Jikosoe udhaifu wako [Thread]

Boss Nina shida apa inataka kunitoa roho...fanya jambo
 
Sipendi watu wajue undani wangu, yaani kuna times hata wife sitaki ajue undani wangu, napenda kuficha issues zangu. Nikiona mtu wangu wa karibu kama wife anahadithia mambo yake kwa mtu tu nakuwa so irritated, nakasirika kabisa.
 
Huo sio udhaifu mkuu, hiyo ni roho nzuri kabisa
 
1: Ninajali amani ya nafsi yangu (inner peace) sanaaa ile sana nimepitiliza, kiasi kwamba mtu au kitu kinachoingilia hii amani nitajiepusha tu, inanicost baadhi ya mambo, vitu vya msingi natakiwa kufanya ila kwakua ndo sina amani navyo naviacha, naacha vitu naacha watu.

2: huwa sijipi umuhimu kwa mtu, kama unaona sina umuhimu napaki pembeni, sijipi umuhimu kwa mzazi, kwa mme, kwa ndugu hata kazini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…