Jimbo la Tigray Ethiopia limeonesha ubaya wa utawala wa majimbo Tanzania

Jimbo la Tigray Ethiopia limeonesha ubaya wa utawala wa majimbo Tanzania

Kiongozi mwenye akili timamu hawezi kukubali nchi yake ikagawanyika hata mita moja
 
Kwahiyo hayo makabila ambayo hujayataja ndiyo yanapinga kiswahili kuwa lugha ya taifa ?
Makabila hayo yamejitahidi kuandika hata bibilia za kilugha. Wanakifananisha kiswahili na uislam na uarabu zaidi, ni Mzee nyerere aliyesimama kidete kukikuza na kukieneza kiswahili nchini kwa juhudi kubwa. Hata Ethiopia waoromo ndilo kabila kubwa sana, hawataki kiamharic kiwe lugha taifa, badala yake wangetaka kioromia kiwe lugha ya taifa. Lakini amhara ndiyo lugha pekee afrika ambayo ina alphabets zake yenyewe.
 
Mtoa mada naona una akili ndogo sana katika maswala ya kimataifa, mkiwa huko ccm mnakaririshwa tu kama kasuku na kwa sababu ya udikteta hamruhusiwi kuhoji chochote.

Migogoro iliyopo katika mataifa mbalimbali duniani chanzo sio mfumo wa utawala wa shirikisho.

Marekani kabla hawajaanzisha mfumo wa shirikisho walipigana vita vikali sana wenyewe kwa wenyewe hadi walipoanzisha mfumo wa Federation na hadithi ilikuwa ni hiyo hiyo kwa Nigeria.

Ukiangalia chanzo cha tawala za kiimla ni huu mfumo wa utawala wa serikali kuu (Unitary System of Government) ambapo nchi inakuwa na Imperial President kama ilivyo hapa Tanzania na matokeo yake tunaona sasa tulivyo na utawala wa kidikteta.
Utawala wa kidikteta unatoka kwenye katiba ambayo mnaiandika wenyewe. Mtu akiitekeleza katiba hiyo kama ilivyo kosa ni lanani? Ukiangalia wapinzani badala ya kuangalia masuala ya msingi ya katiba wanahangaika na aina ya Muungano. Mchakato wa kuiandika katiba ulivurugwa na UKAWA kwa kulazimisha muungano wa mkataba kwenye katiba.
 
una hoja mfu kabisa;
Kuhusu Etjiopia na Tigrey upo sawa kabisa ila mfano uliotoa kuhusu WAsukuma na Wachagga ni wa KI-MATAGA, tena ambaye aliishia form four na kupata ZERO kama BASHITE.

WAkoloni walipokuja Tanzania walikwenda kwenye maeneo ya Kaskazini, Kilimanjaro , Tanga na Arusha{Wajerumani na Waingereza}, Pwani ikiwa na Waarabu n a Wahindi.
Kwakuwa walikaa kaskazini kueneza dini, basi walijenga makanisa, hospitali, na shule huku wakijenga barabara kufikia maeneo hayo.
Mahospitali kama KCMC-inmejengwa na Mjerumani- Kanisa la Luthran, Muhimbili ni Waingereza, Hydom ni wajerumani, Mount Meru Lutheran -wajerumani, na zinajengwa kabla ya kupata uhuru 1961, sasa sijui unafikiri tupo korido za Lumumba kudaanganya watoto wenzio?

shule kama Tanga Technical, Kifungilo, Ashira, Weruweru, Moshi Technical ,Old Moshi, Maua Semiary, Uru Seminary, Kibosho Girls, Ashira, Maranbgu Secondary, Ilboro, Arusha SEcondary , Mawenzi SE-Moshi na nyingine nyingi.
Wachaga wajaokoka na kuwa wakristo, kumpa Yesu maisha yao, wakaachana na uchawi na dini za asili wakati hilo kabila ulilosema lina robo ya Tanzania lina Uchawi, kuua albino na kila aina ya Gambosh, watapata wapi maendeleo, ?
Hizo shuk
Nasikia hao mabeberu walijenga vyote hivyo kwa kuwa walijua wenyeji wana uwezo kuna maeneo walijua hata wakijenga ni kupoteza hela zao kwa kuwa wenyeji bado hawako tayari kwa uelewa.
 
Makabila hayo yamejitahidi kuandika hata bibilia za kilugha. Wanakifananisha kiswahili na uislam na uarabu zaidi, ni Mzee nyerere aliyesimama kidete kukikuza na kukieneza kiswahili nchini kwa juhudi kubwa. Hata Ethiopia waoromo ndilo kabila kubwa sana, hawataki kiamharic kiwe lugha taifa, badala yake wangetaka kioromia kiwe lugha ya taifa. Lakini amhara ndiyo lugha pekee afrika ambayo ina alphabets zake yenyewe.
Sidhani ni sahihi kulinganisha ukabila tanzania na sehemu nyengine nyingi africa (hata na asia) bibilia za kilugha ziliandikwa si na makabila fulani, maana hamna tawala za kikabila zenye nguvu na zilizo centralized kufanya hivyo kwa sasa, ilikuwa hivyo kabla ya uhuru. Kiswahili katika jamii yetu iliyona shule kila kata hakina taswira ya udini au ukanda, wala watanzania hawana mrengo huo
 
Du! Maskini hujui kwanini Tigray inapigana na central governement. Wewe unadhani ni majimbo. Ndugu jiongeze
Najuwa unataka kujuwa lakini unaona aibu kuniuliza.

1. Hawataki kupoteza autonomous
2. Hawataki uislam, Maana wanadhani Abiy ni muislam
3. Hawataki uhusiano na Eritrea
4. Wanajiona chimbuko halisi la Ethiopia
 
USA ni mfano mzuri wa majimbo. Watu waache upumbavu wa kushambulia sera sababu hazitoki CCM.
 
Jimbo la Tigray Ethiopia kuna vita wanasiasa wakora wanataka kujitenga, jimbo la Kaduna kule Nigeria wakora wanataka kujitenga, kule Kabregado Msumbiji wanataka kujitenga, Katalunha Hispania wahuni wanataka kujitenga.

Kumbe hata Tanzania tukianzisha utawala wa majimbo huenda kutakuwa na majimbo ambayo yanaweza kutamani kujitenga kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kiuchumi, kikabila, kidini na za kilevi tu. Maana zipo dini, makabila ambayo yana malalamiko yao hadi sasa.

Mfano, yako makabila makubwa yanayohoji kwanini Kiswahili kiwe lugha ya taifa.

Nadhani tuko sahihi bado mpaka sasa kuwa hivi tulivyo, tuboreshe tu mapungufu.
Mfano wa pili ni Marekani majimbo yana shida gani?
 
Utawala wa kidikteta unatoka kwenye katiba ambayo mnaiandika wenyewe. Mtu akiitekeleza katiba hiyo kama ilivyo kosa ni lanani? Ukiangalia wapinzani badala ya kuangalia masuala ya msingi ya katiba wanahangaika na aina ya Muungano. Mchakato wa kuiandika katiba ulivurugwa na UKAWA kwa kulazimisha muungano wa mkataba kwenye katiba.
Katiba hii ya mwaka 1977 iliandikwa na wananchi gani au ulikuwa haujazaliwa.

CCM walivuruga mchakato wa katiba mpya kwa kuogopa kuacha kulindwa na dola.
 
Un
New York na WAshington vipi, wameonyesha uzuri?

yaani MATAGA na CCM huwa mnatabia kama za nzi wa kijani, mnatafutaga ka-mfano kamoja tu , kudhihirisha ufedhuli wenu.
Duniani nchi nyingi zina utawala wa majimbo, na zimefanikiwa sana mfano Ujerumani, Uingereza, Marekani, Urusi, china , Australia, etc, huko vipi ?
Unajua katiba ya USA inasemaje mtu akizungumzia kujitenga?
 
Nasikia hao mabeberu walijenga vyote hivyo kwa kuwa walijua wenyeji wana uwezo kuna maeneo walijua hata wakijenga ni kupoteza hela zao kwa kuwa wenyeji bado hawako tayari kwa uelewa.
Sio kweli, mara nyingi walijenga kule kwenye hali ya hewa inayokaribia kufanana fanana na kwao ulaya
 
Jimbo la Tigray Ethiopia kuna vita wanasiasa wakora wanataka kujitenga, jimbo la Kaduna kule Nigeria wakora wanataka kujitenga, kule Kabregado Msumbiji wanataka kujitenga, Katalunha Hispania wahuni wanataka kujitenga.

Kumbe hata Tanzania tukianzisha utawala wa majimbo huenda kutakuwa na majimbo ambayo yanaweza kutamani kujitenga kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kiuchumi, kikabila, kidini na za kilevi tu. Maana zipo dini, makabila ambayo yana malalamiko yao hadi sasa.

Mfano, yako makabila makubwa yanayohoji kwanini Kiswahili kiwe lugha ya taifa.

Nadhani tuko sahihi bado mpaka sasa kuwa hivi tulivyo, tuboreshe tu mapungufu.
Hoja dhaifu sana kwa hiyo vita vya wenyewe kwa wenyewe vyote vilivyotekea duniani na kutaka kujitenga vimetokana na utawala wa majimbo.!!!!! Vita asilimia kubwa hutokana na vyama tawala kutotaka ushindani wa kisiasa na kuminya demokrasia na udikteta.
 
Tafuta historia ya Ethipioa utajua chanzo cha uasi wa sasa, Tafuta kwanini Mengistu alipinduliwa - huyu hakuwa rais wa jimbo alikuwa rais wa nchi nzima.
Msumbiji vita iliiyo kaskazini si ya kijimbo, ni ya kidini na inachochewa na umaskini wa watu. Umaskini huo umesababishwa na vita ya wao kwa wao baada ya kupata uhuru na mgawanyo usio sawa wa raslimali za Taifa nk. Inawezekana Msumbiji wangekuwa na utawala wa majimbo, jimbo la cabo delgado lingekuwa tajiri na hao jihadi labda wasingepata nafasi kwa urahisi
 
Sio kweli, mara nyingi walijenga kule kwenye hali ya hewa inayokaribia kufanana fanana na kwao ulaya

Inawezekana lakini kuna nchi ambazo walienda walikuwa wanaangalia na wenyeji pia Kuna watu hata ukiwajengea shule ni kazi bure. Kuna watu wako vizuri kwa nguvu lakini si akili na wao waliyaona hayo.
Walikuwa wanajua kuna watu wao ni kwa ajili ya nguvu kazi tu.
 
Tafuta historia ya Ethipioa utajua chanzo cha uasi wa sasa, Tafuta kwanini Mengistu alipinduliwa - huyu hakuwa rais wa jimbo alikuwa rais wa nchi nzima.
Msumbiji vita iliiyo kaskazini si ya kijimbo, ni ya kidini na inachochewa na umaskini wa watu. Umaskini huo umesababishwa na vita ya wao kwa wao baada ya kupata uhuru na mgawanyo usio sawa wa raslimali za Taifa nk. Inawezekana Msumbiji wangekuwa na utawala wa majimbo, jimbo la cabo delgado lingekuwa tajiri na hao jihadi labda wasingepata nafasi kwa urahisi
Issue ya Msumbiji ni tofauti kidogo. Kule kuna ubaguzi wa wazi, makabila ya Makhuwa na Makonde ndio yaliyopigana sana kwenye vita ya kumtoa Mreno lakini siku zote na mara zote viongozi wa nchi wanatoka kwenye kabila la Shangaan. Marais wote kutoka Mondulane, Masheli na waliofuata wanatoka kwa washangaan. Makhuwa na makonde wanahangaika na kilimo, uvuvi na sanaa, na wengi wao ni waislam. Hivyo Msumbiji kuna shida ya umaskini, udini, maendeleo, elimu na upendeleo wa madaraka kwenye jimbo lenye makonde na makhuwa wengi la Cabo delgado. Washangani na watsonga ndio wanaokula bata na kuwaacha hoi wale waliopigana kumuondoa mreno ambao wengi wao ni waislam, 20% ya wasumbiji wote.
 
Acha theory zako za uongo , wachagga na Wahaya wameishi kama state moja kabla ya kuja Kwa wakoloni , kasome historia vizuri , wahaya wote walikuwa chini ya chieftain moja chini ya omukama na wachaga chini ya Mangi na hawa wachaga walikuwa mpaka na fedha Yao na magazeti Yao kabla ya kuja mjerumani sasa kama ulikuwa hujui ndio ujue , wahaya walikuwa na Baraza la wawakilishi WA koo chini ya Omukama kabla ya kuja mjerumani ,

Acha propaganda za ajabu kama hujui historia fanya utafiti
Nani anawakataza kuchapisha magazeti yenu leo, nani anawakataza kulima ndizi nyingi leo. Hivi hiyo dola ya wachaga wenyewe ingekuwepo hadi leo hii wachaga wangekuwa wanaishi wapi na ardhi hakuna. Kwasababu ya uwepo wa unitary government na ardhi kuwa mali ya serikali ndio maana wachaga wamekamata ardhi kwenye majimbo ya watu wengine huko Morogoro, Dar salaam, kibaigwa. tanga katavi na kwingineko nchini. Chini ya serikali ya majimbo jambo kama hilo ingekuwa vigumu sana kutendeka.
 
Mkuu sina shaka na uelewa wako kuwa Ni mkubwa Ila katika hili hapo unadanganya umma au kwa makusudi au kea kuwa na wewe hujui. Mitano yote hapo uliyotaja ni tofauti na Hali ya Tanzania. Ugomvi wao sio wa kijimbo Bali ni kihistoria Zaidi.

Kama hujui Ni kuwa suala la kujitenga likija, hata Kama Sio Jimbo watu wa kagera Wana uwezo wa kutaka kuwa nchi huru isiyotegemea Tanzania na uwezo wa kujiendesha Kama nchi wanao.

Kwa hiyo mpaka uone hayo ujue Kuna mambo mengi chanzo sio Jimbo Bali ni historian na makabila.
Nadhani haujamwelea mtoa kwa mawazo yangu, ukiwa na mfumo wa majimbo kama kule Ethiopia jimbo lina mamlaka yake ya ndani kama vile utawala, mambo ya fedha na jeshi kwenye jimbo husika. Sasa watu kama hawa ni rahisi kutamani kujitenga kama wanajiona wako finencially enough huku wakiwa na jeshi kwani wanaamini kwa uwezo wao wa jeshi wanaweza kutingisha Federal government.

Hiyo ni tofauti watu kama wa kagera kutamani kujitenga kwa sababu zozote zile, kwa kundi la aina hii ni ngumu na inaweza kuwa ndoto isiyotekelezeka milele kwanini, mosi, hawana vyanzo vya mapato, hawana any administrative structure wala hawana vyanzo vya mapato. Kwahiyo kusema kwa Tanzania dhana ya kujitenga inaweza kuwepo lakini isiwe passive kama nchi ya Ethiopia.

Ni ukweli usiopingika kwa mataifa mengi ya Afrika kuwa na serikali ya Majimbo ni kujitengenezea njia za watu kutamani kujitawala aidha wakiwa wakiwa nia njema au nia ovu. Naweza kuelimishwa zaidi.
 
Back
Top Bottom