Sasa hapa tatizo ni mbunge au serikali yenye jukumu la kujenga barabara hizo..?
By the way huko wilayani na mkoani si kuna wawakilishi wa Rais/serikali moja kwa moja kama RC, DCs, Wakurugenzi wa Halmashauri, TANROAD, TARURA? Kwanini usiwalaumu hao moja kwa moja maana ndiyo wenye mafungu ya fedha zote za maendeleo? Why mbunge?
Mbunge ana fedha za kuweka wakandarasi wajenge barabara kwani?
Sawa. Najua unaweza kuniambia, anatakiwa kusema huko bungeni...
Ndugu muwe mnaelewa tunaposema tatizo la mkwamo wa maendeleo ya nchi hii ni mfumo mbovu wa kiutawala na kikatiba ambao power & authority ya mambo yote yakiwemo ya kifedha yako centralized kwa Rais na Central Government DSM au Dodoma...!
Mbunge unaweza kusema mpaka povu likakutoka na mpaka ukaruka na sarakakasi ndani ya bunge au kwenye ofisi ya waziri wa barabara, lakini kama mwenye fedha (Rais) hataki, huwezi kupata chochote...
All in all, tatizo la miundombinu ya barabara liko nchi nzima. Barabara nyingi za lami na vumbi hazifanyiwa regular maintainance muda mrefu sana....
Mfano leo hii mimi nimepita barabara ya lami ya kutoka Musoma - Lamadi - Bariadi - Maswa hadi Shinyanga. Barabara ni ya lami lakini imebomoka na kuwa na mashimo ya hatari yanayosababisha ajali za mara kwa mara na TANROAD wa maeneo haya wanaangalia tu...
Kuna sehemu shimo la kwenye barabara ya lami, TANROAD wameleta kifusi cha moramu kuziba badala ya lami izibwe kwa lami. Unadhani hii inaashiria nini? Hawana hela au fedha ya matengenezo imeliwa na wajanja...??
Kuna miradi ya ujenzi wa barabara imesimama kwa muda mrefu, haiendelei. Wakandarasi wamechimba mashimo na kumwaga vifusi baada ya hapo wameziacha hivyohivyo, wamekimbia. Wakiulizwa, jibu ni kuwa serikali haiwalipi fedha na wanashindwa kuendeleza kazi...
Sasa hili ni tatizo la mbunge mmoja mmoja kweli au ni tatizo la mfumo mzima wa serikali ambao uko corrupted..??