadilisha title za watu wengi walionunua kwenye mfumo, nilisikia pia Mzee mmoja akiuliza iweje bado bill inasoma jina la mmiliki wa zamani. Mimi ilipodika zamu yangu kuona kama imeshabadilika nikakuta ni vilevile kama mwaka jana. Kwahiyo kuna hilo tatizo sasa ni changamoto gani hiyo isiyoweza kutatuliwa miaka miwili?