Jimbo la arusha mjini na monduli yagawanywe

Jimbo la arusha mjini na monduli yagawanywe

Hivi Freddy anafanya nini Monduli? Anakubalika?
 
We unatumia nini kufikiri

Kinachohitajika ni kuongeza Mbunge au kugawa jimbo au kufanya high Badget Allocation.?

Ikiwa jimbo lina idadi kubwa ya watu kinachohitajika ni kuandaa bajeti inayoendana na ukubwa wa jimbo na sio kuligawa jimbo .

Kuligawa jimbo ni kuiongezea serikali mzigo mkubwa kwa walipa kodi.

So kinachohitajika hapo ni matumizi ya akili na sio hizo fikra mgando
Mkuu umewaza kwa maslahi mapana ya Taifa.
 
Jimbo la Arusha mjini limekuwa na ongezeko kubwa la watu. Itapendeza kama litagawanywa. Hii ni kwa sababu ktk muda mfupi sana uliopita,kumekuwa na kuzaliwa kwa mitaa mipya mingi ambayo inahitaji uwakilishi bungeni. Mfano mzuri ni eneo naarufu la kwa Mrombo ambalo liko busy sana kiuchumi na lina ongezejo kubwa sana ya watu. Hata taasisi za kibenki kadhaa zimeweka Malawi yake eneo husika.

Kwa spande wa jimbo la Monduli,linapaswa pia kugawanywa. Kuna ukuaji mkubwa sana kwa eneo maarufu la Mto wa Mbu ambapo kuna shughuli nyingi za kiuchumi na kijamii zinaendelea kufanyika kwa kasi sana. Eneo lote la Kigongoni amabalo ni sehemu ya Mto wa Mbu nalo linakua kwa kasi sana.
Haya majimbo naomba badala yakugawanywa ni ya unganishwe tu maana mjengoni pangekuwa kijiwe cha vilaza.
 
Kwanza kabisa, mimi ningetamani sanaa kila Mbunge anayehitimisha kipindi chake kwenye jimbo husika, angeandika taarifa fupi na ya kueleweka kwa wananchi wa jimboni kwake. Aelezeee ni mambo yepi aliahidi kuyasemea bungeni na kuyapigania kwa ajili ya wananchi wake, na katika hayo ni mangapi yamefanyika kikamilifu, angalau kuna hatua ya utekelezaji umeanza na ushahidi angalau wa picha, na ambayo hakufanikiwa hata kuyaanza. Aidha aelezee pia tangu ameingia bungeni ameweza kutoa mchango gani ambao yeye anadhani umelisaidia taifa. Nadhani hii ni mbinu nzuri pia ya kupiga kampeni kwa urahisi. Kuliko kila baada ya miaka 5, wanapanda jukwaani wanaanza tena kupiga siasa!
Yangu ni hayo, muhimu tukumbuke kufuata maelekezo ya wataalam wa Afya kwani mgeni tuliyekuwa tukimsikia huko kwa majirani tayari ameshaingia hapa nyumbani na ameshakutana na baadhi ya ndugu zetu. Ni huzuni sanaaa.(Hapa nazungumzia Mpox)
 
arusha population ipo chin yani ni ndogo. mkoa mkubwa ila idadi ya watu ndogo. kuwa na wabunge wengi ni itakua hasara
Arusha jiji Lina watu wengi kuliko mbeya jiji sensa ya 2022 kama mbeya inagawanywa kwanin Arusha ambayo Ina watu wengi zaidi isigawanywe hufikirii
 
IPo siku Mungu atasikia kilio cha watanganyika.

Atafuta machozi ya watanzania.
 
Jimbo la Arusha mjini limekuwa na ongezeko kubwa la watu. Itapendeza kama litagawanywa. Hii ni kwa sababu ktk muda mfupi sana uliopita,kumekuwa na kuzaliwa kwa mitaa mipya mingi ambayo inahitaji uwakilishi bungeni. Mfano mzuri ni eneo naarufu la kwa Mrombo ambalo liko busy sana kiuchumi na lina ongezejo kubwa sana ya watu. Hata taasisi za kibenki kadhaa zimeweka Malawi yake eneo husika.

Kwa spande wa jimbo la Monduli,linapaswa pia kugawanywa. Kuna ukuaji mkubwa sana kwa eneo maarufu la Mto wa Mbu ambapo kuna shughuli nyingi za kiuchumi na kijamii zinaendelea kufanyika kwa kasi sana. Eneo lote la Kigongoni amabalo ni sehemu ya Mto wa Mbu nalo linakua kwa kasi sana.
Kigongoni
Napajua kona ya kwa babu samuge
 
Back
Top Bottom