KERO Jimbo la Lupa-Chunya limetawaliwa na CCM tangu uhuru, halina barabara ya lami hata nusu kilometer

KERO Jimbo la Lupa-Chunya limetawaliwa na CCM tangu uhuru, halina barabara ya lami hata nusu kilometer

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Ukweli Tanganyika ni nchi ngumu.
Jimbo la lupa lililopo chunya, halina hata nusu Kilomita ya Barbara ya Lami.

Na Cha kufurahisha mbunge wake Yuko bungeni na anatarajia kurudi kuomba kura tena, ili aendelee kuwa mbunge wa Lupa.

Ninashauri CCM itusaidie kumuondoa mbunge wa sasa, itupatie mtu anayeelewa wananchi wanachokitaka.

Cha kufurahisha zaidi hata maji safi na salama hayapo, Jimbo nzima
Kwa hiyo jimbo hilo lilikuwepo tangu enzi za Tanganyika?
Wanafunzi bwana hata Historia hamsomi?
 
View: https://youtu.be/4wHLqWVzVkg?si=bEWy5qMPpybs2Vuq
Huyu hapa. Huku umaskini unauwa watu.
Mkutano unakofanyikia magari yanapita,yakitimua vumbi.
Huo ukoo, unatakiwa uondolewe haraka

Inawezekana kabisa wewe ndiye Dr Matayo unayejipigia debe. Maana si kwa kumchukia Kasaka huko.

BTW! Uje wewe, aje nani sidhani kama kutakuwa na mabadiliko kama Serikali imeamua kujitenga na Jimbo la Lupa, Serikali imevaa miwani ya Mbao, na kuweka pamba masikioni kuhusu Jimbo la Lupa.

Mara ngapi tumekuwa tukiwasikia viongozi wakubwa wa Serikali wakitoa ahadi hewa za Ujenzi wa Barabara hiyo (Makongolosi - Rungwa) Kwa kiwango Cha lami? Inawezekana hata Kasaka na Mwambalasya walipaza sauti zao mpaka vinywa vyao vikakauka.
Kwa hiyo, Serikali ndiyo mwamuzi wa mwisho katika hatua za ujenzi.
 
Jimbo la Lupa ni changamoto, kubwa.
Hakuna miundombimu ya maji Wala madaraja Wala Barbara.

Ndio sababu tumeliibua humu Jf.
Kila dalili ccm isimpotishe kasaka kugombea ubunge Lupa.

Hani ni mbaya, hata watumishi wa imma Lupa hawapo.
 
Mbunge wa Jimbo la Lupa Mhe Masache Njeru Kasaka amewataka wananchi wa jimbo la Lupa waendelee kuiamini serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwani mpaka sasa imeendelea kutekeleza ahadi zote zilizoahidiwa mwaka 2020 na bado inaendelea kutekeleza.

Ametoa kauli hiyo leo tarehe 05/10/2023 wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nkwangu kwanza kuwapa mrejeso kuhusu Bunge la bajeti na kueleza shughuli mbalimbali zilizofanyika na ambazo zinaendelea kufanyika pamoja na kusikiliza kero za wananchi hatimaye kuzipatia suluhu kero hizo.

“Mimi na viongozi wenzangu hatujawaangusha na hatutawaangusha maana tukiwaangusha maana yake tumemwangusha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Mama Samia Suluhu Hassan jambo ambalo sisi watumishi wenu mliotutuma kuwasemeeni maeneo mbalimbali hatuwezi kufanya hivyo maana hata ninyi ni mashahidi kwamba ahadi tulizo ahidi tunaendelea kuzitekeleza”.

Akijibu kero mbalimbali za wananchi Mhe Mbunge amesema Wilaya ya Chunya imetengewa fedha zaidi ya Milioni mia nane kwaajili ya kununua vifaa tiba kwa mwaka huu wa fedha 2023/2024 hivyo Zahanati ya kijiji cha Nkwangu itakuwa ni moja kati ya wanufaika wa vifaa hivyo ili wananchi waendelee kupata huduma katika zahanati hiyo huku akiwata viongozi kuwapa mrejesho wananchi kuhusu fedha za maendeleo zinazoletwa na hata michango ya wananchi.

“Hakikisheni wananchi wanapata taarifa ya fedha za serikali zinazoletwa kujenga miradi mbalimbali pamoja na fedha zinazotokana na michango yao ili kuepuka usumbufu kwani wananchi wamekuwa wakilalamika kwamba wanachaga fedha lakini hawaoni kilichofanyika lakini ukifuatilia unakuta fedha hizo zimefanya mambo mazuri lakini wananchi hawajui”.

Diwani wa kata ya Upendo Mhe. Mh. Richard N. Itelekelo amemshukuru Mhe Mbunge kwa namna ambavyo ameendelea kuwa mstari wa Mbele kuwapigania wananchi wa wilaya ya Chunya hasa kata ya Upendo kwani miradi mbalimbali kama vile uchimbaji wa visima, ujenzi wa shule ya sekondari, ujenzi wa zahanati na mingine mingi inatekelezwa katika kata ya Upendo kwa fedha kutoka serikalini.

Awali akisoma taarifa kwa niaba ya wananchi mbele ya Mbunge wa jimbo la Lupa Mtendaji wa kijiji cha Nkwangu ndugu Andrew Msoya amesema kijiji kinakabiliwa na Chnagamoto mbalimbali zikiwepo Barabara, kukosekana kwa mawasiliano, Nyumba za watumishi waliopo katika kijiji hicho, vifaa tiba katika zahanati hiyo pamoja na vitanda na Friji la kutunzia chanjo kwaajili ya watoto jambo ambalo husababisha watoto wanaostahili kupata chanjo kukosa chanjo hiyo hivyo kuhatarisha maisha yao.

Mbunge wa jimbo la Lupa yupo katika Ziara yake ya kawaida kuwatembelea wananchi ili kuwapa mrejeso wa bunge la Bajeti lililotamatika mwezi juni, kusikiliza kero za wananchi na kutafuta suluhu na kueleza namna ambavyo serikali inaendelea kutekeleza majukumu yake ili kuleta maendeleo kwa wanachunya wakiwepo wananchi wa kijiji cha Nkwangu. Ziara hiyo itaendelea kesho tarehe 8/10/2023 kwa kata ya Mkola.
 
Aliyewahi kufika Lupa Tinga tinga tunaomba utupatie ushuhuda wake.

Hali ya miundombinu ya Barbara, maji na umeme ikoje???
 
Nimezaliwa na kukulia Lupa. Ni kweli hali ya upatikanaji wa maji, barabara bado ni changamoto japo imeimarika zaidi tofauti na miaka ya nyuma. Mfano barabara ya lami imejengwa mpaka Makongorosi,pia Kulikuwa na mradi wa maji Matwiga,sijui umefikia wapi!
 
Ukweli Tanganyika ni nchi ngumu.
Jimbo la lupa lililopo chunya, halina hata nusu Kilomita ya Barbara ya Lami.

Na Cha kufurahisha mbunge wake Yuko bungeni na anatarajia kurudi kuomba kura tena, ili aendelee kuwa mbunge wa Lupa.

Ninashauri CCM itusaidie kumuondoa mbunge wa sasa, itupatie mtu anayeelewa wananchi wanachokitaka.

Cha kufurahisha zaidi hata maji safi na salama hayapo, Jimbo nzima
Na Bado tu mnawataka CCM ....aliyewaroga ameokoka ....
 
Ukweli Tanganyika ni nchi ngumu.
Jimbo la lupa lililopo chunya, halina hata nusu Kilomita ya Barbara ya Lami.

Na Cha kufurahisha mbunge wake Yuko bungeni na anatarajia kurudi kuomba kura tena, ili aendelee kuwa mbunge wa Lupa.

Ninashauri CCM itusaidie kumuondoa mbunge wa sasa, itupatie mtu anayeelewa wananchi wanachokitaka.

Cha kufurahisha zaidi hata maji safi na salama hayapo, Jimbo nzima
Wewe kweli hamnazo, CCM haimuondoi Mbunge bali nyie wapiga kura mnaohongwa chumvi na vitenge ndo wenye uwezo wa kumuondoa kupitia sanduku la kura
 
Back
Top Bottom