Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Daima mwanzo huwa mgumu sana na mvumilivu hula mbivu.
Ndio maana yule rais wa PORTLAND mambo ya wapinzani hapendi hata kuyasikia kumbe alishaonjeshwa shubiri.
Kumbe majimbo haya hugawanywa ki mkakati !!
Mbona yeye anawaambia wenzake waroho wa madaraka yeye kashindwa Mara mbili bado anagombea tu alikuwa anatafuta nini!
Bila kufanya hivyo Kigwangala asingetoboa kwa Bashe.
Tatizo la biharamulo ni wakaazi wake wengi wao ni watu wa kuja na kuondoka hasa ukizingatia kuwa ni wanyarwanda na wazinza na wahangazaKabuye ndio alimbwaga jembe Kasusura (mbunge wa biharamulo )miaka mingi sanaa.
Ila biharamulo kwaa nini haipigi mbele kimaendeleo?.
Maoni yangu ni kwamba Magufuli ni mstaarabu sana. Akishindwa anakubali matokeo na kusubiri zamu ijayo.
Hata wewe kapambane mara nyingi uwezavyoMbona yeye anawaambia wenzake waroho wa madaraka yeye kashindwa Mara mbili bado anagombea tu alikuwa anatafuta nini!
Sahihi kabisaBila kufanya hivyo Kigwangala asingetoboa kwa Bashe.
Kwa hiyo Biharamulo kuna wasukuma na wazinza?? Na huu usukuma wa Magufuri unatokea wapiBiharamulo tangu na tangu ipo Kagera
Mungu akitaka lake hutumia NJIA yoyote anayo I penda
Acha kutukumbusha siasa za wazinza tuko wachache tujuane slogan iliyotumiwa Sana na Marehemu Kabuye
UCHAGUZI WA UBUNGE JIMBO LA BIHARAMULO
Mnamo Mwaka 1985 Mwalimu wa Kemia shule ya sekondari Sengerema John Pombe Magufuli aligombea ubunge wa jimbo la Biharamulo akichuana na Mkulima Phares Kabuye. Kabuye alishinda na kutangazwa Mbunge, na Mwalimu Magufuli akarudi Sengerema kufundisha.
Mwaka 1990 Mwalimu Magufuli alichuana tena na Mkulima Kabuye kwa mara ya pili. Kabuye alimshinda tena Magufuli na kutetea kiti chake.
Mwaka 1995 wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi, jimbo la Biharamulo liligawanywa na kupatikana majimbo mawili (Biharamulo Magharibi na Mashariki). Kabuye aligombea Magharibi akashinda. Magufuli nae akagombea Mashariki na kushinda kwa mara ya kwanza baada ya mpinzani wake wa muda mrefu kwenda magharibi. Baadaye jimbo la Biharamulo Mashariki lilibadilishwa na kuitwa Chato.
Miaka kadhaa baadaye Phares Kabuye alifariki kwa ajali Morogoro. RIP Phares Kabuye. "Bila kuigawa Biharamulo mara mbili nadhani sasa hivi John Pombe Magufuli angekuwa mwalimu mstaafu"
Nini maoni yako?
Source: Daniel Matipa
Haha kwan Kagera nzima huishi Wahaya pekee au mkoa utokako lipo kabila lenu tuKwa hiyo Biharamulo kuna wasukuma na wazinza?? Na huu usukuma wa Magufuri unatokea wapi
Ninavyo elewa Kagera ni wahaya na wanyambo, na wahangazaHaha kwan Kagera nzima huishi Wahaya pekee au mkoa utokako lipo kabila lenu tu
Kuna tofauti gani hapo sasa... mwisho wa siku zote zinaishia kupata uongozi...Yeye alikuwa utumishi wa umma hakuwa serkali kuu
Inategemea wewe mungu wako ni yupiMungu Bahari au