Jikumbushe mpambano wa Ubunge kati ya Mwl. na Mkemia Magufuli na Mkulima Phares Kabuye

Jikumbushe mpambano wa Ubunge kati ya Mwl. na Mkemia Magufuli na Mkulima Phares Kabuye

Mimi mzaramo baba tuko Mkuranga
Mkuu acha hizo mambo tuchape kazi na uzur kumbe Mh. Raisi kapambana sana kwenye siasa toka 1985 twice alikosa ubunge bado akapambana then leo ndio Rais wetu kwa hiyo mambo ya kabila lake sio ishu
 
Hiyo I'd yako tu inatosha
Vipi Mkuu? Kulikoni kwenye ID yangu? Mwalimu Magufuli alishindwa na mkulima na akaridhika kwamba ameshindwa kihalali. Hivyo akakubali matokeo na kusubiri zamu nyingine. Hakuleta manenoneno yasiyokuwa na kichwa wala miguu. Wito wangu ni kwamba hao wanaojimwambafai kutaka kushindana na jabali hilo hapo Oktoba nao wawe tayari kukubali matokeo kama alivyoonyesha Magufuli hapo nyuma.
 
Kwa nini tusimtafute "Mkulima" apambane na Magufuli hapo Oktoba; inaonekana 'Wakulima' wanamuweza sana, hapigi raundi mbele yao.

Yule 'mkulima' wa ndege hadi leo anatabasamu tu!
Hhahahahahahahahh!!!
 
ID yako inatosha kutafsiri ulicho kiandika
Vipi Mkuu? Kulikoni kwenye ID yangu? Mwalimu Magufuli alishindwa na mkulima na akaridhika kwamba ameshindwa kihalali. Hivyo akakubali matokeo na kusubiri zamu nyingine. Hakuleta manenoneno yasiyokuwa na kichwa wala miguu. Wito wangu ni kwamba hao wanaojimwambafai kutaka kushindana na jabali hilo hapo Oktoba nao wawe tayari kukubali matokeo kama alivyoonyesha Magufuli hapo nyuma.
 
Hawa wanasiasa successful wengi wamepitia vitasa na rejections sana tu.
 
UCHAGUZI WA UBUNGE JIMBO LA BIHARAMULO
Mnamo Mwaka 1985 Mwalimu wa Kemia shule ya sekondari Sengerema John Pombe Magufuli aligombea ubunge wa jimbo la Biharamulo akichuana na Mkulima Phares Kabuye. Kabuye alishinda na kutangazwa Mbunge, na Mwalimu Magufuli akarudi Sengerema kufundisha.

Mwaka 1990 Mwalimu Magufuli alichuana tena na Mkulima Kabuye kwa mara ya pili. Kabuye alimshinda tena Magufuli na kutetea kiti chake.

Mwaka 1995 wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi, jimbo la Biharamulo liligawanywa na kupatikana majimbo mawili (Biharamulo Magharibi na Mashariki). Kabuye aligombea Magharibi akashinda. Magufuli nae akagombea Mashariki na kushinda kwa mara ya kwanza baada ya mpinzani wake wa muda mrefu kwenda magharibi. Baadaye jimbo la Biharamulo Mashariki lilibadilishwa na kuitwa Chato.

Miaka kadhaa baadaye Phares Kabuye alifariki kwa ajali Morogoro. RIP Phares Kabuye. "Bila kuigawa Biharamulo mara mbili nadhani sasa hivi John Pombe Magufuli angekuwa mwalimu mstaafu"

Nini maoni yako?

Source: Daniel Matipa
Duuh..hii kweli kareee..hakuna kukataa tamaa
 
Enzi hizo kuwa mkulima ilikuwa sifa. Ilikuwa nchi ya wakulima na wafanyakazi (Jembe na nyundo - kwenye bendera ya CCM). Hakukuwa na wafanyabiashara. Walikuwepo lakini kwa sababu za kisiasa hawakutambulika. Wafanyabiashara wote walichukuliwa kama mabepari/mabeberu. Kwa hiyo wafanyabiashara wa wakati huo walijiita wakulima ili kwenda na wakati. Ajabu leo wafanyabiashara ndio wanatoa pesa za kampeni za CCM!
Kabuye alikuwa machachari sana sana pia. Hapa nashangaa kumbe alikuwa Mkulima!
 
Toka jimbo la Chato lianzishwe Magufuli hakuwahi kuwa opposed na vyama vingine kwa kufanya figisu figisu wakati wa mchakato hivyo alikuwa akipita bila kupingwa tu.

Ndiyo maana hata kufanya siasa hawezi maana kazoea vya kunyonga
Mwaka 2015 Mkulima mwingine wa CCM kutoka hukohuko alichukua Fomu ya kugombea Urais na alishiriki kwenye kampeini na kufanya vizuri sana mpaka mwisho kwa gharama zake mwenyewe. Bahati mbaya alitupwa Nje baada ya vikao vya Chama vya kupendekeza wagombea kwa sababu hakuwa na mtu mashughuli wa kumbeba. Utaratibu wa CCM uliozoeleka wa kubeba wagombea kwenye mbeleko unatukosesha viongozi wazuri wenye uwezo kama ilivyokuwa kwenye Uchaguzi wa mwaka huo maana hata akina mama wawili waliofikia hatua ya mwisho ya uteuzi walikuwa wanauwezo mkubwa sana lakini walitupwa nje kwa sababu hizohizo.
 
Toka jimbo la Chato lianzishwe Magufuli hakuwahi kuwa opposed na vyama vingine kwa kufanya figisu figisu wakati wa mchakato hivyo alikuwa akipita bila kupingwa tu.

Ndiyo maana hata kufanya siasa hawezi maana kazoea vya kunyonga
Kwahiyo ata kijiji na kitongoji kwake kilikua chini ya Upinzani! Hii sauti ni kali sana
 
Sasa Kwanini results zisimbebe?
Hana ujuzi wa kujenga hoja kifasaha na watu wakazikubali; he is a bulldozer hivyo hutumia nguvu na sio ushawishi!! Hajui kushawishi hivyo anabebwa na dola!!!
 
UCHAGUZI WA UBUNGE JIMBO LA BIHARAMULO
Mnamo Mwaka 1985 Mwalimu wa Kemia shule ya sekondari Sengerema John Pombe Magufuli aligombea ubunge wa jimbo la Biharamulo akichuana na Mkulima Phares Kabuye. Kabuye alishinda na kutangazwa Mbunge, na Mwalimu Magufuli akarudi Sengerema kufundisha.

Mwaka 1990 Mwalimu Magufuli alichuana tena na Mkulima Kabuye kwa mara ya pili. Kabuye alimshinda tena Magufuli na kutetea kiti chake.

Mwaka 1995 wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi, jimbo la Biharamulo liligawanywa na kupatikana majimbo mawili (Biharamulo Magharibi na Mashariki). Kabuye aligombea Magharibi akashinda. Magufuli nae akagombea Mashariki na kushinda kwa mara ya kwanza baada ya mpinzani wake wa muda mrefu kwenda magharibi. Baadaye jimbo la Biharamulo Mashariki lilibadilishwa na kuitwa Chato.

Miaka kadhaa baadaye Phares Kabuye alifariki kwa ajali Morogoro. RIP Phares Kabuye. "Bila kuigawa Biharamulo mara mbili nadhani sasa hivi John Pombe Magufuli angekuwa mwalimu mstaafu"

Nini maoni yako?

Source: Daniel Matipa
Alilopanga Mola! Kwa vyovyote vile au njia yoyote angekuwa hivi alivyo leo. Huenda humjui Mungu na njia zake.
 
Back
Top Bottom